Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Ndio siasa zilivyo ni lazima kiongozi uwe na ngozi ngumu. Ni wapinzani hawawezi kukuunga mkono mpaka suala liwe la wazi sana ambalo hawawezi kulipinga.Mie nilisema mapema, Mh. Rais wangu SSH achana na wapinzani, piga kazi, hao watukuzodoa, watakudharau, watakutukana, watakuona huna maana hata uwafanyie nini, Mh. Rais akianza kutaka kuwadhirisha wapinzani ni sawa na kujaza maji gunia.
Umeona Lissu alivyogeuka, umeenda kumuona, umempatia passport, umeahidi uso kwa uso kushughulikia maslahi yake aliyokuwa analilia kutwa, bado anasema ww sio alivyokufikuria, kasema vibaya sana juzi kati ulivyokutana na ile tume ya kutoa maoni ya vyama vya siasa.
Lissu au Mbowe hata ufanye nini, ni bure kabisa, huwezi kuwaridhisha. Achana nao. Umeona juzi Mbowe kwenye jukwaa akikunanga.
Pia tukumbuke kuwa roho mbaya huzaa mabaya baadae, cha muhimu ni kuwa wavumilivu siku zote. Kumbuka SSH kachukua pesa nyingi za wazungu hivyo kwa namna moja ama nyingine analo deni la kuongoza nchi yenye haki na usawa kwa hao hao wahisani.