Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Rais Samia; Urais wa nchi ni mambo makubwa

Ndio maana tunasema Magufuli ni mwanaume, hivi hiyo miaka 54 unayoitaja kwa akili yako ni nini kilifanyika?

kulijengwa reli mpya, kulinunuliwa ndege mpya 12, kulijengwa meli mpya, kulijengwa vivuko, kulijengwa madaraja haya yanayojengwa leo,
Vipi mahospitari yalijengwa,

mastandi ya mabasi yalikuwepo, vipi vituo vya afya ktk hiyo miaka mitano tu.

tukikuambia una chuki mbaya na mwendazake unachukia mpaka unaziba macho kujifanya huoni chochote.

Ww ni bendera fuata upepo ndio maana unataja miradi mingi huku hujui hata thamani yake. Wingi wa miradi haimaanishi inafikia hiyo thamani ya 30t. Kwa taarifa yako hospitali zote, vituo vya afya nk miradi hiyo haijafikia 500b, madaraka yote yaliyojengwa na yaliyokuwa kwenye hatua ya ujenzi hayajavuka 2.5t. hizo mali zote na vivuko kwa ujumla wake havivuki 1t. Kwa haraka haraka hiyo ni chini ya 5t. Reli na Bwawa mpaka sasa hazijatoka zaidi ya 12t. Je ni kipi linapandisha hiyo figure kuwa 30t, huku akikusanya kodi zaidi ya 1.3t@ month, na akiwa hajaajiri wala kupandisha mishahara?
 
Tindo, mwombe Mwenyeji Mungu sana akusaidie kujijua jinsi ulivyo mjinga na roho mbaya, yaani kiufupi ujitambue

Nina roho mbaya kweli, na nilijifunza kutoka kwa dhalimu. kujitambua ni kukubali propaganda mfu.
 
Mimi huwa naamini ili tuendelee si lazima sana kuwa na Rais wa haja ya mioyo yetu au mchapakazi sana n.k.

Ili waafrika tuendelee tunahitaji
1. Kubadili fikra zetu kutoka kuwa tegemezi na kuwa na fikra vumbuzi/tatuzi...

2. Kutunza rasilimali tulizonazo, na kuhakikisha zinatufaidisha, hili lilipaswa kuwa ni jukumu la kila mwenye dhamana...kama madini tuliyonayo yangelikuwa managed vizuri pengine leo hii tusingekuwa hivi tulivyo...
 
Habari wana JF,

Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.

Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.

Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!

Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere.

1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa.

Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.

Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.

Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.

Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!

Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?

Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!

Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu.

2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.

Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?

Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.

Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.

Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.

Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.

Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.

Naomba hii iwe part 1

Asante Mh Rais kwa usikivu wako.
umesemea matatizo ya watanzania kwa lugha nyepesi sana sasa kwa kuwa mama huwa anapitia mitandaoni ataona na huu ushauri na kuufanyia kazi
 
Equation ya hiki unachokisema hapa hakiwezi kuwa triggered na mtu mmoja bali collective efforts.

Kuna makundi mawili ambayo haya hayawezi kubadili mentality zao kwakua wamejinasibu kama injini ya mambo kusonga.

Kundi la kwanza la play makers hawa wanajulikana kama watu wa system ambao ni TISS, JUDGES NA JWTZ top ranking official.

Kundi hilo hapo juu ndio moyo wa mambo kwenda au kukwama nchi hii na hawa wanakula 30% ya keki ya Taifa na nitakuambia kitu. They deserve kwakua a single mistake we are all doomed.

Kundi la pili ni la Wanasiasa na wakurugenzi hawa hawapitishi tu maslahi ya kundi la kwanza bali wanajiweka nao hapo na kwakua kundi la kwanza maslahi yao yanalindwa na kundi hili hawana muda wa kuhoji kwakua huzibwa midomo kwa kuongezewa ambacho hawajaomba.

Tatizo la kundi hili la pili hawastahili wanachopata wakiwa madarakani na hata baada ya kuondoka. Kwakua they are just matairi ambayo hayahitaji kutizamwa baada ya kuondolewa kwenye gari.

TATIZO LINAPOANZIA:
Kundi la pili linatakiwa kuja na mikakati ya kukusanya zaidi ili waweze kupeleka kwa wananchi baada ya kutenga fungu la kundi la kwanza.

Sasa hawa Wanasiasa na Wakurugenzi wanaishia kuuza nyago tu na hawana la maana wanalofanya.

Mfano:
TRA/BANDARI/HALMASHAURI NA MANISPAA hawana weledi katika majukumu yao ambapo ndipo fedha inapopotelea...

Hivi unadhani ni kiasi gani cha fedha serikali itakusanya iwapo itatoa kwa kila mfanyabiashara mwenye eneo shilingi 364,000/_ kwa mwaka kwa biashara anayofanya ambayo ni Sawa na shilingi 1000 tu kwa siku?

Manispaa/Halmashauri zikiamua kukusanya kodi ya majengo tu Tanzania nzima kila jengi shilingi 364,000/- kwa mwaka ambayo ni Sawa na hilo 1000 kwa siku?

Hivi TPA wakiamua kutoza 100,000 kwa kila contena ya 40ft inayopita bandarini pale?

Mambo ni mengi sema kundi la pili ndio kikwazo

Wasalaam
Hilo la watu wa manispaa umenifanya nisikie uchungu ka mwendazake alivyokuwa anasikia uchungu mpaka kujaribu kuwapa idea zake ( vitambulisho vya mmachinga),

hawa watu ni ziro kabisa hawana ubunifu wowote, wapo pale kwa maslahi yao tu na kutoa vibari, hawana jipya (angalia walivyomshambulia mkuregenzi wa kinondoni Spora Liana)

hawa watu hata kuwa na ubunifu wa kujenga vituo vya kupumzikia (bustani nzuri hawana)

nchi nyingine wamachinga hawahawa kwa maeneo ambayo wapo wangweza kutengenezewa vibanda safi vya kiubunifu na wenyewe kukusanya kodi hawana,

halafu utegemee siku moja miji yetu itakuwa mizuri kwa watu kama hawa!!!!!
 
au Rais wa nchi ananunua mapapai na kuwagaia wananchi,tuko serious kweli nchi hii?
Wewe ndio haupo serious na mambo madogo kama hayo,
Hivi wewe unaweza kumnunulia mtoto biscuit au pipi ukitoka kazini kweli???

watu wengine bwana, kama huna cha kuongea kaa kimya na chuki zako
 
Hilo la watu wa manispaa umenifanya nisikie uchungu ka mwendazake alivyokuwa anasikia uchungu mpaka kujaribu kuwapa idea zake ( vitambulisho vya mmachinga),

hawa watu ni ziro kabisa hawana ubunifu wowote, wapo pale kwa maslahi yao tu na kutoa vibari, hawana jipya (angalia walivyomshambulia mkuregenzi wa kinondoni Spora Liana)

hawa watu hata kuwa na ubunifu wa kujenga vituo vya kupumzikia (bustani nzuri hawana)

nchi nyingine wamachinga hawahawa kwa maeneo ambayo wapo wangweza kutengenezewa vibanda safi vya kiubunifu na wenyewe kukusanya kodi hawana,

halafu utegemee siku moja miji yetu itakuwa mizuri kwa watu kama hawa!!!!!
Brother ukifanya kazi serikalini hasa Halmashauri unakuta mtu ana MAs lakini hawezi kujisogeza wala kujigusa
 
Ww ni bendera fuata upepo ndio maana unataja miradi mingi huku hujui hata thamani yake. Wingi wa miradi haimaanishi inafikia hiyo thamani ya 30t. Kwa taarifa yako hospitali zote, vituo vya afya nk miradi hiyo haijafikia 500b, madaraka yote yaliyojengwa na yaliyokuwa kwenye hatua ya ujenzi hayajavuka 2.5t. hizo mali zote na vivuko kwa ujumla wake havivuki 1t. Kwa haraka haraka hiyo ni chini ya 5t. Reli na Bwawa mpaka sasa hazijatoka zaidi ya 12t. Je ni kipi linapandisha hiyo figure kuwa 30t, huku akikusanya kodi zaidi ya 1.3t@ month, na akiwa hajaajiri wala kupandisha mishahara?
Nielewe tena, 30tr, iulizie imetumika vipi miaka 10au 15 ijayo sio leo ndugu!!

hizo figure ulizotaja za miradi hiyo mbona miaka na miaka hatukuona hiyo miradi ikijengwa mpaka alipokuja mwendazake?

au wenyewe walikuwa hawakusanyi kodi?
 
Hiyo Miaka 10 au 15 ni ya marejesho. Inaonekana umezaliwa miaka ya 2,000. Hivyo vyote vilikuwa enzi za Nyerere, ila vilikosa mwendelezo. Bomba la mafuta la Zambia, Reli ya Tazara, ndege nyingi, viwanda vya kutosha vilikuwepo enzi za Nyerere. Mabwawa ya umeme pia yalikuwepo na bado deni halikupanda kwa hivi. Umepigwa propaganda juzi ukaona ndio hivyo, hata uwezo wa kujiuliza uwiano wa deni na miradi huna, umebakia kunitajia miradi kwa wingi, lakini hata thamani yake hujui.
 
Brother ukifanya kazi serikalini hasa Halmashauri unakuta mtu ana MAs lakini hawezi kujisogeza wala kujigusa
Mimi huwa najiuliza, kwani huko serikalini wafanyakazi huwa hawapimwi kwa kitu walichofanya au kugundua kila mwisho wa mwaka?
Maana kwa aina hii ya utendaji hata aje Rais wa namna gani hatutafika popote!
Rais anahitaji watu wa kumsaidia kufanya kazi yake iwe rahisi,

mimi siku zote huwa naamini kwa hali tuliyofikia na viwango vya Elimu iliyofikiwa kwa sasa hatuna haja ya kulialia kuhusu elimu tena, ni kwamba uwezo wa ufahamu wetu ndio umeshagota hapo,

tunatakiwa kujitoa muhanga sasa kuomba msaada kwa manalozi wa nchi nyingine zilizopiga hatua ya kimaendeleo watuletee watu wa management ili sisi tuwe pembeni tuone wenyewe wanafanyaje kazi na sisi angalau tuige.
Au la , basi tuwe na mkakati mkubwa sana wa kupeleka watu wetu kwenda kufanya kazi huko kwa muda (intern) hata kwa mwaka 1 na sisi kama nchi tuwalipe huko,

maana kwa hali iliyopo ni kwamba tumedumaa hasa!!!
 
Hiyo Miaka 10 au 15 ni ya marejesho. Inaonekana umezaliwa miaka ya 2,000. Hivyo vyote vilikuwa enzi za Nyerere, ila vilikosa mwendelezo. Bomba la mafuta la Zambia, Reli ya Tazara, ndege nyingi, viwanda vya kutosha vilikuwepo enzi za Nyerere. Mabwawa ya umeme pia yalikuwepo na bado deni halikupanda kwa hivi. Umepigwa propaganda juzi ukaona ndio hivyo, hata uwezo wa kujiuliza uwiano wa deni na miradi huna, umebakia kunitajia miradi kwa wingi, lakini hata thamani yake hujui.
Baada ya Nyerere wamepita marais wangapi,
Nampenda sana Nyerere, lakini Nyerere ndio alijenga reli ya kati, hiyo TAZARA inaprogress vipi mpaka leo,
Unajua hayo mabwawa ya Nyerere yanatoa MEGAWATTS ngapi kuendana na populations ya leo ( hazifiki hata 600), compare na Mwendazake,
Hizo ndege zipo wapi sasa hivi!

hivi unakumbuka kama Taifa tulifikia kukodisha ndege kama national carrier ALLIANCE AIR) na tukaishia kupigwa tu,

leo taifa lina ndege zake unaishia kubeza,,!!

MSWAHILI BWANA ni shida tu,
 
Naumia sana nchi yetu ni nzuri sana, lakini kila mara tunaonekana kama tumepata Rais nusu, yani naumia sana.
Kufa Kama maumivu yamedhidi,,ili umfuate Rais kamili uko alipo kuzimu,uyu si Rais nusu
 
Mimi huwa najiuliza, kwani huko serikalini wafanyakazi huwa hawapimwi kwa kitu walichofanya au kugundua kila mwisho wa mwaka?
Maana kwa aina hii ya utendaji hata aje Rais wa namna gani hatutafika popote!
Rais anahitaji watu wa kumsaidia kufanya kazi yake iwe rahisi,

mimi siku zote huwa naamini kwa hali tuliyofikia na viwango vya Elimu iliyofikiwa kwa sasa hatuna haja ya kulialia kuhusu elimu tena, ni kwamba uwezo wa ufahamu wetu ndio umeshagota hapo,

tunatakiwa kujitoa muhanga sasa kuomba msaada kwa manalozi wa nchi nyingine zilizopiga hatua ya kimaendeleo watuletee watu wa management ili sisi tuwe pembeni tuone wenyewe wanafanyaje kazi na sisi angalau tuige.
Au la , basi tuwe na mkakati mkubwa sana wa kupeleka watu wetu kwenda kufanya kazi huko kwa muda (intern) hata kwa mwaka 1 na sisi kama nchi tuwalipe huko,

maana kwa hali iliyopo ni kwamba tumedumaa hasa!!!
Ukiamua kuwapima waajiriwa wa serikalini kwa KPI utajikuta unamfukuza hata huyo Mkurugenzi mwenyewe.

Sema hilo ni tatizo la Dunia nzima Government official wanakua Hawaii vizuri sana katika utendaji Kazi
 
Habari wana JF,

Binafsi nafurahia uongozi wako Mh Rais Samia, lakini napenda kutoa mtazamo tofauti ili kuboresha kwa kuwa bado una muda.
Rais wangu, asikudanganye mtu, Uongozi wa Nchi ni mambo makubwa, ni juu ya hatma ya kesho, sio leo tu, ni juu ya leo na vizazi vijavyo.

Nchi hii bado ni maskini sana, askidunganye mtu. Wanachi wetu bado ni fukara wa kutupwa, asikudanganye mtu yeyote.
Ninatembea kila kona ya Tz, wanachi wako bado ni fukara sana. Kupiga siasa pekee hakutawasaidia wananchi wako.

Hivi mheshimiwa Rais unajua zipo wilaya, % kubwa ya watu wake hawawezi hata kulipia hela ya kufungua jalada hospitali?
Ni Elfu 1 tu, lakini hana na hapo ni ugonjwa. Anaumwa kwelikweli!

Ngoja nizungumze kidogo kama Nyerere.

1. Tunataka Rais anayejua hali halisi za wanachi wake, kwamba Watanzania bado ni maskini sana.
Bado tu fukara sana. Bahati mbaya ni kwamba mfumo wetu wa kiuongozi unawatenga sana nyinyi mliojuu na sisi wa huku chini.
Ni hakika ukiwa Rais nchi hii huwezi abadani kuhisi shida za watu wako. Shida MFUMO. Shida WAPAMBE.
Watakwambia aaah!, mambo yako sawa Mheshimiwa.

Nitoe mfano halisi kwenye Uongozi wako.

Jana ukiwa na wanawake kwa mara ya pili, binafsi, nimekusikia ukisemea swala la maiti kuzuiwa ktk hospitali za umma ili kulipwa gharama za matibabu.

Ukasema (na uliwahi kusema), Wizara iangalie, labda mgonjwa awe anapewa bili yake kidogo kidogo kadri anavyoendelea na tiba!
MOYO WANGU UNAUMIA SANA.

Hebu Mh Rais yachimbe haya mambo kiundani. Wajue wananchi wako kiundani, itakusaidia. Wananchi wako ni fukara sana, asikudanganye mtu!!

Tatizo sio bili kidogo kidogo! Okay tuseme amelazwa, siku ya pili akapewa bili akashindwa kulipa yote, je madaktari wasitishe huduma ili alipe kwanza?

Hivi maskini anayevumilia maumivu ya kichwa asiweze kununua panadol, ndiye wakupewa bili kidogo kidogo!

Wapo watakaonishambulia hapa, kwamba unataka Rais asemeje, watibiwe bure?! Okay wasikilize tu.

2. Tunataka Rais anayejua kwamba UJINGA, UMASKINI na MARADHI sasa ni maadui waliokubuhu.

Unaogopa nini kuvunja-vunja mfumo wa elimu yetu huu, uutengeneze upya?

Tuna elimu ya ajabu, hata vitabu wanavyosoma watoto wetu leo havichangamshi akili hata kidogo.

Halafu hii ya kujenga shule moja ya wasichana kila mkoa, kwamba tunajaribu au? Hebu Mama acha Legacy, usijaribu-jaribu.

Tunahitaji Rais anayewajua Watanzania wote, kuanzia Machinga, Wakulima, Matajiri, Wafanyabiashara, Wafanyakazi, Wawekezaji, Rika zote, Rangi zote, Jinsi zote, Kabila zote, n.k.

Tunataka Rais anayejua kwa dhati kuwa huu ni "uzandiki" na huu ndio "ukweli", na akatae waziwazi uzandiki wowote ule hata kama umeletwa na rafiki/ndugu yake.

Tunataka Rais anayejua shida za watu wake, 'Matajiri na Maskini', maana wote tajiri na maskini wana shida/mahitaji.
Anayejua kuwa wote wanatakiwa kusaidiwa bila upendeleo, wala kukanyaga mgongo wa mwingine.

Naomba hii iwe part 1

Asante Mh Rais kwa usikivu wako.
Huyu raisi unaye mtaka alikuja toka ubeligiji, akatuletea sera ya mpango wa bima ya afya kwa wote, Cha kushangaza mkamuibia kura, mkamtishia kumuua akaondoshwa na wasamaria wema
 
Tumpe muda gani zaidi? Tangu March Hadi Sasa hajamaliza kuteua . Bado madc,maded wa halmashauri,,makatibu tawala. Speed yake ni ndogo sana sana. Songwe na kigoma atafika lini?
Hama nchi Kama unaona anakuchelewesha,,jizi wewe
 
Binafsi hii nchi aliiweza magufuli peke ake, ili maendeleo yawepo uvunjifu wa mfumo wa kidemokrasia lazima uwepo. hivi viatu alivyovaa mama etu mpendwa ni vigumu na vinahitaji utulivu wa mwili na akili, kwa mwanamke ambaye ameumbwa kuongozwa hawezi kutufikisha popote. unajua hayati hakuwa akimsikiliza kila mtu alifanya vile akili yake ilivyomtuma maana alijua miluzi mingi humpoteza mbwa pia alijua kuwa nchi haijengwi kwa siasa bali kwa jasho na damu na ndo maana alikuwa tayari kupoteza damu yake ili kuleta maendeleo yenye tija, tuache kuwa wabinafsi richa ya kuwa wananchi wengi ni fukara ila hayati alipambana kuijenga nchi kuwaacha wananchi wanaumia ili vizazi vyao vije vifurahie matunda ya jasho za baba zao, ila watanzania wengi hatupo tayari kujitoa kwaajili ya future ya watoto wetu, kila mmoja ana roho ya ubinafsi anaona ni bora aje ateseke mtoto wake ila yeye ale matunda ya nchi. na ndo maana hatukusita kumpinga. Ok turudi kwenye mada, katika kitu cha umuhimu ambacho raisi anatakiwa kukifanya ni kuhakikisha anabadilisha mfumo wa elimu na kuongeza idadi ya technical schools and colleges ili kutengeneza watu wanaoweza kujiajili, pia angewekeza katika kuwapa sapoti local inovators ili kuikuza teknolojia yetu maana hili litapunguza cost burden kwenye foreign importation, huenda maraisi waliopita wangewasapoti local inovators sasa ivi tungekuwa tunatengeneza magari yetu wenyewe, viwanda vingekua, un employment rate ingepungua, kilimo kingebadirika na watu wangevuna mpaka wasingekuwa na mahali pa kuvipeleka vyakula, ila kwa sababu mawazo yao yamefungwa ndo maana akitokea mtu amegundua kitu anasainiwa na mataifa ya kibeberu ili wakawanufaishe wazungu waje watunyonye wakati sisi tunamuona mpuuzi eti hakina quality kitahatarisha maisha ya watu ivii mmesahau kuwa hata britain iliyosumbua kuwa na viwanda vikubwa karne ya 16 walianza na mfumo mdogo (stem engine)?. nchi yetu inahitaji raisi mwenye fikra za kujilisha wenyewe na sio kuombaomba maana hata marekani inapasua vichwa kwa kuwa ba uchumi mkubwa duniani kwa sababu ilipata maraisi wenye akili, wenye kushindana kuiondoa nchi kutoka kwenye umasikini na sio kushindana kwa kiki, tukiendelea kukaza vichwa tutabaki nyumanyuma kama koti la babu msizilo, wazungu wataendelea kututafuna vichwa wakati sisi tukiendelea kuwachekea.
yangu ni hayo tu wakuu.[emoji120][emoji120]
Sawa Kama hii nchi tangu ipate uhuru aliiweza msukuma mwenzenu magfuli, nendeni na gwaji boy mkampe pumzi aje amalizie ingwe,
 
Siku hizi mtu huwezi hata kutoa constructive criticism humu bila ya kuambiwa unamchukia Samia!

SMH
Sio tu unamchukia Bali utaambiwa wewe Ni sukumagang mnufaika wa marehemu Magufuli muombolezaji usieamini jamaa yako kafa....
Dunia Ina Mambo hii
 
Back
Top Bottom