Kumekuwa na utamaduni wa kudanganywa hata na uongozi wa juu. Mama Samia aliomba riport ya kutekwa tekwa kwa watu nchini. Cha ajabu hakuna mtu anaongelea ripoti na wengi kujisahaulisha. Isije ikawa tena tunadanganya danganywa na uongozi wa juu. Chunguzi nyingi za utekaji hazifanyiki maana watekaji wengi wa watu hasa mashuhuri ni hao hao Polisi na usalama. Mo alitekwa , Lussu alipigwa risasi hatujawahi kuona ripoti yeyote.
Swali kuna mtu hata mmoja anajua Mama anaposema ripoti apewa haraka ni hasa kwa muda gani? Mwezi, Mwaka, siku au ...... ukweli ni kwamba ni siasa tu hakuna ripoti. Ikifika sehemu maneno ya Raisi yanapuuzwa na iwe danganya toto iko siku hao hao Polisi na usalama watamgeuka na wataona powa.