Rais Samia amesema anasubiria ripoti ya Timu aliyoiunda Kupitia mashirika ya Umma yanayoripoti Kwa Msajili wa Hazina Ili juyafutilia mbali Yale ambayo hayana Tija Wala faida. Amesema Mashirika Yatakayokufa basi wahusika wajiandae kufa nayo.
“Serikali tumeamua kufanya tathmini ya utendaji wa mashirika yote ya umma na yale ambayo Serikali ina hisa kubwa. Lengo la tathmini hiyo ni kubaini mashirika yasiyo na faida ambayo yameshindwa kujiendesha na yanaitia Serikali hasara.”
"Nasubiri taarifa ya mwisho, ya mashirika gani yanabaki, gani yanaondoka, na gani yasaidiwe vipi kufanya biashara, na siku tutakayoyatangaza...haya mashirika yakifa, wafe nayo, sitaki kusikia shirika linazorota,meneja anapiga suti nzuri anatamba mitaani, hatutaenda pamoja".
---
My Take
Safi sana mh.Rais hakuna kulea ujinga ujinga wa miaka Mingi ambako watu waligeuza Mali ya Umma ni mashamba ya Bibi..