Kwa ujumla ulichoonesha ni upuuzi waa Wakenya. Tabia yako ya kupenda maziwa ya Brookside sijui kama ulijiuliza ni nini unachokunywa. Brookside sasa hivi inaendeshwa na shares za Newzealand. Unakunywa mchanganyiko wa maziwa ya unga toka Newzealand.
Tabia ya kugomea kununua bia ya nje ya Kenya, ndo tabia inayosababisha usiweze kuwekeza Kenya. Siyo uzalendo ni ubaguzi na ukabila. Leo hii kuna wa-TZ wana akaunti KCB, lakini ukifungua tawi la NBC Kenya wanaisusia. Ni ubaguzi unaoanzia kwenye familia, wao kwa wao, then kwa waafrika wengine. Lakini ni wadhaifu sana kwa ngozi nyeupe, hadi kuchapwa viboko. Hapa kwetu pia hili lipo kwa makabila fulani, tukubali wazi.