Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ndugu Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Zilikuwepo taarifa hapa nchini kuwa Mwezi wa kuhitimisha mfungo mtukufu wa Ramadhani umeonekana katika baadhi ya maeneo nchini (Kagera ni mmojawapo) jioni ya tarehe 1/5/2022, Lakini viongozi wakuu wa BAKWATA hawakuutangazia umma juu ya ukweli huo wa muandamo wa mwezi.
Na minong'ono inayopita ni kwamba viongozi hao wa BAKWATA wanafanya hivyo kwa sababu wanataka tu watimize ratiba yao ambayo wameshaipanga toka mapema itakayowahikikishia uwepo wako wewe katika hadhara yao hiyo, Kwamba eti wakiitisha Iddi mapema basi mipango yao hiyo itaharibika.
Mheshimiwa Rais, Suala la Iddi ni suala la Ibada kubwa sana, na inafahamika vyema kwamba mtu kufunga siku ya iddi ni dhambi , Sasa iweje watu waahirishe Iddi ili tu ilimradi waweze kupata ratiba itakayomfit mkuu wa nchi kuhudhuria siku wanayoitaka wao?
Mheshimiwa Rais yawezekanaje nchi nyingi za Africa mashariki wanakula Iddi siku ya Tarehe 2/5/2022 ila tu eti sisi Tanzania tuwe tofauti wakati inajulikana vyema kuwa zamani katika Afrika ya mashariki tulikuwa tukila Iddi siku moja?
Mheshimiwa Rais, Yaani Tanga iliyo karibu na Mombasa isiwe Iddi wakati mwezi umeonekana Kenya kweli hii inakubalika katika mantiki?.
Mheshimiwa Rais, inasemekana mwezi hata ukionekana mahali hapa nchini, na hata viongozi wa kidini wakitoa taarifa zao kwa viongozi wao wakuu wanaogopa kutoka hadharani na kuzifanya zienee kwa kuhofia nafasi zao za kiutawala ndani ya BAKWATA
Mheshimiwa Rais, hili suala la mwezi nchini limegeuka suala la kuflex muscle, yaani kutunishiana msuli baina ya waislamu wenyewe kuwa ni nani ambaye waislamu wengi wanamfuata zaidi, na hapa BAKWATA huwa ndo hupata nafasi ya kuonyesha taasisi nyingine kuwa sisi ndiyo sisi na waislamu wanatusikiliza sisi!
Mheshimiwa Rais, nakuomba kesho usihudhurie baraza hili la Iddi ili kutuma meseji kuwa huna mchezo kwenye mambo ya Mwenyezi Mungu na wasikuingize katika mitihani ya kumuasi Allah sababu tu ya "ulua"wa kidunia.
Asante sana