DOKEZO Rais Samia tafadhali chunguza BRELA kwani ni kikwazo kwa wafanyabiashara, bila hongo hufungui kampuni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari, tumepokea maoni yako kwaajili ya kuboresha huduma zetu.
 
Brela miyeyusho sana.

Nna updates ya kampuni nafanya nao, huu mwaka wa pili now bado hatujamaliza.

Ukipiga simu leo, anapokea huyu anakupa maelekezo haya, ukimaliza kutekeleza maelezo, ukapiga simu tena anapokea mwingine anakupa maelekezo mengine. Yaani taabu tupu.

Na pia nimegundua hawana records ya taarifa za zamani sana. So unawapa risiti za malipo uliyofanya kwao, wanapata kigugumizi, saa zingine hawazitambui.

Wanakuelekezea kwenye penalts tu.
 
Mimi nilisajiri biashara BRELA ndani ya siku 3 kila kitu kilikuwa kimeshakamilka na kupewa certificate ya usajili. Sikutoa pesa yoyote tofauti na elfu 20,000/=, nilienda siku ya maonyesho Kigoma mjini viwanja vya Mwanga community center kwenye mabanda yao kila kitu kikaenda sawa. Sikuona usumbufu wowote.
 
 
Habari, tunaomba namba ya ombi lako (tracking number) ambalo bado hujapokea majibu yako kwaajili ya msaada zaidi.
 
Tunafurahi kukuhudumia, karibu sana.
 
Habari, tunaomba namba ya ombi lako (tracking number) ambalo bado hujapokea majibu yako kwaajili ya msaada zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…