PostGE2025 Rais Samia: Tumeambiwa vijana walioingia barabarani kudai haki walilipwa fedha kwanza

PostGE2025 Rais Samia: Tumeambiwa vijana walioingia barabarani kudai haki walilipwa fedha kwanza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Rais Samia amesema "Tumeambiwa vijana walioingia barabarani kudai haki walilipwa kwanza" wakati akizindua Tume huru ya uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Oktoba 29, 2025


Sasa kama anajua walilipwa, kuna haja gani ya kuunda tume ya kuchunguza jambo analolifahamu?
 
Kuna mwl mwenzako kama ww naye alijifanya anatafuta haki wakati nae kutwa anatoroka kazini yaani saa 7 TU yupo kitaa...now walimdaka kwenye maandamano yupo segerea now...sasa unajiuliza ni haki Gani alikuwa anaidai wakati yy ndo alikuwa haitimizii haki nchi
Kwa hio unataka kusemaje walimu wote nchi nzima waliosimamia uchafuzi wa October 29 na kuidhinisha matokeo feki wote ni mafala si ndio?
 
Mmeambiwa ? Baada ya kuambiwa mlichanganya na zenu ?

Pili kama walilipwa na bado wanadai Haki zao, hata mimi ningeshukuru sana kupata hao watu wa kunilipa ili nidai haki yangu...

Ingawa ukweli ni kwamba mambo yapo ndivyo sivyo na tukiendela kwa mtindo huu wa kutumia muda kutafuta sababu ya matatizo badala ya kushughulikiwa matatizo hayo mambo yaliyotokea yatakuwa ni normal occurance...
 
Siku 90? Wako serious? Wafanye kazi usiku na Mchana. 10 days report itoke. Siku 90 wanachunguza Nini? Ambacho hakijulikani?
 
Rais Samia amesema "Tunaambiwa kwamba vijana wale walioingia kudai haki walilipwa fedha kwanza ndiyo wakaingia barabarani, na wengi wao waliingia barabarani kutokana na hizo fedha walizopewa. Je, fedha hizo zilitoka wapi?" wakati akizindua Tume huru ya uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Oktoba 29, 2025


Aliyembebesha huyu mama gunia la misumari Mungu anamuona yaani wanampeleka wanavyotaka
 
Rais Samia amesema "Tunaambiwa kwamba vijana wale walioingia kudai haki walilipwa fedha kwanza ndiyo wakaingia barabarani, na wengi wao waliingia barabarani kutokana na hizo fedha walizopewa. Je, fedha hizo zilitoka wapi?" wakati akizindua Tume huru ya uchunguzi wa Matukio ya uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi Oktoba 29, 2025


Huyu mama ni zaidi ya tapeli. Kwahiyo anamajibu ya tume tayari
 
Back
Top Bottom