Rais Samia uliomba ripoti ya "haraka" kuhusu utekaji nchini! Haraka ni muda gani?

Rais Samia uliomba ripoti ya "haraka" kuhusu utekaji nchini! Haraka ni muda gani?

Hiyo ya kuomba uchunguzi haraka ilikuwa ni mbinu tu ya kuwafanya watu wapunguze hasira lakini ukweli mhusika wa kutoa maelekezo ni yeye.mhalifu hawezi kujichunguza .
 
Kumekuwa na utamaduni wa kudanganywa hata na uongozi wa juu. Mama Samia aliomba riport ya kutekwa tekwa kwa watu nchini. Cha ajabu hakuna mtu anaongelea ripoti na wengi kujisahaulisha. Isije ikawa tena tunadanganya danganywa na uongozi wa juu. Chunguzi nyingi za utekaji hazifanyiki maana watekaji wengi wa watu hasa mashuhuri ni hao hao Polisi na usalama. Mo alitekwa , Lussu alipigwa risasi hatujawahi kuona ripoti yeyote.

Swali kuna mtu hata mmoja anajua Mama anaposema ripoti apewa haraka ni hasa kwa muda gani? Mwezi, Mwaka, siku au ...... ukweli ni kwamba ni siasa tu hakuna ripoti. Ikifika sehemu maneno ya Raisi yanapuuzwa na iwe danganya toto iko siku hao hao Polisi na usalama watamgeuka na wataona powa.
Yuko Mkoani Ruvuma kwenye majukumu ya kitaifa kwa ratiba maalumu sawa
 
Ni muhimu mno pakawepo na ustahimilivu na subra kwenye hilo,

Nadhani sote ni mashuhuda kwa jinsi ambavyo mashahidi muhimu hususani kutoka vyama vya siasa nchini , wanavyokaidi na kudinda kutoa ushirikiano kwa vyombo vya uchunguzi mpaka walazimishwe. Huo ni miongoni mwa ucheleweshaji wa makusudi wa muafaka wa jambo hilo..

Na hilo nadhani linaweza kuibua mashaka zaidi na na kuonyesha picha halisi ya ugumu wa kufikia muafaka wa mapema kuhusu jambo hilo baya zaidi kutokea Tanzania.

Nachelea kutoa rai kwa wananchi wenzangu wote, kuwa watulivu, wakati uchunguzi ukiendelea, ili hatimae ukweli wa mambo na wahusika waweze kujulikana na kuchukuliwa hatua mujarabu za kisheria, kwa dhuluma waliyoifanya kwa mwanadamu mwezao 🐒
Usitetee uozo hakuna cha ripoti wala nini, hizo ripoti kila siku zinaimbwa na hakuna hata moja iliyotoka.
 
Acha ufala, huyo ndio mwajiri wake ebo!
Lakini ile kesi ya Tigo kule London imesha toa majibu kuwa wauaji, watekaji na wafanya mipango hiyo ni kina nani.
Ila watambue tuu, utawala mwingine ukiingia madarakani eitha kwa uchaguzi au nguvu ya kijeshi kuna watu mnawaheshimu leo mtawaona Ukonga au Isanga wakisubiri kitanzi.
Taratibu tutafika!
Maaaamako!!
 
Kumekuwa na utamaduni wa kudanganywa hata na uongozi wa juu. Mama Samia aliomba riport ya kutekwa tekwa kwa watu nchini. Cha ajabu hakuna mtu anaongelea ripoti na wengi kujisahaulisha. Isije ikawa tena tunadanganya danganywa na uongozi wa juu. Chunguzi nyingi za utekaji hazifanyiki maana watekaji wengi wa watu hasa mashuhuri ni hao hao Polisi na usalama. Mo alitekwa , Lussu alipigwa risasi hatujawahi kuona ripoti yeyote.

Swali kuna mtu hata mmoja anajua Mama anaposema ripoti apewa haraka ni hasa kwa muda gani? Mwezi, Mwaka, siku au ...... ukweli ni kwamba ni siasa tu hakuna ripoti. Ikifika sehemu maneno ya Raisi yanapuuzwa na iwe danganya toto iko siku hao hao Polisi na usalama watamgeuka na wataona powa.
Mo alitekwa, Lussu (Lisu) alipigwa risasi.

Mtekaji wa Mo na aliemmiminia risasi 16 Lisu ametangulia mbele za haki na Dullah Makabila ameshajua wapi kwa kumpeleka yule maruhuni.
 
Budapest, Hungary

Miklós Németh waziri mkuu wa Hungary anaikumbuka barua ya kutoka kijijini

Baba akiwa kijijini akimuona katika runinga mara tu mwanaye alipoteuliwa kuwa waziri mkuu, kwa haraka alichukua kalamu na karatasi kumkumbushakuwa majukumu aliyopewa yanakwenda na dhamana kubwa.

View: https://m.youtube.com/watch?v=9NSKIu_JZX0

Kuwa watu wote kijijini alikozaliwa wanataka Miklós Németh awe mtu msema kweli muda wote ili wanakijjiji watembee kifua mbele huku wamenyanyua vichwa vyao kufurahia mmoja wao ameweza kuweka historia na legacy iliyotukuka.

Miklós Németh alichaguliwa kwa bahati na chama tawala dola baada ya mtangulizi wake kuondolewa.

Miklós Németh umri miaka 40 tu, aliingia ofisini akijisikia mpweke kwa kuwa vigogo waliomzunguka wote walikuwa wameteuliwa na kuwekwa katika nafasi zao na mtangulizi wake aliyekuwa ana ushawishi.

Vigogo hao waliomzunguka Miklós Németh mgeni aliyeingia kibahati katika nafasi hiyo ya juu serikalini, walikuwa wanajua Miklós Németh hataweza kubakia madarakani kwa muda mrefu kwani Miklós Németh hakuwa na marafiki makada wa juu katika uongozi wa chama tawala.

Vigogo hao wa chama tawala na serikalini walimpa Miklós Németh jukumu zito kurekebisha mambo halafu wangemuondoa.

Miklós Németh kutokana na kukosa ufahamu wa ndani wa mfumo wa chama dola kongwe akaamua badala ya kushughulikia mfumo huo mkongwe akajikita kwa kufungua nchi kiuchumi .

Miklós Németh akamuita waziri wa fedha kumpatia taarifa ya kibajeti inayoonesha uchumi wa nchi unakwendaje.

Miklós Németh akagundua kuna bajeti kubwa zisizoeleweka zinazokula fedha nyingi kupita miradi, lakini kuna mradi uliopewa jina siri lenye herufi tatu tu.

Kumbe herufi hizo tatu katika bajeti ilikuwa ni siri kuu wasiofahamu wengi hata ndani ya chama dola kubwa.

Miklós Németh akaamua bajeti hiyo ya siri ifutwe na kuondolewa iliyokuwa inakula kiasi kikubwa cha bajeti ya taifa.

Vingunge vigogo walio na nguvu kuliko Miklós Németh wakamuita na kumueleza juhudi hizo mpya alizokuja nazo ni hatari kwa mfumo uliopo.

Vingunge wa chama kongwe na wale wa idara za usalama na ulinzi wakamuambia Miklós Németh, sasa tutakusaidia ufahamu nini kinaendelea hivyo panda lifti katika jengo lile utapatiwa ripoti kamili.

Miklós Németh akisindikizwa na wanausalama wakaingia ktk lifti ya jengo hilo nyeti la taifa, na kushangaa lifti badala ya kwenda juu ilionekana dhahiri inakwenda mwelekeo kwenda ghorofa za chini ya ardhi.

Waziri mkuu Miklós Németh kiongozi wa serikali akajikuta katika wasiwasi mkubwa kwa kutofahamu serikali hii aliyoirithi ina mambo mengi asiyoyajua na yasiyojulikana pia na wengi ndani ya serikali. Na lilomshangaza zaidi hata yeye waziri mkuu pia hakuwa amefahamishwa masuala haya mazito.

Miklós Németh akaingizwa katika chumba chenye ramani nyingi ukutani, mezani kulikuwa na vitabu viwili kimoja katika lugha ya KiRussia na kitabu kingine lugha ya taifa.

Miklós Németh akimsubiri mkuu wa wizara ya ulinzi na usalama akagundua nchi inaongozwa kwa ulaghai mkubwa ambao uinaiingiza nchi katika matatizo endelevu yasiyoweza kubebeka, ni muda tu mambo yatakuwa magumu sana kwa nchi yake.

Miklós Németh akakumbuka barua ndefu aliyoandikiwa na babaye kutokana kijijini kwao kuwa Ukweli Pekee Ndiyo Utakuinua binafsi kama kiongozi na pia kulinusuru taifa toka uongo uliokuwa jadi ya mfumo wa serikali ya chama dola kongwe . ....
 
Kumekuwa na utamaduni wa kudanganywa hata na uongozi wa juu. Mama Samia aliomba riport ya kutekwa tekwa kwa watu nchini. Cha ajabu hakuna mtu anaongelea ripoti na wengi kujisahaulisha. Isije ikawa tena tunadanganya danganywa na uongozi wa juu. Chunguzi nyingi za utekaji hazifanyiki maana watekaji wengi wa watu hasa mashuhuri ni hao hao Polisi na usalama. Mo alitekwa , Lussu alipigwa risasi hatujawahi kuona ripoti yeyote.

Swali kuna mtu hata mmoja anajua Mama anaposema ripoti apewa haraka ni hasa kwa muda gani? Mwezi, Mwaka, siku au ...... ukweli ni kwamba ni siasa tu hakuna ripoti. Ikifika sehemu maneno ya Raisi yanapuuzwa na iwe danganya toto iko siku hao hao Polisi na usalama watamgeuka na wataona powa.
Ripoti tulishampa tayari.
 
Kingunge kigogo ajiuzulu uMakamu mwenyekiti wa CCM, alikuwa mstari wa mbele katika mazungumzo ya muufaka kuhusu mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi kuelekea 2024 na 2025

Mzee Abdulrahman Omar Kinana ajiuzulu

1728764832766.jpeg
 
Miklós Németh waziri mkuu wa Hungary anaikumbuka barua ya kutoka kijijini
1728765299290.jpeg

KUNA upepo fulani hivi umepita ndani ya CCM, chama tawala chenye umri wa miaka 47 ya kuzaliwa, lakini 70 ya kuona dunia, ikizingatiwa kuwa kilitokana na muungano wa Tanganyika African National Union (TANU) na Afro Shiraz Party (ASP) ya Zanzibar.

Upepo huo umetikisa matawi ya miti iliyooteshwa ndani ya chama hicho, baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti , komredi Abdulrahman Kinana, kuamua kujiuzulu uongozi lakini kuendelea kubaki ndani ya chama hicho.

Hadi leo oktoba 2024 Halmashauri Kuu ya Taifa NEC na Kamati yake Kuu CC hawajaweza kuteua kada wa CCM kuingia katika nafasi hiyo nzito ambayo imeonekana miaka ya nyuma ilitumika vizuri kukibeba chama nyakati za chaguzi za TAMISEMI na Uchaguzi mkuu.

Ni nadra sana kiongozi hususan wa Tanzania kujiuzulu bila kutenguliwa nafasi yake maarufu kama kutumbuliwa, sijui inatokana na nini, lakini inawezekana kila mtu ana wazo lake katika hilo, ila itoshe tu kusema inahitaji roho ngumu..
 
1728765711094.jpeg

Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana akiwa katika uongozi wa chama alijijengea taswira ya mfano. Alikatiza porini na kuvuka mito, maziwa na bahari kukipa uhai chama.

Kinana alikuwa mwenye kukisemea chama hasa. Alikuwa tayari kugombana na mawaziri wa Serikali iliyoongozwa na mwenyekiti wake (Kikwete), ili kuwafanya wananchi waone kwamba CCM ni chama chenye kujali na kutetea masilahi ya umma. Alitaka ionekane kuwa makosa ya Serikali chanzo chake siyo CCM.

Kinana chini ya Kikwete alitaka mawaziri wawajibike kwenye chama.

Kibao hicho cha Kinana kimerejea chini ya bosi wake Mwenyekiti Dr. Samia Hassan. Hotuba yake mara tu alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, ameweka wazi azma yake ya kutaka Serikali iwe inahojiwa na kujieleza mbele ya chama kwa kuwa ndicho huomba kura ...
 
Kawatangazia Watanzania ili mapoyoyo wafahamu kuwa linamuum na analifanyia kazi.

Lakini hajasema kuwa ripoti anazopewa ni kwa ajili ya macho na masikio ya kila mtu.

Ripoti nyingi tu za kiusalama huwa zinafanyiwa kazi kimya kimya na wahusika ni wale walioapishwa tu.

Nchi zina siri kubwa sana.

Nadhani hata wewe, kwenye ukoo wako tu, kuna siri ambazo huzitangazi.

..ripoti inayohusu mauaji ya mwananchi kama Mzee Ally Kibao haipaswi kufanywa siri.
 
Back
Top Bottom