Rais Samia: Tutafuta baadhi ya Mashirika yasiyoleta tija, yakifa wafe nayo

Mama Samia safi sana. Uko very realistic. Shirika kila mwaka HASARA tuu. Sasa lipo for what? Hizo pesa za kuendesha shirika goigoi zingeenda kujenga barabara,mashule,maji nk. Mama usisikilize krlele za watu wavivu. Futa mashirika hayo yote. Mambo mengine iachiwe PRIVATE SECTOR.Serikali ibaki kama regulator tu.
 
Mama Samia ktk hili nakuunga mkono 100%. Mashirika mengi yamepitwa na wakati. Kazi zake zimechukuliwa na private sector. Hoja ya muhimu hapa ni kuweka mikakati thabiti ya kuprotect na kupromote PRIVATE srctor.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi ya Sh45.5 bilioni (Gawio la Serikali) kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya benki hiyo.


Wakuu wa mashirika ya umma na taasisi ambazo Serikali inamiliki hisa kubwa, wanapaswa kukaa mguu sawa wakati Msajili wa Hazina akikamilisha tathimini ya pili ya ufanisi wake, ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amesema ataitumia kufanya uamuzi.

Wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya kuanzishwa kwa benki ya NMB Plc yaliyofanyika jana katika ukumbi wa Mlimani City, Rais Samia na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu walieleza juu ya hatua wanazokusudia kuchukua kwa mashirika yanayosuasua kiutendaji.

"Serikali tumeamua kufanya tathimini ya mashirika yetu yote makubwa na yale ambayo tuna hisa nyingi, lengo ni kubaini yasiyo na faida, ambayo yanashindwa kujiendesha na ambayo yanaitia Serikali hasara," alisema Samia na kuongeza:

"Msajili wa Hazina amefanya tathimini ya awali ameniletea ripoti. Nikamwambia nenda kafanye tathimini ya pili, kwa hiyo wale mnaoshika mashirika TFS (Wakala wa Misitu Tanzania) Dos Santos nakuona, kajitizame vizuri ndani ya shirika lako pamoja na kwamba misitu ni wewe peke yako, kajitizame vizuri”.

Rais alisema ujumbe huo ni kwa wakuu wote wa mashirika, na kwamba hatua hiyo haina kurudi nyuma kwa kuwa kuna yatakayofutwa, kusaidiwa na mengine yatapewa miongozo namna ya kujiendesha ili yote yapate faida.

Alisema Serikali ilianzisha mashirika hayo ili yasaidie kuzalisha mapato na kuisaidia Serikali kubeba mzigo, siyo yenyewe kula serikalini.

"Kwa hiyo msajili vaa njuga, nimekupa baraka zote, nasubiri taarifa ya mwisho ya mashirika gani yanabaki, yapi yanaondoka na yapi yasaidiwe nini kufanya biashara na siku tutakayoyatangaza, yale ambayo tutatoa fedha mfukoni kuyasaidia, nitawaambia hayo mashirika yakifa mfe nayo," alisema.

Alisisitiza kuwa hatavumilia wala hataki kusikia shirika linazorota, ilhali meneja wake anapiga suti nzuri na kutamba mitaani.


Mwananchi
 
Kuna sekta ambazo ni huduma huwezi kuacha mikononi mwa watu binafsi ila kwa sababu mwalimu wake ni yule aliyeshindwa tutegemee hayo mambo anayotaka kufanya
 
Hapo nipo na. Mama
Shida ni vipengele vya mikataba! Isiwe ya miaka nenda rudi tuwape hata 20 au 10na tuwe na uwezo wa kuivunja pale wanapkenda tofauti nasi
 
Rais asijibaraguze kujaribu kutuhamisha kwenye Hoja ya Bandari. Tunataka Bandari yetu. Ebo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…