Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Miongoni mwa mambo makubwa atakayokumbukwa nayo Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Kikwete ni ujenzi wa shule za Kata na Ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma. Licha ya changamoto zilizopo, bado wazo la ujenzi wa shule ya sekondari kila kata limekuwa na msaada mkubwa kwenye jamii tofauti na huko nyuma. Na kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dodoma, hakika ile ni legacy ya milele kwa comrade Jakaya.
Rais Samia naye anaonekana kuipenda sekta ya Elimu kwa ujumla wake na huenda hii inatokana na kauli yake aliyoitoa hivi karibuni alipoulizwa unataka kuiona Tanzania ya namna gani na yeye kusema angependa kuiona Tanzania yenye watu wenye uelewa na maarifa/ujuzi (skilled and knowledgeable society). Hili ni jawabu mujarabu kabisa.
Msingi wa maendeleo tunayoyaona leo Ulaya, Amerika, East Asian countries, China, Japan na kwingineko, SIRI yake kubwa ni kutengeneza jamii yenye ujuzi na uelewa. Full stop. Na kwa hakika, jamii yetu ya kitanzania kama kuna biggest "binding constraint" inayodumaza maendeleo ya Tanzania basi ni watanzania wenyewe. Uelewa, maarifa, ujuzi, nidhamu na yanayohusiana na hayo ni tatizo kubwa kwa jamii ya Kitanzania. Dawa ya matatizo haya ni Elimu tu, si kingine.
Rais Samia ameanza kwa vitendo safari ya kuijenga jamii ya kitanzania yenye uelewa na ujuzi wa mambo kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu na upatikanaji wa vifaa vya elimu, ikiwa pamoja na ujenzi wa vyuo vya ufundi kwa kila Wilaya. Sambamba na hilo Rais Samia ameshaanza kujenga Chuo Kikuu cha TEHAMA kule Dodoma. Natamani chuo hiki kiwe katika kiwango cha "world class" vifanane na vyuo kama Hong Kong University of Science and Technology (HKUST), kule Hong Kong au Georgia School of Technology (Georgia Institute of Technology) aka Georgia Tech cha Marekani. Ujenzi wa vyuo vya namna hii utaleta ubunifu katika jamii ya Kitanzania.
Ombi na ushauri sasa kwa Mama. Katika jitihada hizohizo, tafadhali usiache kujenga vyuo vikuu viwili, kimoja Mtwara na kingine Bagamoyo. Cha Mtwara kiwe maalum kwa masuala ya Gesi na bidhaa za petrol kinaweza kuitwa Mtwara University of Gas and Petroleum Products. Bagamoyo ni kutekeleza ule mpango wa siku nyingi wa kuboresha chuo cha Mbegani na hiki kinaweza kuitwa Bagamoyo University of Fisheries and Marine Products (BUF).
Kwanini vyuo hivi? Ni kwasababu katika hayo maeneo hayo tuna FURSA (potential) ya kutosha ambapo kuna wigo mpana wa kutafiti na kuzalisha brains zitakazoweza kusaidia nchi kuanzishwa kwa projects nyingi na kuleta ajira kwa watanzania. Huko kuna utajiri wa kutisha. Bahari ina mambo mengi na tafiti zake still ni highly demanded duniani.
Kuwa na ukanda wa Bahari mrefu wa aina yetu (takribani km 1400+) si jambo la afya kutokuwa na chuo cha kisasa Ili kuchochea tafiti katika maeneo hayo. Halikadhalika, ni wakati sasa wa kuandaa vijana wenye skills katika maeneo ya Gas na petro- industries na mazao yake.
Ukifanya haya, utakuwa ungeacha alama ya milele kwa nchi yako hii na Rais ajaye tutamuomba ajenge vyuo vya michezo kila Wilaya Ili kuitumia fursa ya Dunia ya kuzalisha wanamichezo katika fani mbalimbali. Aisha anaweza kujenga Chuo Kikuu pia cha michezo na ingefaa chuo hiki kijengwe Arusha au Manyara.
Ni jambo la aibu kila siku kuwaona Kenya, Ethiopia kwenye riadha na kuwaona kwa wingi kina Mane, Kanoute nk. Utajiri ulioko kwenye michezo ni mkubwa na hauna dalili ya kuporomoka kwa utajiri huo.
Kazi iendelee.