Rais Samia, Usiruhusu wakugombanishe na umma

Mkuu katba nzr ni ipi?? Yaan toa mfano hyo katiba mpya unayo itaka iweje?? Eleza tu kwa lugha rahisi..
Mimi napenda nchi yetu iwe na katiba mpya, na isiyo na mafungamano kwa namna yoyote ile na ccm! Kwanini?
Kwa sababu katiba ya mwaka 1977 iliandaliwa mahsusi kwa ajili ya Tanzania ya chama kimoja, na tena cha kijamaa! Yaani ccm.

Ni katiba hii ndiyo iliyo kifanya chama cha mapinduzi kuwa chama dola, lakini pia ni katiba hii hii ndiyo iliyompa mamlaka makubwa Rais kiasi cha kumfanya kuwa Rais Mfalme (Imperial President).

Katiba mpya imependekeza kupunguzwa kwa mamlaka ya Rais! Na pia iliweka mazingira mazuri ya nchi kuwa na tume huru ya uchaguzi, kuliko hii ya sasa ambayo Rais wa nchi anamteua yeyote kuwa mwenyekiti/mkurugenzi wa tume! Hata kama ni mwanachama wa ccm! Ushahidi uko wazi!

Ni katiba hii hii inayotambua mpaka leo vyeo vya ulaji na tulivyorithi kwa wakoloni vya ukuu wa mikoa, wilaya, nk! Katiba mpya (na hasa ile rasimu ya Jaji Warioba) ililenga kupunguza matumizi mbalimbali yasiyo na ulazima serikalini. Mfano kupunguza ukubwa wa bunge, nk.

Leo hii tuna bunge kubwa na lisilo na tija yoyote ile. Tuna wabunge wa majimbo, wabunge wa viti maalum, wabunge wa kuteuliwa na Rais, wabunge kutoka Zanzibar, nk. Kwa ufupi tu, katiba mpya kwa upande wangu ina tija zaidi kuliko hii ya sasa ya mwaka 1977, ambayo kimsingi inaipendelea zaidi ccm na pia inawaongezea tu mzigo watanzania walipa kodi, kwenye uendeshaji wa serikali.
 
Inaonekana wewe hujui lolote kuhusu siasa..ni bora uende lile jukwaa la mapenzi kule. Suala la katiba mpya tayari Jaji Warioba alishamaliza kazi yake. Watu walitoa maoni yao yote pale. Tafuta rasimu ya Warioba usome. Usitusumbue humu
 
Wewe katiba mpya haikuletei ugali mezani, wananchi hatutaki siasa tunataka pesa.

Ila wewe huwezi kuelewa maana kila kitu anakuhudumia mumeo
Ungesema tu kuwa, wajinga wanataka pesa japo hawajui uhakika wao wa kupata pesa unategemea zaidi sheria zinazosimamia uchumi ambazo msingi wake ni katiba.

Katiba mbaya ndiyo iliyomwezesha marehemu kuwasotesha Watanzania kwenye ukata wa pesa.
 
Hivi wewe una kumbukumbu au huna?

Tume ya Warioba ilifanya kazi gani? Yaani huna hata ufahamu kuwa unachokiuliza, kilimalizwa na Tume ya Warioba?
 
Bahati mbaya, sijui kama huelewi au huna kumbukumbu.

Hivi Tume ya Warioba ilipokuwa inazunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi, na wakati anafanya summary presentation, ulikuwa umezaliwa au ulikuwa bado?

Wenzio waliokuwa wamezaliwa, waliambiwa vipengere vyote ambavyo wananchi walieleza kuwa vina matatizo kwenye katiba yetu, na wananchi wakapendekeza wanachokitaka. Waliyoyasema wananchi yalionekana wazi kuwa hayawezi kufanyiwa marekebisho bali yanalazimisha uandaa katiba mpya. Na Tume ya Warioba walieleza ni kwa nini marekebisho hayawezi kukidhi.
 
Hii mistari miwili, ina tofauti kati yake?

Chama kitajitangaza vipi bila kufanya siasa?

Chama kufanya 'campaign' in wananchi wakiunge mkono na kujisajili kwenye chama hicho, ina tofauti na Chama "kujitangaza" kwa wananchi?
Yeah kuna literal confusion in interpretating hiko kipengele ambayo kwenye mikutano inakuwa rahisi ku overlap from a to b.

Either way kujitangaza ni kuongelea mambo ya chama husika tu na kuelezea unasimamia nini.

Whereas political campaign ni kunadi sera, kuponda vyama vingine na utendaji wao na kwanini wasichaguliwe tena; hilo jambo haliruhusiwi.
 
Wanaodai katiba mpya sio wananchi ni wanasiasa.

Na unapodai katiba mpya sio conundrum ya kuku na yai (kipi kimetangulia duniani). Ideas zinaanza katiba iweje, then mchakato unaweza anzishwa.

Wahusika (wanasiasa) wanao push hii agenda sasa hivi wangekua wana highlight areas zinazo wasukuma kudai katiba mpya, mfano:

Ni mfumo gani wa decentralisation (ata kwa bara tu) wanataka utumike na kwanini uliopo unamapungufu based on management perpspectives.

Limitations zipi wanataka kuona kati ya viongozi na wananchi kwenye madaraka yao, wakionyesha mapungufu ya sasa.

Rights zipi za wananchi (realistically) uwezi kusema kila mkulima apewe hela ya pembejeo that is unrealistical.

Etc na mambo yanayotoa legitimising of powers, protection of freedom, government stability and so forth with the principles of national constitution.

Lakini uwezi kuamka asubuhi ukadai tu katiba ukiulizwa iweje unasema hujui tuwaachie wananchi; wananchi kweli wanajua mambo ya sheria au hata wamedai katiba?

Hili swala la constitution ni kupoteza muda ata kuli entertain ni usumbufu scrap kama alivyofanya Magufuli.

You can’t please everyone it’s impossible.
 
Hii ndiyo huitwa 'semantics'.

Sijui kiswahili chake itaitwaje!
 
Limitations zipi wanataka kuona kati ya viongozi na wananchi kwenye madaraka yao, wakionyesha mapungufu ya sasa.

Rights zipi za wananchi (realistically) uwezi kusema kila mkulima apewe hela ya pembejeo that is unrealistical.
Sijawahi kukusoma ukiwa na mihangaiko mingi kama leo; kuna jambo linakusumbua?

Unazunguka na wananchi kutojali uwepo wa katiba, kana kwamba katiba ni ya wanasiasa pekee?

Unataka nani asimamie kuhimiza jambo hilo kama siyo wanasiasa na Asasi zisizokuwa za kiserikali? Wananchi wataibuka tu kama uyoga na kujipanga kudai kuwa katiba iliyopo ina mapungufu, bila ya kuwepo na viongozi wa wananchi hao?

Ni mwananchi gani asiyejali haki yake ya msingi, ya kuchagua viongozi anaotaka wamuongoze? Uchaguzi (uchafuzi) unaofanywa kwenye hizi chaguzi, ambapo kura za wananchi hazina thamani yoyote, unadhani wananchi wanayafurahia hayo?

Kiongozi mmoja, anayejitwalia madaraka yote juu ya wananchi wake, wasiweze hata kumwondoa madarakani bila ya umwagikaji wa damu, wewe hapo unadhani hali hiyo ni ya kuwafurahisha wananchi wasitake uwepo kwa utaratibu unaopunguza /kuondoa hali hiyo?

Kwani wanasiasa ni akina nani, siyo hata hao walioko CCM wasoiotaka kusikia lolote juu ya katiba mpya?
 
Wanataka katiba mpya ili washinde uchaguzi na kuchukua dola ili wagawane rasilimali zetu kifisadi, imagine Sugu awe waziri wa elimu!
 
Sheria inasema mikutano ya kujitangaza na kusajili wanachama.

Sio mikutano ya kufanya campaign za siasa.
Hakuna nchi duniani ambayo kila wakati ni mikutano tu ya siasa na kusahau kunakujenga nchi...Katiba mpya ni muhimu ila nadhani labda its not a right time hasa kwakua cash is needed for that ambayo haijawa budgeted for na haikuwekwa kwenye ilani tuliyoipigia kura
 
kama ikitokea wizi wa mali ya umma na ubadhilifu ukarudi tena, au kujipatia fursa kwa hila na upendeleo balada ya fair process. Hilo litakuwa doa kubwa. Kuna mambo yakifanyika huwa yanaweza kuangusha falme hata kubwa kubwa, ikiwemo hili la rushwa na upendeleo
 
Hivi hao wananchi unaowasemea wewe umewahoji lini wakakwambia hayo unayoyaleta hapa?

Naona unasoma maoni, halafu hujui kilichoandikwa ni kipi kabla hata hujajibu; vinginevyo usingeandika haya uliyoandika hapa, kwa sababu nilishakupa mfano halisi wa upungufu wa katiba ya sasa, au unataka nirudie mara ngapi ndiyo uelewe.
 
I doubt if you have ever sat in a statistics class, if you did, it was a waste of your time.

Hilo swali lako halina maana yoyote, ndiyo maana ninalipuuza. Hujui taratibu zinazotakiwa kufuatwa katika kupata katiba mpya? 'Whether' ninaitaka ya Warioba au ya 'whoever', jibu langu litakusaidia kitu gani.

Polisi na watumishi wa umma kutumiwa kuharibu uchaguzi bado huoni uhusika wa katiba? Inaonesha kama 'jelly fish' ana ubongo wa kutosha kuzidi uliojaliwa na muumba wako, vipi?
Au hata hili la 'jellyfish' akili haitoshi kukuwezesha kutafuta huko 'google' anayo akili kiasi gani?
 
I am not gonna waste my time with you; sio mpaka nikwambie kiazi wewe nilichoandika statistically kina relation na trends analysis; do you know how that is important in decision making or concluding a research.
Hovyo kabisa.

Representative sample ya population ya watu zaidi ya 60 million, unakwenda kuitafuta mitandaoni, are you crazy?

Eti "kanuni za ku'control hayo mambo and legal ways", hizo sheria zinatokana na nini kama siyo katiba yenyewe. Kama katiba ni mbovu, sheria ndizo zitakazoirekebisha?

Sioni 'analysis' yoyote ya kupotezea muda na akili yangu katika maandishi yako yote hapa.
 
Sisi sio wajamaa tena katiba ya Kijamaa ya nini?
Hatuko kwenye Taifa la Chama kimoja tena katiba iliyotunguwa kukudhi matakwa ya chama kimoja itatufaa vipi?
Hatutaki katiba ambayo Rais anaweza kulivunja bunge na kulifanya bunge kuwa kivuli cha serikali tu.
Hatutaki katiba ambayo Rais anateua kila nafasi tena bila ushiriki wa bunge kuthibitisha.
Hatutaki katiba ambayo wananchi hawashiriki kuwachagua watu muhimu wanaosimamia maisha yao ya kila siku kwa ukaribu.
Hatutaki katiba ambayo unaweza kuwa na Sabaya na Bashite na usiwe na chochote cha kufanya zaidi ya kulalamika tu.
Hatutaki katiba ambayo kada wa chama asiye na uzoefu wa utumishi wa umma anaweza kuteuliwa Mkuu wa utumishi wa umma.
Hatutaki katiba ambayo mtu mmoja anaweza kuamua kodi za umma zinunue ndege au zijenge uwanja wa ndege kijijini kwake.
Hayo ni baadhi tu.Hiyo preamble soma wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…