Rais Samia Suluhu, Waganda wamekupigia 'Salute' kwa Kiingereza chako kizuri japo huna PhD yoyote

Rais Samia Suluhu, Waganda wamekupigia 'Salute' kwa Kiingereza chako kizuri japo huna PhD yoyote

Tafadhali bwana siyo thesis zote duniani zinaandikwa kwa kiingereza, na wala siyo presentations zote kwenye mikutano ya kimataifa zinafanywa kwa kiingereza.

Tafadhali tafadhali tafadhali .......... Wacuba ni katika taifa ambalo lina madaktari wazuri sana na wa kuaminika duniani lakini asilimia kubwa hawajui kiingereza, wao ni kispanish kwa kwenda mbele.
Ila za Tanzania ni lazima ziwe katika Kiingereza
 
Jana Usiku nilipokea Meseji moja kutoka kwa Rafiki mkubwa kutoka Uganda akielezea Kufurahishwa Kwake na 'Kiingereza ' kizuri alichonacho Rais wa Tanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan.

"Mr. Generalist are you sure that this President of yours Mama Samia she's not a Briton? She speaks fluent English, very articulate, attractive and comfortable with it unlike other so called intellectuals with their doctorates on hand "

Na Waganda hawakuishia hapa tu kwa huyu Rafiki yangu Kunitumia hiyo Meseji bali hata ukienda huko Ugandans On Twitter ( UOT ) Wachangiaji wengi wamevutiwa na Uwezo mkubwa wa Kuongea Kiingereza ' kilichonyooka ' cha Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.

Wameenda mbali zaidi na Kuhoji inakuwa Marais wengine (hasa Barani Afrika) wana Elimu Kubwa lakini walipokuwa wakiwasikiliza (wanapowasikiliza) huwa wanaongea Viingereza 'vibovu vibovu' tu wakati Makabatini mwao wamehifadhi Vyeti vya ' PhD ' zao.

Kongole sana Kwako Rais Mama Samia.
Tulikuwa tukiaibika sana.
 
Watu wanamsifia lugha. Badala ya kusifia dili ya bomba la mafuta. Hongera JPM
 
Sawa, kasoro tu alikosea matamshi sahihi ya "invitation" na "demise"
hapana, Samia anajua kiingereza, sio kama wengine wale. anakifahamu na alishafanya kazi katika organisation ya kimataifa. sawa tu na polepole, hajaishi ulaya ila ile kufanya kazi na wazungu kwenye maNGO anao uwezo mkubwa sana kujieleza kwa kiingereza. so is Samia.
 
Tunaacha kutumia Kiswahili tunashangilia lugha ya wakoloni.
"Kiingereza ni Kiswahili cha dunia," aliwahi kusema Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kama Kiswahili kilivyotuunganisha Watanzania, hivyo hivyo Kiingereza kimeiunganisha Dunia nzima.

Hakuna taifa duniani hapa ambalo Kiongozi wake Mkuu hajui Kingereza...narudia hakuna!

Kwa mtu kama jiwe, kutojua Kingereza kulionesha tu kudumaa kwa akili ya kuzaliwa.

Watu wa aina hii kujitahidi sana kuficha upungufu wao mkubwa wa IQ kwa vitendo vya kukurupuka hovyo!

Mitihani wanapita tu kwa kukariri na ukifuta waliyokariri, wanabaki watupu kichwani na hali hii huwapa hasira!
 
Siyo wote wanaoongea Kiingereza wana elimu mkuu,Kiingereza ni lugha na wala siyo elimu.

Ukisema English ni Elimu utaonekana huna elimu

Kuna Warusi, Wataliano, Wafaransa hawazungumzi Kiingereza sio kwamba hawana elimu...KIINGEREZA NI LUGHA
Acha ujinga wa kijiwe, hao wafaransa wanasoma kwa lugha gani na sisi tunasoma kwa ligha gani?
 
Nadhani aliandikiwa akawa anasoma kitu ambacho hata Mtu wa kawaida anaweza ngoja waje wageni kutoka Magharibi tumuone
Kweli kila mtu anaweza kusoma akiandikiwa, hata wale wanaoandikiwa election wakasoma erection
 
Jana Usiku nilipokea Meseji moja kutoka kwa Rafiki mkubwa kutoka Uganda akielezea Kufurahishwa Kwake na 'Kiingereza ' kizuri alichonacho Rais wa Tanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan.

"Mr. Generalist are you sure that this President of yours Mama Samia she's not a Briton? She speaks fluent English, very articulate, attractive and comfortable with it unlike other so called intellectuals with their doctorates on hand "

Na Waganda hawakuishia hapa tu kwa huyu Rafiki yangu Kunitumia hiyo Meseji bali hata ukienda huko Ugandans On Twitter ( UOT ) Wachangiaji wengi wamevutiwa na Uwezo mkubwa wa Kuongea Kiingereza ' kilichonyooka ' cha Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.

Wameenda mbali zaidi na Kuhoji inakuwa Marais wengine (hasa Barani Afrika) wana Elimu Kubwa lakini walipokuwa wakiwasikiliza (wanapowasikiliza) huwa wanaongea Viingereza 'vibovu vibovu' tu wakati Makabatini mwao wamehifadhi Vyeti vya ' PhD ' zao.

Kongole sana Kwako Rais Mama Samia.

Tanzania mtu ana PHD muulize kaandika lini paper
 
Ni kweli kabisa, ila alikosea matamshi ya "invitation" na "demise"

Hili neno watu wengi sana huwa wanalikosea na hii inatokana na neno la msingi "invite" kutamkwa "invai-ti" hiyo ndiyo sababu "invitation" inatamkwa kimakosa invai-teshen badala ya "inviteshen". Hii ni common mistake kwa non natives wengi wa lugha ya kiingereza.
 
Back
Top Bottom