Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Hata masanja mkandamizaji kwenye hii nchi akigombea CCM anaweza kushinda........hamna jipya uchaguzi ukifika,TISS,polisi,wanajeshi,walimu wote wanaisaidia CCM ibaki madarakani maana ndio ulaji wao ulipo
waalimu ndio wanaotumika Kama kondom na hawapati manufaa yoyote zaidi ya vilio baada ya uchaguzi
 
KWA UBADHIRIFU HUO MKUBWA ALIOSEMA HADHARANI MHESHIMIWA RAIS
tunategemea barua za UTENGUZI haiwezekani Mheshimiwa Rais afike akute na kukiri Hadharani kuna UBADHIRIFU MKUBWA kisha wateule wake Waziri husika Mkurugenzi wa bandari nk wakabaki ofisini kwa awamu ya TANO ambapo Mheshimiwa Rais alikuwa Makamu wa Rais leo ndio ingekuwa mwisho wa wateule hao

Hapa Mheshimiwa Rais kwa kinywa chake kakiri kuwa kuna UBADHIRIFU mkubwa kwa tulivyozoea UBADHIRIFU ni kazi ya jeshi la polisi na TAKUKURU lakini hakuna hata mmoja pale bandarini kakabidhiwa kwa vyombo hivyo
Baada ya kusema kuna UBADHIRIFU mkubwa hakuna hatua zozote zilizosema na kiongozi mkuu kwa waliofanya UBADHIRIFU huo mkubwa
 
Ngoja tusubirie mkeka usiku wa MANANE
Halafu tusuburie waliohusika na UBADHIRIFU huo MKUBWA kuchukuliwa na vyombo vya DOLA hasa TAKUKURU na Polisi kwa hatua zaidi za kisheria

Pia kiongozi wetu mkuu kumwambia Waziri UTAKAPOSHINDWA njoo uniambie DADA NIMESHINDWA NITAANGALIA MWINGINE labda ataweza kunisaidia
Itachukua muda gani Waziri kwenda kwa dada yake kiongozi mkuu kuwa kashindwa miaka 5 au 10 ???
Kalamu ya kiongozi mkuu alosema imepotelea wapi..
WATANZANIA tumemkabidhi STATE MACHINERIES zote tunataka kuona MATUMIZI yake katika kulinda NCHI dhidi ya kila ikiwemo UHUJUMU Uchumi UFISADI UJAMBAZI UGAIDI
Hivyo tunataka vitendo kutoka kwa kiongozi wetu sababu yeye ndio MDHAMINI wetu namba moja wa mali ZA UMMA kwa niaba ya WATANZANIA WOTE.
 
Okay ndiyo maana hii kesi ya FAM ya kuonyogonyesha upinzani mapema,,alisoma alarm za nyakati
 
Acheni kumdanganya huyo mama,ukweli ni kwamba waTZ wanamchukia the way anavyo associate na mr.Msoga na kundi lake,huku akiwapa VYEO lukuki watu ambao Wana image chafu ndani ya jamii,Hivyo Basi yeye kama anahisi ni msafi Basi amekumbatia gunia la taka ambalo lazima nzi wamfate na anuke.

Wacheni muda utaongea tu
 
Kuna shida kidogo katika leadership skills. Sio kila kitu ni lazima raisi atamke hadharani. Raisi anaweza akawa anaoperate in shadow sababu anavyo vyombo vya kumtendea kazi aitakayo. Kama issue ya.mbowe kuna shadow operations ambazo bahati mbaya zinakuwa revealed everyday as the case hearing goes by.

Mkuu lazima awe bold and firm na awe na maamuzi magumu na sio story nyepesi. Ufisadi na gharama za maisha zilivyo wananchi hawawezi kumuelewa analalamika ufisadi wakati wananchi wanaumia na tozo,
 

Ikiwa Mama atataka kufanikiwa,Mambo yafuatayo ni lazima yafanyike.

Mosi,Katiba Mpya haikwepeki.
pili,Unda serekali yako hii ya sasa ilikuwa ya Mwendazake.
Tatu,Kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe futilia mbali inakuchafua na kuichafua Serekali yako katika kiwango ambacho hakivumiliki.Hii kesi mpaka sasa haina mashiko wala dalili zozote kwamba ugaidi ulikuwepo au ulitaka kufanyika.Hii Kesi ni michongo ya ACP Kingai na genge lake kutaka kupata ulaji zaidi Serekali hasa nafasi ya IGP.
Nne,Miradi yote mikubwa eg SGR,Ununuzi wa ndege,Uzalishaji wa umeme ifanyiwe tathimini upya.
Tano,Suala la muungano litazamwe upya eg 21% ajira ya WaZanzibar litazamwe upya huu ni upendeleo uliopitiliza.
Mwisho mama anatakiwa kuwa Rais wa JMT si Rais wa kuipendelea Zanzibar.
 
Naona Mijadala ni Kati ya sukuma gang Na Urojo gang endeleeni Na mijadala isiyo Na tija. Tunataka maendeleo kila mmoja awajibike kwenye nafasi yake.
 
Fikicha macho uondoe tongotongo wewe kibwengwo
Sukuma gang Bado hawaamini kinacho wakuta wamebaki tembelea mzimu wa jamaa dadeq watakwisha mwaka huu mama anaupiga mwingi kuwaondoa wote
 
Yeye mwenyewe mtu wa Magufuli pia, maana yake naye asifanyekazi na mwenyewe ahaha
 
Magufuli hakuwahi kuwa Dikteta sahihisha hapo. Samia atavuna anachopanda inaonekana moyoni hakuwa mwema na hakuwa na utiifu wa dhati kwa Magufuli.
Mkuu 'Galileo_Gaucho', mimi ndio leo nakusoma humu JF, kwa vile umeni'quote', sijapata kamwe hata siku moja kujuwa uwepo wako.

Sasa unaponiambia mimi nisahihishe nilichoandika mimi mwenyewe kwa ufahamu nisioutilia mashaka kabisa, nakuona wewe kama 'juha' (ashakhum si matusi, sina neno bora zaidi ya hilo).
Inawezekana sana, kwa elimu hizi za siku hizi uwe hujui maana ya hilo neno "DIKTETA", vinginevyo wewe utakuwa ni 'chawa' tu wa Magufuli aliyekuwa akikunywesha uchafu ili uweze kwenda chooni.
Usihangaike, sijibishani na watu wa aina fulani humu JF.
 
Angetuundia tume yakuchunguza kifo cha magufuli kidogo sisi sukuma geng tungemuuelewa,hiii kupita hivi kimya kimya na anashuhudia magufuli akinangwa na wapumbavu wachache na hasemi chochote tunaumia sana.tunamuona naye ni walewale
 
Kabisa.tujifunze zanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…