Rais Samia usilalamike, unachokisikia ndio kinasemwa nchi nzima, kubali tu yaishe!

Kama hujui Hili kundi Lina kura zaidi ya asilimia 60 anzia Mwanza, Mara, Geita, Simiyu, Tabora , Dodoma, Shinyanga,Katavi, kigoma, Morogoro, Kagera unafikili hizo kura ni Chache?
Shida wengi hawaijui political demographics za nchi hiiiiiiiiii.Usichezee Kanda pendwa ni pendwa kwa sababu maalumu.Isye isye bana ng'weli isyeeeeee
 
chadema walimbeba kwa slogan ya mama anaupiga mwingi. mara paap akawalambua likofi la haja kwa kumkamata gaidi
 
Huu utopolo toka Denmark ungeachana nao. CHaDEMA walikuwa kimya!? Kwa dhuluma zote walizofanyiwa na makatazo ya shughuli za siasa za malaika jpm hiyo nguvu wangeitoa wapi!? Unadhani nao wan mioyo ya chuma isiyoogopa risasi , vifungo magerezani na hujuma za kiuchumi !?
 
Unaweza kuniambia hilo kundi unalosema la sukuma gang kiongozi wake ni nani na kwa akili yako km limejikusanya mpk likapata kiongozi wake.Serekali haimujui kumbuka Lowasa alikuwa na nguvu na yuko.hai alifanya nini.achen kucheza na Rais anamadaraka makubwa na hamuwezi.kumfanya chochote.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Hapo kuhusu wapinzni na hasa Mbowe amechemka sana.
Ila wapinzani wa ndani ya chama chake anawanyoosha.
Suala la MBOWE ili Maushungi apoze kundi Moja la MBOWE ni kumfutia mashitaka au Kama anaogopa kudhalilika ampige fine hata ya milioni kumi then amuachie huru tofauti na hapo Hilo kundi litammaliza kisiasa make Sukumagang tayari ameshakosana nalo basi ajitahid Chaggagang alirudishe kundini tofauti na hapo mama Wafa kisiasa
 
Na hao ndio wanaompotosha. Spana anazopigwa saizi ni kuchukia team ya Magufuli
 
Makosa ni sehemu ya maboresho ya taasisi yoyote ile. Ila hiyo haiondoi ukweli kuwa kwa sasa CCM haina uwezo tena wa kushinda kihalali kwa zaidi ya 2/3. Na haitakaa iweze tena kwani hiki sio kizazi cha ccm.
Mimi upinzani niliupenda sana tu hasa CHADEMA, Lakini siku Mwenyekiti alipobadili gia angani na kumpitisha mtu aliyesemwa sana na wapinzani kwamba ni fisadi kugombea uraisi, kuanzia siku hiyo nikakata tamaa na upinzani kabisa. Ya au mhhh.
 
Asante kwa uchambuzi wako kilichopo maadui wa mama wapo hukohuko ccm naamini upinzani hususani chadema wala hawana uadui na mama,karata imechezwa na maadui wake humohumo chamani kwake kumuongezea adui mwingine(chadema) Mungu mwema maza kastuka hajachelewa asafishe wote,ayajenge na upinzani mbona jk alifanyakazi na upinzani na alimaliza salama na mwisho awaletee katiba mpya watanzania atamalize ungwe yake vizuri.
 
Mpuuzi wewe kwa iyo Kagera, Mara, Dodoma na Morogoro kumejaa wasukuma??πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kweli nyie jamaaa ni washamba na wajinga sana!!

Na kwa ukabila wenu huo sahauni tena kushika madaraka ya hii nchi wajinga nyie
Lofa wewe huwezi kuzuia mafuriko kwa mkono, mdanganyeni mama yenu atajuta mwenyewe Sukumagang sio Wasukuma Kama unavyofahamu ni Magufuli followers wote ambao wengi wapo mikoa hyo kwan niliposema Dodoma uliamin Kuna Wasukuma? Kuna Kuna wagogo lakin ni Magufuli followers,
 
Zalemda you are right. Kujaribu kufanya tumuatimua kama huyo jamaa anavyo shauri kunaweza kuleta mitafaruku isiyo kuwa ya lazima. Rais aliyepita ameondoka madarakani kwa kifo, hivyo bado ana wafuasi wengi sana.
 
Hao sukuma gang ni wachumia tumbo wa JPM hawana msingi wowote wa sauti zao kusikilizwa na kuheshimiwa.

Ulikuwepo mtandao wa JK na Lowassa leo hii upo wapi?, ulisambaratishwa ukapotea.

Na wao watapotea mapema tu. Mama aendelee kujifungua ili makucha yake yawe kazini muda wote.

Apambanie maslahi ya Tanzania, haya makundi ni unafiki mtupu.
 
Kwani anahitaji kura ili avuke?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…