Rais Samia, Usiruhusu wakugombanishe na umma

Bunge la mkono wa jiwe ni la kijani, liwatetee hao wakulima na wafugaji.
Wanasiasa wanadai haki zao,

Wakulima, wafugaji na wafanyakazi hawana mtetezi.
 
Ziuzwe drimulaina zilipaki airport hiyo pesa iandakie katiba mpya.
 
Sisi sio wanasiasa na tunataka katiba mpya.
Wanasiasa ni wananchi pia wanaofanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria za nchi, wana haki ya kudai katiba mpya.
 
Huu ndio ulikuwa msimamo wa Bashiru wa zamani!
 
Nani alikufundisha wanasiasa sio wananchi??
 
Hayo yote hatajawahi kuondoka, kuna Mayanga construction, kuna mpwa kuteuliwa kuwa mkuu wa hazina, kuna ya Airport kujengwa kijijini kwa mtu mmoja.
 
Umesema kweli kabisa, lakini chama sio bendera mkuu ni watu wenye chama chao pamoja na ninyi mashabiki wa haki na siasa, chama kinahitaji kuungwa mkono na watu wote wenye uchungu na nchi yao, badala yake mnasubiri mfanyiwe na viongozi wa vyama, haiwezekani. Mfano mzuri ni harakati za ukuta mlivyoitwa barabarani nani alitokea?
 
Tunataka katiba ambayo bunge ndilo litakuwa na mandate yote ya kuchagua na kthibitisha vipaumbele vya nchi.Hatutaki katiba ambayo mtu mmoja anaweza kuamka akapiga simu akaagiza ndege kwa cash kutoka Ulaya, Hatutaki katiba ambayo mtu mmoja anaweza kuamka akaamuru pesa za walipa kodi BoT zikanunue korosho Mtwara.
 
Wala sio kosa kumsafisha mtu kama anatenda vizuri. Na badp ji wajibu wetu kumshauri pale inapobidi
 
Kazi kuu ya bunge katika mataifa yote ya demokrasia ya kweli ni kupanga kodi na matumizi yake pamoja na kutunga sheria nyingine na kuisimamia serikali kutekeleza hayo kwa niaba ya wananchi.Hichi ndicho kilikuwa mzizi wa vita iliyoundoa ufalme wa Uingereza kwenye makolini ya Marekani na ukisikia Government shutdown Marekani ujue ni Rais hakubaliani na bajeti iliyopitishwa na House of Representatives.
 
Wewe katiba mpya haikuletei ugali mezani, wananchi hatutaki siasa tunataka pesa.

Ila wewe huwezi kuelewa maana kila kitu anakuhudumia mumeo
kwani hiyo iliyopo inaleta ugali mezani? Umeambiwa tunatafuta ugali hapo? we need justice and rights that we deserve. Pamoja na kulaaniwa na kulaanika hadi jiwe na genge lake wanateketea bado hamjifunzi
 
Taifa linamiradi mingi ambayo ni very critical iliyoachwa na mwenda zake ambayo taifa letu litakapo yumba kuwalipa wakandarasi,taifa letu litaingia katika hasara na madeni makubwa kupindukia,
Sisi wananchi tunalielewa hili na Mh.rais wetu hatuwezi kugombana naye kwa sababu tunaelewa majukumu mazito aliyoachiwa ambayo ni lazima ayatimize,tumuache rais wetu kwa sasa.
Sisi wananchi tunakuunga mkono kwa RAIS wetu kwa 100%.
 
Mama Samia ni Rais, na alisha sisitiza hivyo, kwanini mnahisi yeye yuko pale kama roboti kwamba yanayofanyika anashauriwa vibaya na lawama hazimuhusu?

Ni kama kuonyesha yaliyofanyika awamu iliyopita pia hayamuhusu wakati yeye alikuwa makamu wa Rais, na amepata nafasi ya kuwa Rais kupitia hiyo.
 
Una point nzuri sana mimi ni CCM na mwana fikra huru. Mtazamo ama fikra yaweza kuwa katika namna ifuatayo.
1. Rais huyu ni Mchanga, Hakujiandaa, koti hili ni kubwa, ukomavu na ustahimilivu wa mawimbi ya kisiasa pia mchanga
2. Msingi wa malezi, tamaduni, dini si ule kuwa na hali ya kujiamini kwa kiwango cha nafasi hio na kuheshimiwa kikwelikweli katika muktadha mambo tajwa na wahusika wa mambo hayo tajwa.
3. Kipindi cha mpito cha Covid19 na cha Awamu yake si wakati muafaka kufanya hayo yenye mukari, haina ubishi mtake msitake haiwezekani atoke madarakani kwa taswira ya Rais wa Mitkasi never.
4. Msiojua Utulivu hasa kiulinzi na Usalama mtasumbuka sana. Strategically huu si wakati wa boat Tanzania kuyumba.
5. Hakuna mwaka uporaji wa kisiasa utakosekana ama matumizi ya dola. Namna mojawapo mjaribuni kwa kuitisha mikutano muone alivyoanza vizuri na utawala katiba na sheria.
6. Msiojua hali si shwari kiihivyo mjuavyo hasa katika msigano wa nguvu ya kimadaraka,e.g kivisasi, kimaslahi, kuelekea 2025, na e.tc
7. Mwambieni aimarisha Chama katika Mashina na Matawi katika ngazi hizi hamasa ya kuvuna na kuvuta wanachama na wapenzi iamke, Tuone viongozi wa CCM katika ngazi hizi waonekane viongozi na waheshimike, wapeni posho boresheni ofisi, amsheni mioyo iliokufa ya umaskini ya wanachama na viongozi.
8. Aruhusu walau Monthly Grassroot Political Mobilisation Campaigns. Hii inahitaji akili kubwa kisiasa na ustahimilivu.
9. Political Rapes and Defilements have devasting evils in economics terms more than they may think.
10. Nguzo yetu ni Uhuru na Umoja. Nashauri na napendekeza, salamu ya kitaifa ibadilike itumike hii " Uhuru na Umoja" kiitikio " Nguzo yetu", tunarudia kinyume chake " Nguzo yetu" kiitikio " Uhuru na Umoja"
11. Basi yote afanyayo yaakisi kuimarisha Uhuru na Umoja. Aachane na Nawasalimu kwa Jina la JMT ....Kazi iendelee waliomshauri hii slogan hawakuwa na expansive na Inclussive oriented thinking kwa wakati huo na hopefully hawakuwa na muda wa kutosha kwa jukumu hilo.
Nitapokea kwa moyo mkunjufu, wa kizalendo, wenye ukomavu na himilivu maoni na mtazamo kinzani= Diversity/ Variety is healthier than the opposite
 
Hivi wewe una kumbukumbu au huna?

Tume ya Warioba ilifanya kazi gani? Yaani huna hata ufahamu kuwa unachokiuliza, kilimalizwa na Tume ya Warioba?
Mkuu, unachoshangaa hapa si nilichouliza mimi hapo juu

Nisome vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…