DED wa Halmashauri ya Monduli pamoja na RC wa sasa wa Arusha Idd Kimanta wamepora fidia ya ardhi kwa taasisi za dini ya Kikristo na Kiislam pamoja na mwanamke mmoja waliopitiwa na umeme wa Kilovolt 400 kutoka Singida -Namanga katika Kijiji cha Makuyuni Wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha.
Mwaka 2016- 2017 Idd Kimanta akiwa DC wa Monduli alishirikiana na DED Monduli kuwadhulumu wananchi na taasisi za dini fidia iliyokuwa ilipwe na TANESCO kwa wananchi hao ambao walikuwa wamepewa ardhi hiyo kisheria na serikali ya kijiji cha Makuyuni kati ya miaka ya 2007- 2009.
Kijiji cha Makuyuni kiligawa ardhi hiyo kupitia vikao na mikutano halali kama inavyotakiwa katika sheria ya ardhi.
Mwaka 2016 TANESCO iliwatangazia wananchi wanaopitiwa na umeme huo katika ardhi yao wajitokeze ili kulipwa fidia na hapa ndipo DED wa Monduli na DC wa wakati huo IDD Kimanta walipoingia tamaa na kufanya kila mbinu ili wananchi na taasisi za dini ya Kikristo na kiislam wasipewe fidia bali wao wachukue kwa kigezo eti ardhi ni ya Halmashauri.
Baadhi ya wananchi walichukua uamuzi wa kupeleka shauri mahakamani lakini hata baada ya DED kushindwa vibaya katika mahakama kuu bado amewashawishi TANESCO isiwalipe fidia wananchi hao.
Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu naomba utusaidie kuingilia kati ili tuweze kulipwa fidia ya ardhi yetu na kukomesha huu uonevu.