#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

#COVID19 Rais Samia: Tanzania tuna wagonjwa wa Wimbi la Tatu la Corona

Hilo wimbi la tatu liko kwenye magazeti na televisheni, lakini huku mtaani hakuna cha wimbi wala bibi yake na wimbi.

Hizo fedha za wazungu mlizokula hakika mtazitapika majizi nyinyi. Maana hamuishi kuweweseka na makorona kama visungura tope.

Huku Buzza kwanza hatujui hata maana ya corona. Tunaisikiaga tu kwenye mitandao na majarida.

Kwendeni huko na mabarakoa yenu uchwara!

Matapeli wakubwa!
Buza kwa Mparange vigodolo kama kawa,kwani huyo Corona ndi bosi wa wapi jemeni 😂
 
Haya sasa akina fuata upepo njooni tena hapa mtuambie sasa hivi kuna corona na mwaka jana haikuwepo!!

Objective truth siku zote iko supported na scientific evidence na haitabadilika bila kujali mitazamo, imani za dini au za kipagani! Mama anaonesha kuwa objectively truthful na hali ya dunia. Haiwezekani wengine wote wana tatizo hili halafu tukamshihaki Mungu kuwa sisi tatizo hilo halipo huku tukikataa kupima na kuchukua tadhadhari. Uongo wa mwendazake umefanya nipoteze mama yangu!! Ninamchukia kwa jambo hili!!
 
Ni vizuri wakatupatia takwimu za hao wagonjwa, itasaidia zaidi kutoa hamasa ya watu kuchukua tahadhari kuliko maneno matupu bila ushahidi
Ni mbinu tu za kutakatisha mikopo ya fedha toka kwa waliotengeneza hiyo Corona ili watupige kwa kutuuzia chanjo zinazobadilisha DNA!
 
Noma sana 👇👇

Screenshot_20210626-002725.png


Screenshot_20210626-002700.png


Screenshot_20210626-002725.png
 
Hilo wimbi la tatu liko kwenye magazeti na televisheni, lakini huku mtaani hakuna cha wimbi wala bibi yake na wimbi.

Hizo fedha za wazungu mlizokula hakika mtazitapika majizi nyinyi. Maana hamuishi kuweweseka na makorona kama visungura tope.

Huku Buzza kwanza hatujui hata maana ya corona. Tunaisikiaga tu kwenye mitandao na majarida.

Kwendeni huko na mabarakoa yenu uchwara!

Matapeli wakubwa!
Unataka afe mumeo ndio ukubali? Lije wimbi lisije ila tambueni mkuu ni mamy
 
Lije wimbi lisije ila tambueni mkuu ni mamy
Huyo mamy wako ni bingwa wa maigizo (futuhi).

Nakutuma kwake ukamwambie kwamba sisi wakazi wa Buzza tuna afya tele mpaka zinabaki. Asitulazimishie magonjwa ambayo hatuna.

Ukishamueleza hayo, nenda kwenye kioo ujiangalie kisha ujipige kifua mara tatu huku ukisema "mimi ni mpumbavu sana".
 
“Tanzania tuna wagonjwa wa wimbi la Tatu la Corona. Hili jambo bado lipo, tuchukue hadhari zote na tunawaomba viongozi wa dini mseme hili kwa sauti kubwa"

Rais Samia Suluhu Hassan wakati akizungumza na baraza la maaskofu katoliki (TEC) #Tanzania #COVID19

=========

Rais Samia Suluhu: Wahashamu, baba Maaskofu kama mnavyofahamu, dunia kwasasa inakabiliwa na mlipuko wa Covid-19 na nafahamu kanisa tangu mwanzo limekuwa na msimamo Thabit katika kupambana na ugonjwa huu hivyo basi niwaombe sana Maaskofu msisahau kuwakumbusha waumini kuhusu wa kujikinga na kuchukua Tahadhari zote zinazoelekewa na wataalam wa Afya dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Kwakuwa Kinga ni Bora kuliko Tiba, tusiache kutumia kila kitakachotukinga na maradhi haya ili kuepesha vifo vya makundi.

Kama tunavyojua, duniani sasa hivi kuna wimbi la tatu la Corona, tumetoka kwenye wimbi la kwanza Tanzania tumeingia, limekwenda limepungua kidogo, tumeingia Wimbi la Pili tumekwenda nalo na sasa kuna Wimbi la Tatu.

Ishara ndani ya nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana katika kwenye wimbi hili la Tatu. Kama mnakumbuka siku nilitembelea hospitali ya Mwananyamala, kuna wodi daktari mfawidhi alikuwa ananiingiza akaniambia humu kuna wagonjwa wenye matatizo ya kupumua, nikamwambia hebu kuwa muwazi, ni covid, akaniambia ndio Covid wakati wapiga picha wangu tayari wameshatangulia, nikawaambia nyie tokeni haraka huko.

Kwahiyo ni kusema kwamba hili jambo bado lipo, tusijiche, bado lipo tuchukue hadhari zote na tunawaomba sana viongozi wa Dini mliseme hili kwa sauti kubwa, kwa waumini wetu ili tujiepushe na vile vifo vya makundi.

Pamoja na yote hato, ni vyema pia tumuombe Mungu kwa kiasi kikubwa aendelee kutuepusha na kutupa hifadhi yake kutokana na maradhi hasa Janga hili la Corona kwakuwa yeye ndio Muweza wa Yote.


kama hali ni serious kwa namna ambavyo Serikalu na Raisi wanavyo taadharisha nilitegemea kusikia tamko la kuamuru vyuo na shule zote kufungwa mpaka pale hali itakapokuwa sawa. Otherwise hii itakuwa ni episode nyingine ya comedy.
 
Barakoa huendana na kuepuka mikusanyiko ila sisi tunakusanyana tu mikusanyiko isiyo ya lazima mara sijui mkutano wa vijana mara wanawake halafu et tunategemea barakoa.
Binadamu wengi sana pato lao hutegemea mikusanyiko. Wazungu wanaufahamu ukweli huo na wanakesha maabara wakitengeneza chanjo, wanataka maisha yarudi hali ile ya zamani.

Kuna matatizo makubwa kiakili yanayokwenda pamoja na maisha ya kujitenga. Kujiua kumeongezeka Ulaya na Marekani kipindi hiki cha corona.
 
Kwa Nini Baraza la maaskofu katoliko TU?

Wao ndiyo wenye waumini TU??
Misikitini hakuna waumini?
Akina gwajima na makanisa mengine ya kilokole Hakuna waumini?

Waumini ndyo wanahatari ya kuambukizwa na Corona?

Na wasio na dini wahimizwe na Nani kuchukua tahadhari??

Kuna Nini nyuma ya katoliko na wimbi la tatu,?

Hata wimbi la pili katoliki walipiga kelele Sana! Kuna Nini nyuma ya pazia?

Wenye wananchi Ni serikali au Baraza ka katoliki??

Nway ,watu wasioitakia nchi hii mema, wanapenda tahadhari ya lockdown na kuzika watu bila ndugu.

India walikuwa wanachukua viungo vya watu waliokufa kwa kivuli Cha Corona.
Hawa si walipigwa mshono na JPM wakatapatapa km cockroaches...

They are helping each other to find a grip
 
Very technical presentation
Kaanza na maaskofu
Inakuja part 2
Chanjo
Lockdown
Mama anafeli sana, anyway, zigo ni lake, akisema tusiende kazini sisi poa, lockdown itakua ya kutokwenda kazini tu maana mitaani nina uhakika uswahilini maisha yataendelea, itakua likizo kwetu ya kazini.
 
Hili sizani kama watanzania watamuelewa huyu mama!

Jpm aliiweka imani kwao
 
hiyo corona ipo huko huko ushuani kwenu sisi huku tandale atujui hiyo kitu kabisa
 
Back
Top Bottom