kimsingi unazungukia mle mle kwenye "talking points" zile zile toka mwanzo, hakuna jipaya hata moja katika haya yote uliyoandika hapa.Unapouongelea mkataba ni kama vile mstari fulani wa kwenye kitabu kitakatifu cha ZABURI, au Matendo ya Mitume.
Wanasheria kila siku wanaelimisha kuhusu huo huo mkataba tofauti na hawa kina Mwabukusi wanaochagua kifungu kimoja au viwili badala ya kuuchambua mkataba mzima ili mwananchi wa kawaida apate ufahamu sahihi.
Samia amekuwa ni rais msikivu sana tofauti na waliomtangulia, ameifufua demokrasia na kuleta uhuru na uwazi wa kusema chochote mtu anachojisikia.
Hafanyi kwa msukumo wa maslahi yake, sio kweli. Ni lazima mamlaka ya nchi iheshimu mchango wa wafanyabiashara kwa mfano. Ni lazima nchi iongozwe na weledi katika kila sekta.
Kuna hawa lobbyist wamekuwa na nguvu sana awamu hii, na yeye kama rais amewapa uhuru. Sioni kama hilo ni kosa au ni udhaifu wa uongozi wake.
Hayupo ikulu kuridhisha kila mtu kutoka katika kila taasisi, yupo pale kutimiza zile ahadi zote ambazo CCM waliziahidi kupitia ilani ya uchaguzi. Na anazitimiza moja baada ya nyingine.
Ndio maana wakubwa wa zile taasisi nyeti za kiserikali hakutaka kuwabadilisha, alitaka wamalize kazi walizoanza awamu ya tano. Hata salamu ya Kazi iendelee ni tafsiri ya hali halisi aliyoachiwa na mtangulizi wake hayati JPM.
Sasa ngoja nikwambie kitu, na sitarudia tena. Najua lilishakieleza kwako, lakini hukuzingatia niliyokueleza.
Usidharau uwezo wa kufikiri wa watu unaojadiliana nao hapa. Usichukulie wote unaobadilishana nao mawazo kuwa akili zao ni pungufu.
Yaliyomokwenye "Makubaliano/Mkataba" kati ya Tanzania na Dubai sasa hivi yanajulikana kwa yeyote anayejua kusoma na kuelewa, na si lazima awe mwanasheria (hizi myth za kipuuzi). Unapoendelea kudai hakuna tatizo lolote na Makubaliano/Mkataba" huo, eti kwa vile wewe ni mwanasheria unayejua sheria sana, unaonyesha upungufu katika fikra zako.
Samia ni kiongozi dhaifu sana tena mwenye hadaa za kijinga sana kama mnavyoendeleza hadaa hizo hizo mbele za watu kama unavyofanya wewe hapa.
Ukitaka kujua ubaya wa huyo kiongozi unayeshinda hapa ukitetea mambo anayofanya sasa hivi, ni kujua jinsi alivyokuwa akifanya chini ya mkuu wake JPM.
Hakunayanyua kidole wala kutikisa mdomo juu ya lolote lililofanywa na huyo huyo kiongozi aliyekuwa akimsaidia kazi.
Sasa baada ya huyo kiongozi kufa, huyu aliyekuwa kavaa ngozi ya kondoo, mara moja kageuka kuwa chui, anageka na kufanya tofauti kabsa na yale yaliyokuwa yakifanywa na JPM.
JPM asingekumbatia hawa walanguzi wa mali za waTanzania, ndio wawe watu wa kuendesha serikali yake.
Sitashangaa sana ukiwa ni mmoja wa waajiriwa wa hawa watu, kuja hapa kuweka upotoshaji hata katika maswala yaliyo wazi kabisa, na kudhani watu hawana akili ya kuyatambua.