Kwa nilivyoelewa hiyo taarifa ni kwamba kwa sasa Dar 94% wanapata maji, hii maana yake ni kwamba mifumo ya maji imeshawafikia kwa asilimia hizo. Mfano, umeme vijijini kufika umefika lkn sio kila nyumba itakuwa na umeme au kila siku utawaka.
Hapo wanamaanisha kama Dawasa watakuwa at its maxima level ya uzalishaji basi 94% watapata maji kwa wakati mmoja.
Hajasema kuwa wakati huu maji yanatoka na watu wanapata kwa asilimia hizo.
Kabla ya kupost chochote kaa chini uelewe hoja ni nini.
Si umeona amesama vyanzo vya maji vimepungua?
Hivyo wanaposema 94% wanapata huduma ya maji maana yake wanauwezo wa kupata maji kama DAWASA watafungulia maji at par.
Naomba kuwasilisha wanabodi.