Rais Samia: Tuna ‘crisis’ ya umeme, tunafanya ukarabati wa mashine

Rais Samia: Tuna ‘crisis’ ya umeme, tunafanya ukarabati wa mashine

Akizungumia kuhusu changamoto ya kukatika kwa umeme, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mitambo haikufanyiwa maboresho kwa muda mrefu, hivyo maboresho yanapofanyika baadhi itazimwa na ndio maana imesababisha upungufu wa umeme
Changamoto nyakati za KIANGAZI ... nyani wanacheka haswaa!
Ugimbi ulochacha hata ukitiwa kwenye kibuyu kipya hamna kitu hapo.
Changamoto ya UENDESHAJI wa taasisi zetu nyingi ni pamoja na MAPUNGUFU YASIOTIBIKA KWENYE RASILIMALI watu ... hakuna seriousness ya kibiashara ya kusimika COMPETENCE kwenye uongozi na badala yake wenye mamlaka wanazingatia undugu, siasa na kuendeleza RUSHWA. NAFASI hizo zishindanishwe KIMATAIFA. Kwani shida nini ikiwa miradi mingi mikubwa inafanyika na wakandarasi wa nje? Biashara na makandokando ya siasa chafu itapekekea kufunguka zaidi kwa milango ya kutumbukia shimoni. Tumbonomics shiida sana.
 
Lini alikua mkweli? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Huyo anachoweza ni mipashooo na kusutana.
😁😁😁 kama jana alivyokuja kutupasha akaona awaite na wakurugenzi ikulu wakati hawaapishi😁😁😁ili kuja kujitetea na panga pangua zake zisizoeleweka

Tutajuta kuongozwa na mzanzibar wa kizimkazi
 
Maharage kabla ya kuenguliwa angeshurutishwa yeye na ukoo wake wakojolee mabwawa ya uzalishaji umeme mpaka yajae ,yakishajaa ndio aenguliwe
 
Huyu Hangaya hana kauli yoyote....anasubiri remote itoe signal ndio afungue mdomo.

👇👇....c&p
Gangsters in Suit.

KIPARA na Maharage mwezi Machi 2023, waliagiza na kuamuru maji katika bwawa la Mtera (Catchment area; 68,000 km² (26,000 sq mi)) yafunguliwe na kumwagika nje.

Hoja yao; Maji yangelijaa sana na yangelipasua bwawa la Mtera. Wahandisi na wataalam kutoka katika bwawa la Mtera wakapinga jambo hilo kitaalam.

Wataalam na wahandisi kutoka Mtera wakawaleza hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam hutumika kwa shughuli nyingi siyo Hydropower tu.

Hifadhi ya maji (reservoirs) kwenye Rock-fill dam (kama Mtera) hutumika hata katika irrigation, human consumption, industrial use, aquaculture, na navigability.

Lakini kwa mamlaka yao, KIPARA na Maharage wakaagiza kwa lazima maji yafunguliwe katika bwawa la Mtera. Maji yakafunguliwa.

Maji hayakujaa tena katika bwawa la Mtera, kwa sababu mvua zilipotea. Sasa nchi yetu inapitia mgao mkali wa umeme kwa sababu ya wahuni.

Septemba 2023 mgao umekuwa mkali na wanaohusika na umeme wanajitetea kwamba kuna upungufu wa uzalishaji umeme kwenye mabwawa kutokana na ukame.

Kuliko kuwahamisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, hawa ‘wahuni’ walipaswa kupumzika utumishi wa umma. Hawatufai.

Tunataka kuamini kwamba ‘Rais ni taasisi’ na Rais anatakiwa kuwaondoa katika utumishi wa umma hawa wahuni. Haitakiwi kuwahamisha waharibifu kutoka ofisi moja kwenda nyingine.

Wakati hawa wahuni wakisubiri nje ya utumishi wa umma, Tunahitaji uchunguzi wa kamati maalum ya bunge katika jambo hili, haraka. Ingawa lenyewe ni dhaifu.

Haiwezekani wahuni wananufaika kuingiza na kuuza majenereta wakati wengine tunapata msoto wa mgao wa umeme. Wanatutia umaskini.

MMM, Mtikila.
Hii story ni ya kutunga. Kwa sababu bwawa la mtera linazalisha 80 MW at maximum capacity. Ni kiasi kidogo sana katika gagrade yenye kubeba 1500+ MW. Bila bwawa la Mtera still kama vyanzo vingine viko vizuri hakuna mgao wa umeme.
Kuna tatizo sehemu lakini siyo kwa issue ndogo ya bwawa la mtera.
 
Back
Top Bottom