Ni muhimu mno pakawepo na ustahimilivu na subra kwenye hilo,
Nadhani sote ni mashuhuda kwa jinsi ambavyo mashahidi muhimu hususani kutoka vyama vya siasa nchini , wanavyokaidi na kudinda kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uchunguzi mpaka walazimishwe. Huo ni miongoni mwa ucheleweshaji wa makusudi wa muafaka wa jambo hilo..
Na hilo nadhani linaweza kuibua mashaka zaidi na na kuonyesha picha halisi ya ugumu wa kufikia muafaka wa mapema kuhusu jambo hilo baya zaidi kutokea Tanzania.
Nachelea kutoa rai kwa wananchi wenzangu wote, kuwa watulivu, wakati uchunguzi ukiendelea, ili hatimae ukweli wa mambo na wahusika waweze kujulikana na kuchukuliwa hatua mujarabu za kisheria, kwa dhuluma waliyoifanya kwa mwanadamu mwezao 🐒