Rais Samia usipende kila mara 'Kuingizwa Chaka' hivi bali shtuka mapema kwani unaniangusha sana tu

Rais Samia usipende kila mara 'Kuingizwa Chaka' hivi bali shtuka mapema kwani unaniangusha sana tu

GENTAMYCIME Rais Samia hakika amefanya kazi nzuri ya kuenzi kazi za watangulizi wake. Tatizo linalomsumbua ni mfumo dume. Yaani kuna vijeba vimejipanga kuhakikisha Rais Samia vinampatia info au data za uongo na akiziongea unakuwa ushahidi. Chukua tu mfano wa status ya uchumi wa Tanzania. Waziri wake wa fedha kasema tupo uchumi wa kati. Yeye wakamuandalia hotuba ya kusema eti tumeshashushwa na yeye kakiri kwa kinywa chake. Madhara yake nini? Ni kuwa ikija 2025 watasema hivi Rais Samia hafai kabisa kuongoza nchi kwa sababu tulikuwa uchumi wa kati na uongozi wake mbovu ulipelekea tukashushwa mpaka uchumi wa kati. Hata kama Mwigulu ni Muongo ila Rais Samia anadhani watanzania eti wapo naye, hapana. Rais Samia mpaka sasa hana mashabiki kabisa kila kona anatukanwa na kudhauriwa kwa kukosa uthubutu. In short Rais Samia anaonekana hafai kabisa na watanzania walio wengi wanamchukia kwa sababu wanaona ni msaliti wa maendeleo yaliyoasisiwa na Dkt Magufuli. Mi msimamo wangu ni kuwa Rais Samia ni kiongozi mzuri sana ila kazungukwa ma watu ambao inaoekana wanautamani urais wak

Mfumo dume tuliopewa na Mungu umehudhunika kwa sasa ndivyo wasemavyo wazee vijiweni
 
"Mtendaji Mkuu wa DAWASA ameniambia ukiacha hii hali ya ukame tunayopitia Dar es salaam upatikanaji wa maji upo asilimia 94. hii ina maana kwamba tupo karibu sana au tumeshafikia ile asilimia tuliyoelekezwa na CCM ya asilimia 95" - Rais

Chanzo: EATV

Mimi GENTAMYCINE siyo Mathematician kama Mkurugenzi wa NEC Poti wangu wa Kizanaki Dk. Mahera au Marehemu Profesa Ngowi ila kwa hii hii Hesabu yangu ya hapa na pale ( ya Kubahatisha ) ukisema 94% Maji yanapatikana hapa unamaanisha Jiji lote la Dar es Salaam sasa lina Maji, hatunuki tena Vikwapa na kwamba labda sehemu isiyo na Maji ndogo mno kama kusema Msasani Maandazi Road kuja mpaka usawa wa Namanga au Ada Estate.

Mama ( Rais ) una uhakika kuwa Mkoa wako huu wa Dar es Salaam sasa hivi upatikanaji wa Huduma ya Maji ni hiyo 94% uliyoitaja baada ya Kudanganywa ( Kuingizwa Chaka ) na hao ( hawa ) Dawasa?

Mama ( Rais ) una habari kuwa sasa unaenda Mwezi wa Pili huu Watu wa Ushuani ( Oysterbay ulikokuwa Unaishi ) na Masaki yote hadi kule anakoishi Mzee Wetu na Mwanadiplomasia Nguli ( Ngwena ) Salim Ahmed Salim na kwa Hayati Rais Mstaafu Mkapa hawana Maji?

Halafu Mama ( Rais ) upatikanaji wa Maji kwa Mkoa wa Dar es Salaam unahusiana nini na CCM yako? Kwahiyo wana CCM pekee ndiyo Wanaooga na wenye Shida ya Maji ila Wapinzani na Sisi Watu Neutral akina GENTAMYCINE ndiyo hatupaswi kuyapata na hatuyahitaji hayo Maji?

Binafsi huwa sipendi kabisa Kukusema kwani ukiachilia mbali kuwa Wewe ni Rais wangu ila pia ni kama Mama yangu vile hivyo ukiwa Unavapa ( Unakosea ) kila mara na Kuingizwa Chaka na Watendaji au Wasaidizi wako huwa najisikia vibaya sana tu.

Hali ya Maji Dar ni mbaya sana Rais!!!

Cc: bolivia
🤔🤔🤔🤔
 
Mi najiuliza kwanini wanaongelea Dar tu?

Lakini tatizo lipo mikoa mingi sana yaani hata mikoa inayotegemea ziwa Victoria tatizo la maji lipo na limekua endelevu toka msimu wa mvua mwaka jana.

Sasa hii mikoa inayozunguka ziwa Victoria tatizo ni nini?
 
Yooote tisa nipo nasubiria bill ya mwezi November maana October pia nililipa na maji sikuyaona hata siku moja
 
That's a totally unacceptable gesture and behaviour !! (If he was at all lying). Unless proven otherwise, such an act deserves a severe punishment (It's a mockery to all.....and inclusive).
You must be a certified and damn Fool.
 
Mi najiuliza kwanini wanaongelea Dar tu?

Lakini tatizo lipo mikoa mingi sana yaani hata mikoa inayotegemea ziwa Victoria tatizo la maji lipo na limekua endelevu toka msimu wa mvua mwaka jana.

Sasa hii mikoa inayozunguka ziwa Victoria tatizo ni nini?
Dar es salaam ndiyo Tanzania na ndiyo Ubongo wa Tanzania nzima na Watanzania wote tu Kifikra, Kimaamuzi na Kimihemko.
 
Jana wametumia Bajeti ya
Tsh million 500 kuandaa uzinduzi wa maji kigamboni wakati hiyo Bajeti ingetosha kuchimba visima 100 uswahilini kwetu huku
Hi inji ni failed state
Aiseeee!
😴😴😴😴😴
Halafu Rais Kagame mwaka 2013 alipomwambia Mtu Mmoja mkutanoni nchini Ethiopia kuwa anaongoza Maiti hakueleweka wakati wenye Akili Kubwa kama Yeye tulimwelewa na Kumuunga mkono.
 
Kwa nilivyoelewa hiyo taarifa ni kwamba kwa sasa Dar 94% wanapata maji, hii maana yake ni kwamba mifumo ya maji imeshawafikia kwa asilimia hizo. Mfano, umeme vijijini kufika umefika lkn sio kila nyumba itakuwa na umeme au kila siku utawaka.

Hapo wanamaanisha kama Dawasa watakuwa at its maxima level ya uzalishaji basi 94% watapata maji kwa wakati mmoja.

Hajasema kuwa wakati huu maji yanatoka na watu wanapata kwa asilimia hizo.

Kabla ya kupost chochote kaa chini uelewe hoja ni nini.

Si umeona amesama vyanzo vya maji vimepungua?

Hivyo wanaposema 94% wanapata huduma ya maji maana yake wanauwezo wa kupata maji kama DAWASA watafungulia maji at par.

Naomba kuwasilisha wanabodi.
 
Halafu Rais Kagame mwaka 2013 alipomwambia Mtu Mmoja mkutanoni nchini Ethiopia kuwa anaongoza Maiti hakueleweka wakati wenye Akili Kubwa kama Yeye tulimwelewa na Kumuunga mkono.
Mizukule ya kitanganyika inashangaza sana yaani,
Kuna taarifa mwaka juzi nilikua naangalia wakazi wa ukerewe wanashukuru wazungu flani kukamilisha mradi wa maji
Aibu niliona Mimi yaani miaka yote wamezungukwa na maji safi ziwani ila hawana mabomba aisee
Sasa Wagogo wa Idodomya watakuaje?
 
Kwa lile Tumbo lake kubwa kama Tenki la Maji Goba ulitegemea kabisa Akili zitajihifadhi Mwilini mwake?

Unamaana anatumbo kubwa kama simtank? Maana wenye matumbo makubwa wao wanawaza kujamba na kula muda wote, hasa mkiwa na kiongozi mwenye kitambi mjue kipaumbele chake sio kutatua shida zenu mjue anawaza kula na kujamba ndio shughuli zao, hata yule wa mawasiliano unadhani kwa tumbo lile atawaza bando za wananchi thubutu,
 
Tunachotaka ni quality na siyo quantity. Alichosema CEO pamoja na Comrade waziri inaweza kuwa kweli kuwa wameweka infrastructure ya kuwafikia 94% ya wakazi wa Dar es Salaam lakini in reality they can only provide/supply water to less than 30% ya wakazi wa Dar. Its better to not say anything than to seek political mileage. The CEO na Comrade Waziri should face the consequence.
 
Naunga hoja mkono, hali ni mbaya kwa dobi nguo kwa sasa naambiwa elfu moja kufulia maji baridi na miatano kwa nguo kufulia maji chumvi hali sio nzuri kabisa
Mkuu kwani kabla ya hii hali, nguo moja kwa dobi hspo Dar ilikuwa inafuliwa kwa bei gani?
 
Back
Top Bottom