Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Hata masanja mkandamizaji kwenye hii nchi akigombea CCM anaweza kushinda........hamna jipya uchaguzi ukifika,TISS,polisi,wanajeshi,walimu wote wanaisaidia CCM ibaki madarakani maana ndio ulaji wao ulipo
waalimu ndio wanaotumika Kama kondom na hawapati manufaa yoyote zaidi ya vilio baada ya uchaguzi
 
KWA UBADHIRIFU HUO MKUBWA ALIOSEMA HADHARANI MHESHIMIWA RAIS
tunategemea barua za UTENGUZI haiwezekani Mheshimiwa Rais afike akute na kukiri Hadharani kuna UBADHIRIFU MKUBWA kisha wateule wake Waziri husika Mkurugenzi wa bandari nk wakabaki ofisini kwa awamu ya TANO ambapo Mheshimiwa Rais alikuwa Makamu wa Rais leo ndio ingekuwa mwisho wa wateule hao

Hapa Mheshimiwa Rais kwa kinywa chake kakiri kuwa kuna UBADHIRIFU mkubwa kwa tulivyozoea UBADHIRIFU ni kazi ya jeshi la polisi na TAKUKURU lakini hakuna hata mmoja pale bandarini kakabidhiwa kwa vyombo hivyo
Baada ya kusema kuna UBADHIRIFU mkubwa hakuna hatua zozote zilizosema na kiongozi mkuu kwa waliofanya UBADHIRIFU huo mkubwa
 
Ngoja tusubirie mkeka usiku wa MANANE
Halafu tusuburie waliohusika na UBADHIRIFU huo MKUBWA kuchukuliwa na vyombo vya DOLA hasa TAKUKURU na Polisi kwa hatua zaidi za kisheria

Pia kiongozi wetu mkuu kumwambia Waziri UTAKAPOSHINDWA njoo uniambie DADA NIMESHINDWA NITAANGALIA MWINGINE labda ataweza kunisaidia
Itachukua muda gani Waziri kwenda kwa dada yake kiongozi mkuu kuwa kashindwa miaka 5 au 10 ???
Kalamu ya kiongozi mkuu alosema imepotelea wapi..
WATANZANIA tumemkabidhi STATE MACHINERIES zote tunataka kuona MATUMIZI yake katika kulinda NCHI dhidi ya kila ikiwemo UHUJUMU Uchumi UFISADI UJAMBAZI UGAIDI
Hivyo tunataka vitendo kutoka kwa kiongozi wetu sababu yeye ndio MDHAMINI wetu namba moja wa mali ZA UMMA kwa niaba ya WATANZANIA WOTE.
 
Okay ndiyo maana hii kesi ya FAM ya kuonyogonyesha upinzani mapema,,alisoma alarm za nyakati
 
Leo kwa mara ya kwanza Rais Samia amekuja hadharani na kukiri wazi kuwa anaongoza serikali iliyogawanyika vibaya, amezungukwa na wasaidizi wanao mhujumu wazi wazi na yuko kwenye vita kali ya kuupambania urais wake kwa hali na mali. Hali ni tete mnoo kwake, na hatakubali!

Bila kumumunya maneno, wacha tuuseme ukweli ili kumsaidia Rais Samia popote alipo na ikibidi utafute njia ya kutokea.

Kwanza niweke wazi jambo moja kubwa na muhimu, kwa sasa Rais Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka makundi yote muhimu ya kijamii na kisiasa, yaani umechokwa. Hili halina ubishi na halihitaji takafari yote yote kubwa.

Kitendo cha mama Samia kuja hadharani na kukiri kuwa 'wenzake wanamzunguka' hivyo hatakubali! Hapo tunaona picha kubwa moja tu, maji yamezidi unga na mama Samia anahitaji msaada ili avuke.

Sasa kuna jambo moja kubwa pekee linaloweza kumuokoa mama Samia mahali alipo, hana ujanja inabidi alikimbilie. Kwa ufupi, jambo hilo ni;

Kutafuta muafaka wa kitaifa ili kuweza kuiunganisha nchi iliyoparaganyika vibaya kisiasa. Kama Samia hataweza kukaa na kumaliza tofauti zake na kundi kubwa la wafuasi wa Magufuli (sukuma gang) au wapinzani (hususani Chadema) basi ajue hawezi kutoboa. Hayo ndio makundi yenye nguvu kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, na kwa sasa yote mawili kwa pamoja (pasipo kuongozwa na mtu yoyote) yanasema wazi wazi kuwa mama Samia hafai, hatoshei kwenye kiti cha urais na hayamtaki tena. Huo ni uasi wa kisiasa.

Wakati ukuta, na majuto ni mjukuu, wenye hekima wameshaelewa!
Acheni kumdanganya huyo mama,ukweli ni kwamba waTZ wanamchukia the way anavyo associate na mr.Msoga na kundi lake,huku akiwapa VYEO lukuki watu ambao Wana image chafu ndani ya jamii,Hivyo Basi yeye kama anahisi ni msafi Basi amekumbatia gunia la taka ambalo lazima nzi wamfate na anuke.

Wacheni muda utaongea tu
 
Kuna shida kidogo katika leadership skills. Sio kila kitu ni lazima raisi atamke hadharani. Raisi anaweza akawa anaoperate in shadow sababu anavyo vyombo vya kumtendea kazi aitakayo. Kama issue ya.mbowe kuna shadow operations ambazo bahati mbaya zinakuwa revealed everyday as the case hearing goes by.

Mkuu lazima awe bold and firm na awe na maamuzi magumu na sio story nyepesi. Ufisadi na gharama za maisha zilivyo wananchi hawawezi kumuelewa analalamika ufisadi wakati wananchi wanaumia na tozo,
 
Leo kwa mara ya kwanza Rais Samia amekuja hadharani na kukiri wazi kuwa anaongoza serikali iliyogawanyika vibaya, amezungukwa na wasaidizi wanao mhujumu wazi wazi na yuko kwenye vita kali ya kuupambania urais wake kwa hali na mali. Hali ni tete mnoo kwake, na hatakubali!

Bila kumumunya maneno, wacha tuuseme ukweli ili kumsaidia Rais Samia popote alipo na ikibidi utafute njia ya kutokea.

Kwanza niweke wazi jambo moja kubwa na muhimu, kwa sasa Rais Samia amepoteza uungwaji mkono kutoka makundi yote muhimu ya kijamii na kisiasa, yaani umechokwa. Hili halina ubishi na halihitaji takafari yote yote kubwa.

Kitendo cha mama Samia kuja hadharani na kukiri kuwa 'wenzake wanamzunguka' hivyo hatakubali! Hapo tunaona picha kubwa moja tu, maji yamezidi unga na mama Samia anahitaji msaada ili avuke.

Sasa kuna jambo moja kubwa pekee linaloweza kumuokoa mama Samia mahali alipo, hana ujanja inabidi alikimbilie. Kwa ufupi, jambo hilo ni;

Kutafuta muafaka wa kitaifa ili kuweza kuiunganisha nchi iliyoparaganyika vibaya kisiasa. Kama Samia hataweza kukaa na kumaliza tofauti zake na kundi kubwa la wafuasi wa Magufuli (sukuma gang) au wapinzani (hususani Chadema) basi ajue hawezi kutoboa. Hayo ndio makundi yenye nguvu kwenye siasa za Tanzania kwa sasa, na kwa sasa yote mawili kwa pamoja (pasipo kuongozwa na mtu yoyote) yanasema wazi wazi kuwa mama Samia hafai, hatoshei kwenye kiti cha urais na hayamtaki tena. Huo ni uasi wa kisiasa.

Wakati ukuta, na majuto ni mjukuu, wenye hekima wameshaelewa!

Ikiwa Mama atataka kufanikiwa,Mambo yafuatayo ni lazima yafanyike.

Mosi,Katiba Mpya haikwepeki.
pili,Unda serekali yako hii ya sasa ilikuwa ya Mwendazake.
Tatu,Kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe futilia mbali inakuchafua na kuichafua Serekali yako katika kiwango ambacho hakivumiliki.Hii kesi mpaka sasa haina mashiko wala dalili zozote kwamba ugaidi ulikuwepo au ulitaka kufanyika.Hii Kesi ni michongo ya ACP Kingai na genge lake kutaka kupata ulaji zaidi Serekali hasa nafasi ya IGP.
Nne,Miradi yote mikubwa eg SGR,Ununuzi wa ndege,Uzalishaji wa umeme ifanyiwe tathimini upya.
Tano,Suala la muungano litazamwe upya eg 21% ajira ya WaZanzibar litazamwe upya huu ni upendeleo uliopitiliza.
Mwisho mama anatakiwa kuwa Rais wa JMT si Rais wa kuipendelea Zanzibar.
 
Naona Mijadala ni Kati ya sukuma gang Na Urojo gang endeleeni Na mijadala isiyo Na tija. Tunataka maendeleo kila mmoja awajibike kwenye nafasi yake.
 
Fikicha macho uondoe tongotongo wewe kibwengwo
Sukuma gang Bado hawaamini kinacho wakuta wamebaki tembelea mzimu wa jamaa dadeq watakwisha mwaka huu mama anaupiga mwingi kuwaondoa wote
 
Mnapokosea ni ile kusema ati asifanye kazi na watu wa Maguguli.I can tell you hapo mnakosea sana na mnataka kumwangusha.Wabunge wote waliyopo ni wa Magufuli.sasa unaposema ati asifanye kazi na watu wamagufuli what do you mean ?Hivi wakitaka kumwangusha si ni kupitisha azimio kule bugeni kuwa hawana Imani na Rais? What is so wrong akifanya kazi na watu wa Magufuli? Guys acheni kumpotosha rais wetu.Na akifanya vita na watu wa Magufuli vita hii itamshinda vibaya sana.Yawezekana kuna mahara JPM alikosea lakini makosa yake ni 5% ya mabaya yake compared to 95 % ya mazuri aliyoifanyia nchi hii.She better be careful na watu wa Magufuli. Mnapokosea etu watu wa Magufuli ni wasukuma.you are 100% wrong.

Hata wabunge wanaojifanya kuwa wanamchukia JPM wakati yeye ndiye aliyewapitisha na kuwanadi kwa waanchi,nao mwisho wao 2025.Nawashauri wafanye kazi kwa kufuata ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020 ,mambo mengini hayana faida kwa taifa letu.
Mama ukifanya vita na watu wa Magufuli iko siku watakurushia bomu la shutuma hutapona walahi.
Yeye mwenyewe mtu wa Magufuli pia, maana yake naye asifanyekazi na mwenyewe ahaha
 
Magufuli hakuwahi kuwa Dikteta sahihisha hapo. Samia atavuna anachopanda inaonekana moyoni hakuwa mwema na hakuwa na utiifu wa dhati kwa Magufuli.
Mkuu 'Galileo_Gaucho', mimi ndio leo nakusoma humu JF, kwa vile umeni'quote', sijapata kamwe hata siku moja kujuwa uwepo wako.

Sasa unaponiambia mimi nisahihishe nilichoandika mimi mwenyewe kwa ufahamu nisioutilia mashaka kabisa, nakuona wewe kama 'juha' (ashakhum si matusi, sina neno bora zaidi ya hilo).
Inawezekana sana, kwa elimu hizi za siku hizi uwe hujui maana ya hilo neno "DIKTETA", vinginevyo wewe utakuwa ni 'chawa' tu wa Magufuli aliyekuwa akikunywesha uchafu ili uweze kwenda chooni.
Usihangaike, sijibishani na watu wa aina fulani humu JF.
 
Uzuri wa watz huwa hawajali nani yuko madarakani na ni wa chama gani, wao wanachojali ni maisha yao yaende tuu.

Uzuri wa watz hawaandamani road ila huo msusio watakaokupa utajuta mwenyewe, utapigwa vita ya kidiplomasia ndani kwa ndani mpaka ukome.

Sasa mama walimuingiza chaka kwenye haya mambo:

1. Tozo za miamala
2. Kuwafurusha wamachinga
3. Mfumuko wa bei unaopanda kila mwezi hasa mafuta
4. Kubwa kuliko ni kesi ya ugaidi ya FAM, ambayo hata darasa la 7 anaona "hapa hamna kitu".
5. Kuendelea kufanya kazi na 90% ya awamu iliyopita.

Hayo mambo juu yasiposawazishwa 2025 % ya kushinda ni <20% hata atumie goli la mkono.
Angetuundia tume yakuchunguza kifo cha magufuli kidogo sisi sukuma geng tungemuuelewa,hiii kupita hivi kimya kimya na anashuhudia magufuli akinangwa na wapumbavu wachache na hasemi chochote tunaumia sana.tunamuona naye ni walewale
 
Ningelipata nafasi ya kumshauri Mama neno moja tu, ningemshauri ahamishie alichokifanya Karume Jr, afanye kampeni ya muafaka wa kitaifa, serikali ya umoja wa kitaifa, katiba ibadilishwe kuwapatia room wapinzani.

In that case, CCM itajihakikishia kubaki na wapinzani watajihakikishia nafasi ya ushiriki kwenye serikali.

Kuongoza watanganyika ni rahisi sana, coz wengi wao wanalilia maslahi tu! Agawe keki ya taifa kwa wote.
Kabisa.tujifunze zanzibar
 
Back
Top Bottom