MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
- Thread starter
- #21
Wewe Generalist ni mshamba na muathirika wa neo colonialism, unaona kuongea kiingereza ni dili, kwani ngeli na kizaramu zina tofauti gani? Zote si lugha tu tunajifunza?
Ningeshangaa sana kama Uzi huu usingevamiwa na wasiokijua ' Kiingereza ' na najua mtajitokeza wengi tu.
Ninachojua tu ni kwamba duniani kuna Lugha nyingi na nzuri ila hakuna ambayo hadi hivi leo imeweza kuwa ni Kiungo ' Kikuu ' cha Mataifa yote duniani iwe Kiuchumi na hata Kidiplomasia kama cha Kiingereza.
Kama Mchina, Mrusi, Mjerumani na Mchina pamoja na Jeuri zao zote za kuwa ' Super Powers ' ulimwenguni na Lugha zao pia ni Kubwa lakini bado hao hao wanakizungumza Kiingereza Wewe Mpuuzi Mmoja wa Kiswahili usiye na mbele wala nyuma ni nani ukipinge?
Itatuchukua muda mrefu sana na huenda pia hata isitokee kwa Mataifa mengi duniani Kuachana na Lugha ya Kiingereza kwani kama kuna Mafanikio makubwa ambayo nchi ya Uingereza ilipata tokea Kipindi cha ' Colonialism ' ni kuhakikisha Lugha yao si tu inaendelea kutumika bali pia inapendwa na kuendelea Kuaminiwa na Vizazi na Vizazi.
Kama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere pamoja na kutowakubali Wazungu ( hasa kwa Sera zao na Matendo yao kwa Waafrika ) lakini Mwenyewe kwa Mdomo wake ( na Clips zipo Mitandaoni ) alikiri kuwa Kiingereza ni Lugha muhimu, siyo ya Kuepukwa duniani na ya Kibiashara zaidi.