Samia atosha tukutane2030
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 17,728
- 49,762
1. Wakala wa vipimo (WMA).
Wakala wa vipimo ulianzishwa ili kuleta usawa kwa mlaji na mtoa huduma lakini vituo vya mafuta vinadhulumu walaji.
Sasa hivi bei ya mafuta iko juu na vituo vya mafuta bila aibu wanatuibia huku wakala wa vipimo upo tu . Wakala hii ifutwe haraka na watumishi wake wote wasihamishiwe taasisi nyingine ili kuwepo na funzo kwa watumishi wa taasisi zingine za umma .
Nilifanya utafiti kwenye mabucha, kati ya mizani 6 ni moja tu kidogo ilitia moyo, hii maana yake ni kwamba zaidi ya 80% ya mizani za buchani wananchi tunalaliwa.
2.SIDO
Tangu nazaliwa naikuta SIDO na kila kwenye maonyesho SIDO lazima uikute ila ukifika sokoni bidhaa za SIDO sizioni.
Futa kabisa
3.TARURA
Hawa TARURA wamegeuka jeshi usu, wako busy kufukuzana na bodaboda na vigari . Barabara za mitaani zina hali ngumu .
Futa kabisa
4. Mamlaka za maji hasa DAWASA
Hii ifutwe na jukumu lake ipewe taasisi nyingine au iundwe mamlaka nyingine lakini watumishi wa DAWASA wote tupia nje iwe fundisho kwa watumishi wengine.
5. Bodi ya nyama
Ifutwe kabisa haina tija kwa wananchi.
6. Shirika la nyumba.
Mtumishi wa umma hana cha kujivunia kutoka NHC , mwananchi wa kawaida pia hana cha kujivunia kutoka NHC.
Sasa hili shirika lina umuhimu gani kama limeshindwa kukopesha nyumba angalau 50% ya watumishi?
Kweli mtumishi wa Tanzania wa kujenga kwa kuungaunga kama digidigi huku shirika la nyumba la serikali lipo!!!
Lifutwe haraka.