Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Raisi Samia, utafanya yote, ila kama unataka kuacha jina, basi fanya kila uwezalo kuhakikisha eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa kisasa mkoani Dodoma ujenzi huo unaanza na kukamilika kabla ya 2025.
Kwa ukimya uliopo na muda uliokwishapita, ni vigumu sisi wananchi kuamini Mfalme wa Morocco bado ana nia ya kufadhili ujenzi wa huu uwanja hivyo ni bora ujenzi huo ukajengwa na serikali au makampuni binafsi kama inawezekana.
Kama wasaidizi wako hili hawalioni, bali wanaona mambo mengine wanayoamini yatakujengea legacy basi napata wasiwasi na wasaidizi ulionao.
Lingine ni serikali yako kufuta kesi ya Mbowe na wala si kusubiri uamuzi wa mahakama kwani uamuzi wowote (wa kumfunga au kumuachia huru) ni doa kwa serikali yako.
Futeni kesi ya Mbowe na uwanja uitwe kwa jina lako utakuwa na la kukumbukwa.
Kazi kwako Mama.