Rais Samia tafadhali nakuomba chukua muda wako leo na uupokee huu Ushauri wangu GENTAMYCINE, nina uhakika utakusaidia sana na Kunishukuru pia

Rais Samia tafadhali nakuomba chukua muda wako leo na uupokee huu Ushauri wangu GENTAMYCINE, nina uhakika utakusaidia sana na Kunishukuru pia

Poti hii issue zimenikera sana
Mtu kuchoma picha,kukupinga unamteka na kuuaaa
Hiyo nguvu badala wa tumiee kulinda uchumi wa nchi wa deal na mambo madoogo

Ova
Nakubaliana nawe 100% Poti.
 
Alafu yule kule mjengoni dodoma mambo haya anaongelea kama hajali vile

Ova
Huwezi kuwa na Kichwa kama alichonacho huyo Waziri halafu ukawa na Akili sawa sawa. Kichwa kinasadifu mengi tu.
 
..hili kundi la Watekaji na Wauwaji Samia alilikuta.

..kama Samia alikuwa hataki kushirikiana nao, au wamfanyie kazi, angelifuta mara alipoingia madarakani.

..Watekaji na wauwaji ktk vyombo vya dola hawawezi kuondoshwa na Rais anayetokana na Ccm.

..kundi hilo limejifungamanisha na Ccm na kila awamu ya uongozi hapa nchini. Kila Raisi anayetokana na Ccm analihifadhi kundi hilo. Na malipo ni kusaidia Ccm kubaki madarakani.
 
Pole na Majukumu yako ya Kiutendaji na hongera kwa yale mazuri unayofanya kwa Tanzania japo kwa kawaida changamoto za Kiutawala / Kiuongozi kwa Rais yoyote hazikosekani na kama hutozimaliza Wewe basi atakuja Kuzimaliza ajaye.

Tafadhali Rais Samia nakuomba fanya yafuatayo ikikupendeza.......

1. Mbadili upesi sana Rais wako wa Mambo ya Ndani Masauni kwani hana anachofanya japo Unampenda

2. Mfute Kazi upesi Ndugu yangu kabisa Mzanaki IGP Wambura kwani Polisi imemshinda teua Mtu sahihi

3. Unda Kikosi Kazi chako cha Uchunguzi waichunguze TISS kwani kunaonekana kwa sasa huko kuna tatizo

4. Acha kupokea Ushauri wowote juu ya Watesi wa Utawala wako kuwa wanyamazinywe kwa kulala mazima

5. Kuwa makini sana na Kitengo cha Operation ndani ya TISS kwani huenda kikawa na Njama ya Kukuchafua

6. Pokea sana Ushauri wa CDF Gen Mkunda na siyo wa DGIS au wa Poti wangu wa Kizanaki IGP Wambura

7. Nchi haiko salama vile kama ambavyo unadanganywa hivyo simama sasa kama Amiri Jeshi Mkuu

Nikutakie tu Majukumu yako mema, ila ninakuomba yazingatie Kiumakini haya mambo Saba (7)niliyokuandikia hapa.

Tatizo liko Usalama wa taifa na Polisi kuwaogopa maana wana ripoti moja kwa moja kwa Raisi. Sasa tatizo ni mfumo hapo sio watu. Sirisiri za usalama ndiyo tatizo na kwanini Usalama wanajihusisha na mambo ambayo haya wahusu
 
..hili kundi la Watekaji na Wauwaji Samia alilikuta.

..kama Samia alikuwa hataki kushirikiana nao, au wamfanyie kazi, angelifuta mara alipoingia madarakani.

..Watekaji na wauwaji ktk vyombo vya dola hawawezi kuondoshwa na Rais anayetokana na Ccm.

..kundi hilo limejifungamanisha na Ccm na kila awamu ya uongozi hapa nchini. Kila Raisi anayetokana na Ccm analihifadhi kundi hilo. Na malipo ni kusaidia Ccm kubaki madarakani.
Ungekuwa unajibu Mtihani kwa hiki ulichokiandika hapa nadhani nisingekupa tu 100% bali ningekupa kabisa 101% zote.
 
Tatizo liko Usalama wa taifa na Polisi kuwaogopa maana wana ripoti moja kwa moja kwa Raisi. Sasa tatizo ni mfumo hapo sio watu. Sirisiri za usalama ndiyo tatizo na kwanini Usalama wanajihusisha na mambo ambayo haya wahusu
Nakubaliana nawe 100% Mkuu.
 
Back
Top Bottom