#COVID19 Rais Samia: Tupo hatua za mwisho za kuagiza chanjo

Sasa hao majority utawapataje kama wengi bado hawaitaki hiyo chanjo?
Utoaji wa chanjo utakuwa ni zoezi endelevu, kutoa elimu na kuhamasisha watu kuchanjwa kunatakiwa kuanze mapema.
 
Hata hivyo, ifike wakati Serikali isicheke na watu wababaishaji, hii kitu inapaswa kuwa ni LAZIMA. Haiwezekani watu 2.4 billion dunia wamechomwa na sasa hadi viwanjani wanaingia halafu tuwaone kuwa hao ni wajinga. Ifike mahali kama kweli tunataka kutatua tatizo iwe ni lazima
 
Kwa hiyo mkuu unaona ni bora wote wachanje? Hapana nakupinga kwa hilo..
Tuheshimu maamuzi ya kila Mtu asee.
N.b mbeleni chanjo itakua moja na kila Mtu itamlazimu achanje kwa lazima. Sio leo wala kesho.. but mbeleni
Sawa, ila hii kitu ikitolewa nusu nusu inaweza leta madhara kwa wengine mbele ya safari, herd immunity hadi ifanye kazi lazima wengi wawe wamechanjwa.
 
Hamjibu swali langu la mwanzo, kama ni hiari vipi ikitokea wengi hawajapata hiyo chanjo, herd immunity itafanyaje kazi?
Haitafanya. Ndiyo maana kila serikali inatumia elimu na ushawishi ili watu wengi kadiri iwezekanavyo wachanjwe. Kuna nchi walikuwa wanatoa mshiko ili vijana wachajwe. Ila hali ilivyo ni kuwa nchi karibu zote duaniani wananchi wake wamepokea chanjo vizuri. Bongo ndiyo naona kuna ujinga mwingi.
 
Utoaji wa chanjo utakuwa ni zoezi endelevu, kutoa elimu na kuhamasisha watu kuchanjwa kunatakiwa kuanze mapema.
Ndio maana naona tunacheza na Corona badala ya kupambana nayo.
 
Ndio maana naona tunacheza na Corona badala ya kupambana nayo.
Shida aliyeuanzisha huo mchezo na corona kafa, jamaa alitoa kauli ambazo zinaweza kuishi zaidi ya miaka 100 kwenye akili za wabongo
 
Ok, kumbe nawe unaona kuna ujinga mwingi, sasa kipi kilichowafanya mnipinge mwanzo niliposema chanjo itolewe kwa lazima sasa ili herd immunity ifanye kazi badala ya kusubiri wakati mwingine?
 
Shida aliyeuanzisha huo mchezo na corona kafa, jamaa alitoa kauli ambazo zinaweza kuishi zaidi ya miaka 100 kwenye akili za wabongo
Kweli alikosea, ila sasa naona ni wakati elimu ya kujikinga itolewe kwa nguvu ili kuwaokoa wale waliodanganywa.
 
Nyie ndio tatizo la hii nchi, huu ujingao wenu utawadhuru wengine.
Tutawadhuru kivipi, mimi kutochanja nimekuathiri vipi wewe uliyechanja na kwa nini isiwe kinyume chake.............sababu hamjielewi mtaishia kutegeneza susceptible population ambayo itaishi kwa kutegemea hizo takataka mnazoita chanjo, mbona hamjasema tulazimishe watu waanze kuchanja mafua (common cold) au hujui huko kwa mabeberu wanachanja mafua.....
 
Wajinga hawaelewi kitu gani kinaendelia, na waelevu wanaelewa kitu gani kinaendelea.
 
Wewe ukichanjwa si huambukizi tena? Hofu ya nini kwa asiechanja?
 
Chanjo ni hiari!
 
Hamjibu swali langu la mwanzo, kama ni hiari vipi ikitokea wengi hawajapata hiyo chanjo, herd immunity itafanyaje kazi?
Aliyekwambia herd immunity inategemea chanjo ni nani? ni asilimia ngapi ya watu wamewahi kuchanja malaria.....nenda kawapime kama hawana hiyo kinga ya malaria, tatizo mnashadadia mambo ambayo hamna uelewa hata tone....
 
Good, tuache maigizo kwenye afya za watu, mara sijui mapapai, mbuzi, kujifukiza, tangawizi, maembe na ujinga mwingine.
Mimi sichanji ila ntakuwa mstari wa mbele kuwashika bavicha matakle ili chanjo zipenye vizuri
 
Right now the French People are protesting/rioting over the mandatory vaccinations instituted by President Macron...There is a lesson here
 
Ok, kumbe nawe unaona kuna ujinga mwingi, sasa kipi kilichowafanya mnipinge mwanzo niliposema chanjo itolewe kwa lazima sasa ili herd immunity ifanye kazi badala ya kusubiri wakati mwingine?
Ujinga ni mwingi kwa sababu walidanganywa na Magufuli. Ikitolewa elimu wengi watabadilika. Siku zote sula la matibabu linatakiwa liwe ni hiari. Ila suala la lazima linaweza kutumika iwapo itaonekana kuna ulazima. Imagine nchi nyingine karibu zote zichanje ila Tanzania iwe kikwazo na kusababisha virus mutation kushika kasi. Hapo kutakuwa na ulazima wa kuingilia. Hata sasa hivi ugonjwa kama TB mtu akionyesha kutoka kufuata matibabu kwa hiari na akawa tishio kwa wengine sheria inaweza kutumika kumlazimisha atibiwe.
 
Zanzibar wafanyakazi wa afya tayari wamepiga chanjo ya mwanzo.
Wamezitoa wapi? Kwa mataifa ya mbele stock haitoshi huku wameshapata, wamezipata wapi au ndio maji tu yaewekwa chumvi kisha kudai ni chanjo?
Hizi chanjo watqwachanja wazembe sio mimi. Familia yangu haichomwi...
 
Hujui namna herd immunity inavyofanya kazi, lazima wengi wawe wamechanjwa ili hiyo immunity ifanye kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…