Rais Samia usimuonee mtu aibu, mifumo ya Serikali inachezewa kwa makusudi

Kwani yeye Magufuli aliikuta hiyo mifumo imara? mwambieni mama aunde hiyo mifumo imara.

Si ameshaanza kuteua anaoona wanafaa kwenye uongozi wake, Tupo hapa tutaona huo uongozi mpya
 
Mkuu acheni kupotosha umma, andikeni mambo yanayo eleweka, mbona mnaandika ujinga mnawadanganya watanzania. Acheni kudanganya andikeni point zinazoeleweka.
Usipaniki.
Meko kufukuza watu wote wa JK ni kupotosha? Wewe umezaliwa leo?
 
Mama Samia anapaswa kujua kwamba, mifumo ya TEHAMA imechezewa makusudi ili upigaji uanze kama ilivyokuwa kabla Hayati Magufuli kuingia madarakani. Ilifikia wakati ukinunua umeme wa elfu kumi unapata tokeni ya thamani ya hiyo pesa lakini kinachokwenda Tanesco ni elfu NNE na zingine elfu SITA zinakwenda mifukoni mwa wajanja. Wameharibu mfumo ili wakorokochoe kuuweka ule wa kwao wa upigaji
 
Nilitaka kuonyesha kuwa hii mifumo huwa sometimes inapata changamoto..kuwa nyeti sio guarantee kuwa haitopata dosari...lakini pia sikatai kuwa inawezekana kuna wajanja wanataka kupiga hela za maintainance kwa kuchokonoa systems.
Ya true
 
Watu hawaeleweki kabisa wakati wa JPM mlisema amebana pesa sasa watu wanataka kuleta mzunguko wa pesa mitaani mnaanza kulalamika tena?! Madhara ya kutaka pesa zirejee mitaani ndiyo hayo sasa.
Ww unaeleweka, unataka kitu gani. Pesa ziwe nyingi au chache
 
Mbele ya njaa uaminifu unatokea wapi.
Waingereza walipozileta hizi system walishauri watumishi wapewe package Ili kupunguza au kuondoa tamaa.Lkn roho ya mswahili waijua
Umeongea point sana mkuu
 
Bado daladala kuanza kugoma, kafanana na JK kila kitu kasoro jinsia tu.
Tayari Kigamboni zimeanza kugoma.. SSH anahujumiwa kutokea nje ya mawaziri wake??
 
Mama anatakiwa afanye kama Meko..meko alifukuza watu wa JK wote.
yeye muach ewatammaliza kabisa hawa kenge hawana dogo wana roho mbaya kama meko
Nani alimchagua Mama? Kwanini awafukuze waliohangaika na Mwendazake kutafuta kura za ushindi??
 
Alaumiwe Magufuli kwa kuongoza nchi kama anaongoza familia yake badala ya kutengeneza mifumo imara
Hakuna wakulaumiwa pekee. Kila upande una madhaifu yake. Tulaumu kwa makosa mahususi.
 
Hata kipindi cha Magufuli mambo mengi tu yalikuwa yanaenda hovyo..sema watu walikuwa wanaogopa kusema
 
Ila Tanesco nao hawako 'serious' wanatoa Tangazo baada ya watu kupiga kelele Bungeni 'poor decision making', there are taking customers for granted. Kwenye hili tumejifunza kwamba tuwe na makampuni mengi ya kuzalisha umeme kwaajili ya upinzani
 
Ila Tanesco nao hawako 'serious' wanatoa Tangazo baada ya watu kupiga kelele Bungeni 'poor decision making', there are taking customers for granted. Kwenye hili tumejifunza kwamba tuwe na makampuni mengi ya kuzalisha umeme kwaajili ya upinzani
Watu bado wanaogopa kivuli cha mwenda zake, mambo k ama hayo hayakutakiwakuongelewa kipindi hicho
 
Napata wasiwasi na kuongezeka kwa sauti za kumtaka mama aendeshe nchi kwa hofu na ubabe ilihali. Mshaurini Mama aendeshe nchi kwa utawala wa sharia na mifumo.
 
Na likalemani bado lipo ofisini tu, leo Majaliwa kaamua wasimamishwe kazi hao ndezi wa tanesco likalemani lilisema wakae nyumbani siku kumi , tuna shida sana nchi hii
 
Hana huo ubavu, magu ndo alikua kila kitu bhana, Mama anademka tu na kiremba chake kama kiroba cha bangi

Hakika hakuna kama Magu. Sikutarajia kukukuta Mkuu ukivurumisha makombora pande hizi. Bila shaka Magu kakuvunjisha mwiko.

Lakini taratibu basi; mpe Mama muda wake. Hii sio nchi rahisi kuongoza. Haina misingi wala kanuni. Kila kiongozi na lwake. Aidha, si rahisi mtu kuigiza kashkash “unorthodox” za Magufuli; inabidi uwe “fyatu” kwanza.
 
mitizamo hii ndio inafanya matatizo hayaishi.

badala ya kudeal na tatizo kama lilivyo mnaanza ramli.
Kama ww umeona ni ramli chonganishi tujipe muda. Baada ya Bunge la Bajeti kumalizika kila kitu kitakuwa wazi.
 
JPM alifanikiwa kutimiza kazi zote kwa style yake, sasa mwambie huyo SSH na yeye atimize kazi kwa style yake, kama ni mipasho itafanya kazi kama kwenye kanga sawa, tunasubiri tuone hizo kazi tu...

Kwani alichofanya waziri Kalamani na MP Majaliwa kwa viongozi wa Tanesco hamjaona? mpaka Raisi aende hata ktk issue za luku.? huyu mama Samia anaelewa nini Maana ya Raisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…