nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,035
- 2,938
Uko sahihi 100%.
Dkt Magufuli aliweza kuongoza vizuri bila kutegemea makundi. Hao wapinzani waliishiwa kabisa sera kwa sababu Dkt Magufuli alikuwa upande wa wananchi. Mama alichokosea kabisa kwanza ni kuafiki kwake bila kukemea Dkt Magufuli kutukanwa (Dkt Magufuli aliwa kukemea na kupiga marufuku kumtukana au kumkejeli Dkt JK). Lakini Mama akaenda mpaka kupiga picha na Mange mtu ambaye system inamchukulia ni msaliti maana hakuwa na jema kwa nchi. Pia Mama kakubali kuingizwa mkenge na wahuni wa kuwatungia jina la SUKUMA gang wale wote wanaoamini ktk uzalendo kwa nchi hii kitu ambacho alipaswa akemee haraka sana hizo kejeli. Alikubali watu wamdhihaki Dkt Magufuli kwa kumuita eti mwendazake etc. labda kama ilikuwa ni mfumo ili kupembua, ila ni muhimu sana tena sana yeye kutambua yeye na Dkt Magufuli ni kitu kimoja, na wananchi walikuwa wanamkubali sana Dkt Magufuli. Yaani ni kama Dkt JK 2005, yaani wananchi walipiga kuta kwa Dkt JK tu. Ndiyo maana Mama anapaswa ausome mchezo mapema maana wahuni wamemtengenezea matukio mabaya mabaya ili aonekane hafai (mfano lile la prof mkenda, machinga, kuchoma masoko, kutaka kulazimisha mgao wa umeme, kulazimisha mgao wa maji, chanjo ya korona na kutaka kulazimisha lockdown). Kikubwa tuungane kumuombea Mama aweze kuendelea na kushinda 2025.