Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Mimi napenda nchi yetu iwe na katiba mpya, na isiyo na mafungamano kwa namna yoyote ile na ccm! Kwanini?Mkuu katba nzr ni ipi?? Yaan toa mfano hyo katiba mpya unayo itaka iweje?? Eleza tu kwa lugha rahisi..
Kwa sababu katiba ya mwaka 1977 iliandaliwa mahsusi kwa ajili ya Tanzania ya chama kimoja, na tena cha kijamaa! Yaani ccm.
Ni katiba hii ndiyo iliyo kifanya chama cha mapinduzi kuwa chama dola, lakini pia ni katiba hii hii ndiyo iliyompa mamlaka makubwa Rais kiasi cha kumfanya kuwa Rais Mfalme (Imperial President).
Katiba mpya imependekeza kupunguzwa kwa mamlaka ya Rais! Na pia iliweka mazingira mazuri ya nchi kuwa na tume huru ya uchaguzi, kuliko hii ya sasa ambayo Rais wa nchi anamteua yeyote kuwa mwenyekiti/mkurugenzi wa tume! Hata kama ni mwanachama wa ccm! Ushahidi uko wazi!
Ni katiba hii hii inayotambua mpaka leo vyeo vya ulaji na tulivyorithi kwa wakoloni vya ukuu wa mikoa, wilaya, nk! Katiba mpya (na hasa ile rasimu ya Jaji Warioba) ililenga kupunguza matumizi mbalimbali yasiyo na ulazima serikalini. Mfano kupunguza ukubwa wa bunge, nk.
Leo hii tuna bunge kubwa na lisilo na tija yoyote ile. Tuna wabunge wa majimbo, wabunge wa viti maalum, wabunge wa kuteuliwa na Rais, wabunge kutoka Zanzibar, nk. Kwa ufupi tu, katiba mpya kwa upande wangu ina tija zaidi kuliko hii ya sasa ya mwaka 1977, ambayo kimsingi inaipendelea zaidi ccm na pia inawaongezea tu mzigo watanzania walipa kodi, kwenye uendeshaji wa serikali.