Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Rais Samia: Uchumi wetu unakua lakini tunachokusanya kingi kinaingia mifukoni kwa Watu

Acha kudanganya bwana...!!! Mara ngapi wamekuwa wanampinga CAG kwa taarifa anazotoa? Si unamkumbua Prof Assad?? Zile 1.5T ambazo matumizi yake hayakujulikana, mwenzetu umeyajua? Wana CCM wengi walisimama kidete kutetea ishu ya Tshs. 1.5T lakini hakuna aliyekuwa akisema zipo wapi..!! Ujinga mtupu.

Halmashauri zenye HATI CHAFU umeshawahi sikia mtu kashitakiwa?
Ni ruksa kula kwa urefu wa kamba zao.Alisema mchungaji wao,kwa maana hiyo hakuna kushitakiwa mtu hapa.
 
Hata tukiongeza tax base bado mapato yatakuwa kiduchu maana tatizo lipo kwenye ukusanyaji mapato na si vingine.
 
Yeye mwenye na CCM wenzake ni wakwepa kodi, mshahara wake haukatwi kodi? nilitegemea awe mfano
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo tarehe 04 Oktoba, 2024.
RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi lakini hauakisi mapato ambayo Wananchi wanayapata, amesema hayo wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024.

RAIS SAMIA: UCHUMI WETU UNAKUA LAKINI HAUAKISI TUNACHOKIPATA
Akizungumza wakati akizindua Tume ya Rais ya Marekebisho ya Kodi Dar es Salaam, leo Oktoba 4, 2024, Rais Samia Suluhu Hassan amesema mchakato wa ulipaji kodi unatakiwa kuwa rafiki ili kumwezesha mlipa kodi kukamilisha zoezi hilo ikiwemo mifumo inayotumika.

Amesema kuna umuhimu wa kutoa elimu zaidi kwa walipa kodi ili wajue wanamlipa nani na kiwango gani, akitoa mfano amesema alikutana na changamoto Mkoani Ruvuma ambapo alisema kuna Mama Lishe waliokuwa wakilalamika kuhusu kulipishwa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


=========================

RAIS SAMIA: HATUA MPYA KATIKA MABORESHO YA MFUMO WA KIKODI TANZANIA

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa kiongozi wa kwanza tangu Rais Benjamin Mkapa kuboresha mfumo wa kikodi nchini Tanzania, baada ya kuunda Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi. Tume hii ina lengo la kuangazia changamoto mbalimbali zinazokabili mfumo wa kodi na kutoa mapendekezo yanayoweza kuboresha ukusanyaji wa kodi na ufanisi wa matumizi yake.

Moja ya mambo makuu ambayo Rais Samia anatarajia kuyatekeleza kupitia tume hii ni kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa kodi. Hii ni muhimu katika kujenga imani ya wananchi kwa serikali na mfumo wa kodi, ambao mara nyingi umekuwa ukikabiliwa na malalamiko kuhusu ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma.
Pia, tume hiyo inatarajiwa kuzingatia njia mpya za kukusanya kodi ambazo zitasaidia kuongeza mapato ya serikali bila kuweka mzigo mzito kwa wananchi. Hii inaweza kujumuisha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ukusanyaji wa kodi, kama vile mifumo ya kielektroniki inayorahisisha malipo ya kodi na kuondoa urasimu usio wa lazima.

Aidha, Rais Samia amesisitiza katika ushirikiano na sekta binafsi ili kuboresha mfumo wa kikodi. Ushirikiano huu unaweza kuleta mawazo mapya na mbinu za kisasa katika ukusanyaji wa kodi na pia kutoa fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya uchumi wa nchi.

Kwa kufanya hivi, Rais Samia atasaidia kukuza mazingira ya biashara yanayovutia wawekezaji na kuimarisha uchumi wa nchi. Hii ni muhimu katika kipindi ambacho uchumi wa dunia unakabiliwa na changamoto, na Tanzania inahitaji kuongeza mapato yake ya ndani ili kufikia malengo yake ya maendeleo.
 

Attachments

  • IMG-20241004-WA0041.jpg
    IMG-20241004-WA0041.jpg
    46.1 KB · Views: 0
Shida sio raisi Samia

Shida ni wapumbavu tuliowaweka kumshauri raisi.

Tume ya marekebisho (where on earth umewahi ona kitu kama hiko) kwa jinsi budget ya nchi inavyopangwa na maamuzi ya wizara ya fedha.

Huu ujinga wa watu mnaopeleka Ikulu is beyond me.

Tume ya kodi 😂😂😂
Lini ulimchagua au kuteua washauri wa Rais?
 
Anasema hivi ,juhudi za kukusanya ziongezwe zaidi na kuwabana majizi.

Namuamini bwana Mwenda maana Kwa robo ya kwanza amevuka malengo na haijawahi tokea kabla.

Huyu bwana hana Ubabe lakini anachat na wafanyabiashara so Kwa mara ya kwanza TRA itavuka lengo la Kukusanya Mapato ya Serikali ya Trilioni 30.3 yaliyopangwa.
 
Kama Kodi inaishia mifukoni mwa watu binafsi, Viongozi wahusika wanafanya kazi gani? Mbona hawachukuliwi hatua?
 
Nimeshindwa kumuelewa Rais anaposema nchi ina watu milioni 65 ila wanaolipa kodi ni watu milioni 2 tu!

Najiuliza sipati jibu!

Anataka WENDAWAZIMU, VICHAA, WASIO NA KAZI, WATOTO, VICHANGA walipe kodi!
 
Mtu anayeangalia watu kwanza kuwa hawalipi kodi badala ya kuangalia makampuni makubwa km makampuni ya simu..fahamu hajui analoongea!! hata afanye vipi hatapata jibu..
 
Come 2025 wananchi wafanyanye maamuzi magumu.
Haiwezekani mtu vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo chini yako kisha wahuni wanachota mapesa badala ya kuja kusema nimenyonga kadhaa kwasababu wamedokoa kiasi fulani unalalamika!
Aibu kabisa hii.
 
Come 2025 wananchi wafanyanye maamuzi magumu.
Haiwezekani mtu vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo chini yako kisha wahuni wanachota mapesa badala ya kuja kusema nimenyonga kadhaa kwasababu wamedokoa kiasi fulani unalalamika!
Aibu kabisa hii.
Yeye kwanza ndiyo anatakiwa anyongwe kwa kushindwa kusimamia na kushiriki kwenye wizi wa mali za umma
 
Back
Top Bottom