Rais Samia unajiandalia majuto ambayo hutayasahahau kwenye maisha yako ya kisiasa

Ndio siasa zilivyo ni lazima kiongozi uwe na ngozi ngumu. Ni wapinzani hawawezi kukuunga mkono mpaka suala liwe la wazi sana ambalo hawawezi kulipinga.

Pia tukumbuke kuwa roho mbaya huzaa mabaya baadae, cha muhimu ni kuwa wavumilivu siku zote. Kumbuka SSH kachukua pesa nyingi za wazungu hivyo kwa namna moja ama nyingine analo deni la kuongoza nchi yenye haki na usawa kwa hao hao wahisani.
 
Hatuna compromise kwenye haki za watu. Mnaojiona kwa kuwa mpo CCM mnafaidika sana mnajidanganya sana na mnajivika ujinga.

Nchi hii ni moja, ubovu wa siasa unapelekea ubovu wa serikali, na serikali ikiwa mbovu, kila kitu katika nchi kitakuwa kibovu.

Madhara ya Ubovu wa nchi hayachagui vyama. Wote mtasoma elimu duni, mtaamrishw na wala rushwa na mafisadi, mtapigwa na ugumu wa maisha, mtakosa huduma hata zile za kawaida kabisa kama maji, umeme, huduma za matibabu na madawa hospitalini, mtauliwa kwa sumu (Mto Mara), mtaporwa mali zenu mlizozitolea jasho, mtaishi kwenye makazi holela, nk.

Kwa ufupi, mtakufa mkiwa mmechoka sana, na mbinguni huenda msifike kwa kuwa mlikubali kuishi chini ya mfumo wa kishetani (unaoamini katika kuwanyima watu haki) huku duniani.

Taifa linalotaka kuendelea halipaswi kuongozwa kwa uongo uongo na ujanja ujanja kama CCM inavyofanya.

Chini ya hawa waliopo na wanaowashabikia, nchi itachelewa sana kupiga hatua ya kimaendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…