Rais Samia usihudhurie Baraza la Iddi ili kukomesha siasa katika dini

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Ndugu Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Zilikuwepo taarifa hapa nchini kuwa Mwezi wa kuhitimisha mfungo mtukufu wa Ramadhani umeonekana katika baadhi ya maeneo nchini (Kagera ni mmojawapo) jioni ya tarehe 1/5/2022, Lakini viongozi wakuu wa BAKWATA hawakuutangazia umma juu ya ukweli huo wa muandamo wa mwezi.

Na minong'ono inayopita ni kwamba viongozi hao wa BAKWATA wanafanya hivyo kwa sababu wanataka tu watimize ratiba yao ambayo wameshaipanga toka mapema itakayowahikikishia uwepo wako wewe katika hadhara yao hiyo, Kwamba eti wakiitisha Iddi mapema basi mipango yao hiyo itaharibika.

Mheshimiwa Rais, Suala la Iddi ni suala la Ibada kubwa sana, na inafahamika vyema kwamba mtu kufunga siku ya iddi ni dhambi , Sasa iweje watu waahirishe Iddi ili tu ilimradi waweze kupata ratiba itakayomfit mkuu wa nchi kuhudhuria siku wanayoitaka wao?

Mheshimiwa Rais yawezekanaje nchi nyingi za Africa mashariki wanakula Iddi siku ya Tarehe 2/5/2022 ila tu eti sisi Tanzania tuwe tofauti wakati inajulikana vyema kuwa zamani katika Afrika ya mashariki tulikuwa tukila Iddi siku moja?

Mheshimiwa Rais, Yaani Tanga iliyo karibu na Mombasa isiwe Iddi wakati mwezi umeonekana Kenya kweli hii inakubalika katika mantiki?.

Mheshimiwa Rais, inasemekana mwezi hata ukionekana mahali hapa nchini, na hata viongozi wa kidini wakitoa taarifa zao kwa viongozi wao wakuu wanaogopa kutoka hadharani na kuzifanya zienee kwa kuhofia nafasi zao za kiutawala ndani ya BAKWATA

Mheshimiwa Rais, hili suala la mwezi nchini limegeuka suala la kuflex muscle, yaani kutunishiana msuli baina ya waislamu wenyewe kuwa ni nani ambaye waislamu wengi wanamfuata zaidi, na hapa BAKWATA huwa ndo hupata nafasi ya kuonyesha taasisi nyingine kuwa sisi ndiyo sisi na waislamu wanatusikiliza sisi!

Mheshimiwa Rais, nakuomba kesho usihudhurie baraza hili la Iddi ili kutuma meseji kuwa huna mchezo kwenye mambo ya Mwenyezi Mungu na wasikuingize katika mitihani ya kumuasi Allah sababu tu ya "ulua"wa kidunia.

Asante sana
 
Ndiyo nimetoka kumpatia mhe rais risala ya waislam itakayosomwa kwenye baraza la Idd yeye akiwa mgeni rasmi. Kwahiyo ombi lako limechelewa Sana

By the way, BAKWATA ndiyo chombo pekee kinachotambuliwa na serikali kuwa ndiyo kinasimamia waislam wore nchini. Kama Kuna walio nje ya BAKWATA wanapaswa kuwa wapole tu.
 
Ndiyo nimetoka kumpatia mhe rais risala ya waislam itakayosomwa kwenye varaza la Idd yeye akiwa mgeni rasmi. Kwahiyo ombi lako limechelewa Sana

By the way, BAKWATA ndiyo chombo pekee kinachotambuliwa na serikali kuwa ndiyo kinasimamia waislam wore nchini. Kama Kuna walio nje ya BAKWATA wanapaswa kuwa wapole tu.
Tawile Tawile tawile
 
Yaani Bora ungemwambia asiende marekani angekuelewa kuliko kumkata kwenda huko.
nakumbuka kuna kipindi Samia alikuwa anatajwa Sana na redio KHER Kama kiongozi wa dini.
Zamani Sana hata kabla hajakuwa makamu
 
Una utani, asiende Marekani!

Unazijua Per Diem na Imprest za nje ya nchi wewe?
 
Kama Jiwe alishawahi kua mgeni rasmi katika baraza la Eid, why Samia asiende? Tusitake mijadala isiyo ya lazima katika petty issues

Ingawa mama anatakiwa awachane ukweli wanachofanya hao BAKWATA ni upimbi.
 
Ndugu Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Zilikuwepo taarifa hapa nchini kuwa Mwezi wa kuhitimisha mfungo mtukufu wa Ramadhani umeonekana katika baadhi ya maeneo nchini (Kagera ni mmojawapo) jioni ya tarehe 1/5/2022, Lakini viongozi wakuu wa BAKWATA hawakuutangazia umma juu ya ukweli huo wa muandamo wa mwezi.

Na minong'ono inayopita ni kwamba viongozi hao wa BAKWATA wanafanya hivyo kwa sababu wanataka tu watimize ratiba yao ambayo wameshaipanga toka mapema itakayowahikikishia uwepo wako wewe katika hadhara yao hiyo, Kwamba eti wakiitisha Iddi mapema basi mipango yao hiyo itaharibika.

Mheshimiwa Rais, Suala la Iddi ni suala la Ibada kubwa sana, na inafahamika vyema kwamba mtu kufunga siku ya iddi ni dhambi , Sasa iweje watu waahirishe Iddi ili tu ilimradi waweze kupata ratiba itakayomfit mkuu wa nchi kuhudhuria siku wanayoitaka wao?

Mheshimiwa Rais yawezekanaje nchi nyingi za Africa mashariki wanakula Iddi siku ya Tarehe 2/5/2022 ila tu eti sisi Tanzania tuwe tofauti wakati inajulikana vyema kuwa zamani katika Afrika ya mashariki tulikuwa tukila Iddi siku moja?

Mheshimiwa Rais, Yaani Tanga iliyo karibu na Mombasa isiwe Iddi wakati mwezi umeonekana Kenya kweli hii inakubalika katika mantiki?.

Mheshimiwa Rais, inasemekana mwezi hata ukionekana mahali hapa nchini, na hata viongozi wa kidini wakitoa taarifa zao kwa viongozi wao wakuu wanaogopa kutoka hadharani na kuzifanya zienee kwa kuhofia nafasi zao za kiutawala ndani ya BAKWATA

Mheshimiwa Rais, hili suala la mwezi nchini limegeuka suala la kuflex muscle, yaani kutunishiana msuli baina ya waislamu wenyewe kuwa ni nani ambaye waislamu wengi wanamfuata zaidi, na hapa BAKWATA huwa ndo hupata nafasi ya kuonyesha taasisi nyingine kuwa sisi ndiyo sisi na waislamu wanatusikiliza sisi!

Mheshimiwa Rais, nakuomba kesho usihudhurie baraza hili la Iddi ili kutuma meseji kuwa huna mchezo kwenye mambo ya Mwenyezi Mungu na wasikuingize katika mitihani ya kumuasi Allah sababu tu ya "ulua"wa kidunia.

Asante sana
Wanasiasa wanapenda mikusanyiko ili waoate jukwaa la kujimwambafai. Ataenda tu japo alupokua makamu sikumbuki kumwona mbele ya mimbari.
 
Kama Jiwe alishawahi kua mgeni rasmi katika baraza la Eid, why Samia asiende? Tusitake mijadala isiyo ya lazima katika petty issues
Hujaelewa mada.
Mada siyo kwamba asiende
Mada ni tuhuma za viongozi wa BAKWATA kutokutangaza muandamo halisi wa mwezi ili tu waweze kupanga ratiba zao za sherehe ya Iddi kitaifa kufuatana na ratiba ya upatikanaji wa rais ktk shughuli hiyo.
 
Kwani hawa viongozi wa BAKWATA mnawachagua kwa kuwapigia kura ?

Kama ni Ndio, basi msubirie sanduku la kura
 
Zilikuwepo taarifa hapa nchini kuwa Mwezi wa kuhitimisha mfungo mtukufu wa Ramadhani umeonekana katika baadhi ya maeneo nchini (Kagera ni mmojawapo) jioni ya tarehe 1/5/2022, Lakini viongozi wakuu wa BAKWATA hawakuutangazia umma juu ya ukweli huo wa muandamo wa mwezi.
Acha uongo na uchochezi
 
Naona ungemwambia aivunje Bakwata ingekuwa vizuri zaidi, kuliko kumwambia asiende huko halafu tatizo la msingi liendelee kubaki pale pale.
 
Back
Top Bottom