Rais Samia: Uanaharakati, vikundi vya kigaidi na maandamano ni mfumo wa vurugu kuwasilisha sauti ya watu

Sasa kama Rais hajui vifungu vya katiba alivyoapa kuvilinda ikiwepo na haki ya maandamano,basi hii ni hatari.
 
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Mama anatamka
Mama anatamka kizungu swaaafi kabisa. Siyo kama Tibaijuka na intonation yake ya kihaya.
 
Vipi tena zile 4R’s zake alizotuambia aziamini tena, si kuna ‘resilience’ mule imekuwaje.
 
Anajua yeye ndo sheria.

Mungu anapita nao kimya kimya
 
Watanzania tuna akili na ni wengi na tunao uwezo wa kujitokeza hadharani tofauti na watanganyika wenye ukosefu wa jeuri ya kutoka huko nje wakaonekana.

Watanganyika wengi ni mashujaa wa nyuma wa keyboard.
Usije siku moja ukashangaa huyo huyo atajitokeza na kulalamika juu ya hawa "Watanganyika wengi, mashujaa wa nyuma ya keyboard."

BTW: upo hapa" nyuma ya keyboard" kwa vile unauelewa umuhimu wa kuwepo, au siyo?

Sasa jaribu kutumia akili vizuri zaidi; ili usiwe unajinyesha kuwa kigeugeu.
 

Hakuzungumzia la bandari kuwa yeye ameshindwa kuwasikiliza wananchi? Kumbe anajua ni nini kitafuata pale ambapo wananchi watachoshwa na mfumo mbovu wa kiutawala?
 
Harakati za kuidai Tanganyika nyingi zinatokana na ubaguzi ulio katika mawazo yetu sisi tunaoficha majina yetu halisi.

Bado Tanganyika haina nguvu wala sababu ya kudaiwa kwa kigezo chepesi cha suala la bandari. Hilo ni suala la kiuchumi zaidi kuliko la kianaharakati.

Wanaharakati wamelivamia kwa wingi, wengi wao wakitumika na wapigaji wa muda mrefu wa hapo bandarini. Kwa makusudi kabisa wakitambua namna wanavyowakwaza wafanyabiashara wa kweli wanaoagiza na kusafirisha mizigo bandarini kila siku.
 
Nilikuelewa vizuri sana nilipokusoma bandiko lako la mwanzo kabisa humu JF na kukuona jina ulilojipachika ili uwe mtoa fikra zako humu jukwaani.

Swala la kuidai Tanganyika, kama ujuavyo halikuanza na uwepo wa DP World hapa. Ila watu wa aina yako kila mara mnakimbilia upande huo wa kundi mnalojitambulisha nalo zaidi kuliko uTanzania unaotuhusu sote bila ya hayo makundi yanayotengeneza jamii yetu ya kiTanzania.
Tatizo linalotuandama ni hilo la vikundi, na hapa ni wazi kabisa upo hapa tokea uingie JF kwa sababu hiyo hiyo.

Hutetei maslahi ya Tanzania kwa ujumla wetu, bali wewe ni mshirika wa mpambano ya vikundi maalum.
 
Sio kweli, Tanganyika inatumiwa kama ngao ya kukwepesha mjadala mzima wa DPW. Wanajua wakija na mada nzito kipindi hiki cha rais mzenji watasikilizwa na mjadala mzima utahamia huko na suala la bandari litakuwa ni secondary tu.

Wameweza kuwapata baadhi ya watu wepesi wepesi na ndio hawa wanaosema SSH ni mwarabu anayetaka kuuza nchi hii kwa wajomba zake, huko UAE, Ni upuuzi mtupu.

Hayati JPM angekuwa hai mpaka muda huu tungetia saini na hawa hawa DPW na hakuna mtu ambaye angeweza kuinua mdomo wake kusema eti ni waarabu. Imejengwa hoja ya uarabu kwa sababu rais wetu wa sasa ni mzenji, angekuwepo mjenzi mwenyewe wa SGR muda mrefu tu tungeshamaliza hii biashara.
 
Swala la Tanganyika limekuwepo muda mrefu sana, na Samia kalipa uzito zaidi kwa matendo yake mbalimbali, na siyo hilo la Bandari pekee.
Sasa swala hilo haliondoki tena, na wala halififishwi kwa njia yoyote.

Mtu unapokuwa kiongozi wa nchi, kitu muhimu cha kuzingatia katika uongozi wako ni pamoja na kutambua maswala yenye kuleta mtafaruku katika nchi unayoiongoza. Unakuwa mwangalifu sana na maswala hayo, ili unapoyagusa yasilete kutokuelewana ndani ya nchi yako. Kiongozi unapojifanyia tu mambo yako, kwa msukumo wa maslahi yako, au ya makundi yanayokuhimiza ufanye hayo, kiongozi huyo anakosa weledi katika uongozi wake.
Haya sasa ndiyo yaliyomfika Samia. Hakuna njia tena ya kuyafumbafumba.

Kuhusu hilo la JPM, unaweza kuwa sahihi kwa upande wa "kutia saini na hawa hawa DPW"; lakini kama ilivyo kawaida yenu kwa upande wa kundi hilo, mnajifanya kujisahaulisha tu kwamba kinachozungumziwa hapa siyo DPW.
JPM asingkubali "Makubaliano/Mkataba" unaowahusu hao DPW. Hili ndilo jambo muhimu zaidi, pamoja na nyinyi kutotaka lifahamike hivyo kwa kupotosha tu kwa maksudi.
 

Hilo ni wazi kabisa na ni ukweli 100%.


Ni vikundi na watu wasikubalika wasiyo na na mvuto ndivyo huishia kuwa hivyo.
 
Unapouongelea mkataba ni kama vile mstari fulani wa kwenye kitabu kitakatifu cha ZABURI, au Matendo ya Mitume.

Wanasheria kila siku wanaelimisha kuhusu huo huo mkataba tofauti na hawa kina Mwabukusi wanaochagua kifungu kimoja au viwili badala ya kuuchambua mkataba mzima ili mwananchi wa kawaida apate ufahamu sahihi.

Samia amekuwa ni rais msikivu sana tofauti na waliomtangulia, ameifufua demokrasia na kuleta uhuru na uwazi wa kusema chochote mtu anachojisikia.

Hafanyi kwa msukumo wa maslahi yake, sio kweli. Ni lazima mamlaka ya nchi iheshimu mchango wa wafanyabiashara kwa mfano. Ni lazima nchi iongozwe na weledi katika kila sekta.

Kuna hawa lobbyist wamekuwa na nguvu sana awamu hii, na yeye kama rais amewapa uhuru. Sioni kama hilo ni kosa au ni udhaifu wa uongozi wake.

Hayupo ikulu kuridhisha kila mtu kutoka katika kila taasisi, yupo pale kutimiza zile ahadi zote ambazo CCM waliziahidi kupitia ilani ya uchaguzi. Na anazitimiza moja baada ya nyingine.

Ndio maana wakubwa wa zile taasisi nyeti za kiserikali hakutaka kuwabadilisha, alitaka wamalize kazi walizoanza awamu ya tano. Hata salamu ya Kazi iendelee ni tafsiri ya hali halisi aliyoachiwa na mtangulizi wake hayati JPM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…