Rais Samia, Usiruhusu wakugombanishe na umma

Rais Samia, Usiruhusu wakugombanishe na umma

Bunge la mkono wa jiwe ni la kijani, liwatetee hao wakulima na wafugaji.
Wanasiasa wanadai haki zao,

Wakulima, wafugaji na wafanyakazi hawana mtetezi.
 
Ziuzwe drimulaina zilipaki airport hiyo pesa iandakie katiba mpya.
Katiba mpya ni gharama siyo sawa na kuandika vitabu vyako uchwara vya kijasusi. Huwezi kuacha kutekeleza miradi ya kimkakati au kupelekea watu maji na umeme ukakimbilia kuandika Katiba Mpya kwa ajili ya kuwaridhisha watu fulani kwa maslahi yao ya kisiasa.

Kikwete alivyokubali mchakato wa Katiba mpya tuliona madhara yake, fedha zilitumika nyingi lakini pia baadhi ya watu hawakukubaliana na maoni ya wengi wakataka ya kwao ya wachache ndo yazingatiwe. Mwisho wa siku taifa likasimama, tukaingia kwenye mgogoro.

Uzuri Mhe. Rais anajua huu mchakato ulivyo kwasabbu alishiriki kikamilifu. Kwahiyo, anajua kinachokwenda kutokea ni KUPOTEZA MUDA NA RASILIMALI huku mambo mengi ya msingi yakisimama.

After all, mchakato wa Katiba mpya ulishakamilika na Katiba inayopendekezwa tayari ipo, kilichobaki ni kupigiwa kura tu. Sasa sijui kinachodaiwa hapa ni nini?

Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
 
Sisi sio wanasiasa na tunataka katiba mpya.
Wanasiasa ni wananchi pia wanaofanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria za nchi, wana haki ya kudai katiba mpya.
1)-Katiba mnataka nyie wanasiasa Mnahis labda ndo mtakuwa viongoz lkn sisi Wananchi Tunataka Maendeleo Na huduma za kijamii zpatikane...

2)-Mchakato wa Katiba enz za JK mliuharibu Nyie Ukawa mlipotoka Bungen..
Hakuna muda wa kupoteza pesa Zetu Wananchi..

3)-Kama Katiba Rais ataawaachia Wataalam washauri iweje Cyo Nyie Wanasiasa Njaa Mnaotaka Posho za Bunge la Katiba
 
Huu ndio ulikuwa msimamo wa Bashiru wa zamani!
Mimi napenda nchi yetu iwe na katiba mpya, na isiyo na mafungamano kwa namna yoyote ile na ccm! Kwanini?
Kwa sababu katiba ya mwaka 1977 iliandaliwa mahsusi kwa ajili ya Tanzania ya chama kimoja, na tena cha kijamaa! Yaani ccm.

Ni katiba hii ndiyo iliyo kifanya chama cha mapinduzi kuwa chama dola, lakini pia ni katiba hii hii ndiyo iliyompa mamlaka makubwa Rais kiasi cha kumfanya kuwa Rais Mfalme (Imperial President).

Katiba mpya imependekeza kupunguzwa kwa mamlaka ya Rais! Na pia iliweka mazingira mazuri ya nchi kuwa na tume huru ya uchaguzi, kuliko hii ya sasa ambayo Rais wa nchi anamteua yeyote kuwa mwenyekiti/mkurugenzi wa tume! Hata kama ni mwanachama wa ccm! Ushahidi uko wazi!

Ni katiba hii hii inayotambua mpaka leo vyeo vya ulaji na tulivyorithi kwa wakoloni vya ukuu wa mikoa, wilaya, nk! Katiba mpya (na hasa ile rasimu ya Jaji Warioba) ililenga kupunguza matumizi mbalimbali yasiyo na ulazima serikalini. Mfano kupunguza ukubwa wa bunge, nk.

Leo hii tuna bunge kubwa na lisilo na tija yoyote ile. Tuna wabunge wa majimbo, wabunge wa viti maalum, wabunge wa kuteuliwa na Rais, wabunge kutoka Zanzibar, nk. Kwa ufupi tu, katiba mpya kwa upande wangu ina tija zaidi kuliko hii ya sasa ya mwaka 1977, ambayo kimsingi inaipendelea zaidi ccm na pia inawaongezea tu mzigo watanzania walipa kodi, kwenye uendeshaji wa serikali.
 
Nani alikufundisha wanasiasa sio wananchi??
Wanaodai katiba mpya sio wananchi ni wanasiasa.

Na unapodai katiba mpya sio conundrum ya kuku na yai (kipi kimetangulia duniani). Ideas zinaanza katiba iweje, then mchakato unaweza anzishwa.

Wahusika (wanasiasa) wanao push hii agenda sasa hivi wangekua wana highlight areas zinazo wasukuma kudai katiba mpya, mfano:

Ni mfumo gani wa decentralisation (ata kwa bara tu) wanataka utumike na kwanini uliopo unamapungufu based on management perpspectives.

Limitations zipi wanataka kuona kati ya viongozi na wananchi kwenye madaraka yao, wakionyesha mapungufu ya sasa.

Rights zipi za wananchi (realistically) uwezi kusema kila mkulima apewe hela ya pembejeo that is unrealistical.

Etc na mambo yanayotoa legitimising of powers, protection of freedom, government stability and so forth with the principles of national constitution.

Lakini uwezi kuamka asubuhi ukadai tu katiba ukiulizwa iweje unasema hujui tuwaachie wananchi; wananchi kweli wanajua mambo ya sheria au hata wamedai katiba?

Hili swala la constitution ni kupoteza muda ata kuli entertain ni usumbufu scrap kama alivyofanya Magufuli.

You can’t please everyone it’s impossible.
 
Hayo yote hatajawahi kuondoka, kuna Mayanga construction, kuna mpwa kuteuliwa kuwa mkuu wa hazina, kuna ya Airport kujengwa kijijini kwa mtu mmoja.
kama ikitokea wizi wa mali ya umma na ubadhilifu ukarudi tena, au kujipatia fursa kwa hila na upendeleo balada ya fair process. Hilo litakuwa doa kubwa. Kuna mambo yakifanyika huwa yanaweza kuangusha falme hata kubwa kubwa, ikiwemo hili la rushwa na upendeleo
 
Tatizo mlimsifia sana mkasahau kama huyo ni kiongozi wa CCM, vyovyote iwavyo maslahi yake na chama chake lazima ayaweke mbele, sasa mnasubiri hisani toka kwake kwa kumbembeleza hata kama anavunja sheria wazi, mnatakiwa muamke sasa mjue ni njia gani mtaitumia kudai haki yenu, muache na ule ushamba wa mapambio yasiyo na maana.
Umesema kweli kabisa, lakini chama sio bendera mkuu ni watu wenye chama chao pamoja na ninyi mashabiki wa haki na siasa, chama kinahitaji kuungwa mkono na watu wote wenye uchungu na nchi yao, badala yake mnasubiri mfanyiwe na viongozi wa vyama, haiwezekani. Mfano mzuri ni harakati za ukuta mlivyoitwa barabarani nani alitokea?
 
Tunataka katiba ambayo bunge ndilo litakuwa na mandate yote ya kuchagua na kthibitisha vipaumbele vya nchi.Hatutaki katiba ambayo mtu mmoja anaweza kuamka akapiga simu akaagiza ndege kwa cash kutoka Ulaya, Hatutaki katiba ambayo mtu mmoja anaweza kuamka akaamuru pesa za walipa kodi BoT zikanunue korosho Mtwara.
Let’s just say unachanganya apples and pears.

Raisi/Serikali ina mandate ya kuchagua priority za nchi kama akiamua kununua ndege regardless of weaknesses on the decision by electing him we have bestowed him/her those powers.

Any president is not always going to make the best decision for the nation that’s why a constitution gives time to choose after a time.
The latter part in conclusion ni kwamba unazungumzia influence za raisi kwenye kusimamia uwajibikaji wa teuzi zake; I can agree there is a need of mechanimism to eliminate protectionism ya raisi. Lakini jambo hilo aliitaji katiba mpya but changing areas on how constitution could be amended.

Listen realistically katiba is an evolving document either codified or uncodified depending on the needs of a nation given the time; kwa sababu moja tu sababu za kuweka mambo kadhaa kwenye katiba zina badilika with time and evolution of several things such as morality and interpretation of rights.

Tatizo la watu wanaodai katiba mpya don’t have an argument zaidi ya kudai mpya wanaweza sema chochote before you know watakwambia we need a federal constitution kwa sababu US is doing so. Waulize sasa managerial system zake hawajui lolote zaidi ya kuleta fujo tu.

Mama anatakiwa kuifunga hii chapter akutakuwa na katiba mpya watanyamaza tu maana hiyo sio hoja ya wananchi.
 
Tatizo mlimsifia sana mkasahau kama huyo ni kiongozi wa CCM, vyovyote iwavyo maslahi yake na chama chake lazima ayaweke mbele, sasa mnasubiri hisani toka kwake kwa kumbembeleza hata kama anavunja sheria wazi, mnatakiwa muamke sasa mjue ni njia gani mtaitumia kudai haki yenu, muache na ule ushamba wa mapambio yasiyo na maana.
Wala sio kosa kumsafisha mtu kama anatenda vizuri. Na badp ji wajibu wetu kumshauri pale inapobidi
 
Kazi kuu ya bunge katika mataifa yote ya demokrasia ya kweli ni kupanga kodi na matumizi yake pamoja na kutunga sheria nyingine na kuisimamia serikali kutekeleza hayo kwa niaba ya wananchi.Hichi ndicho kilikuwa mzizi wa vita iliyoundoa ufalme wa Uingereza kwenye makolini ya Marekani na ukisikia Government shutdown Marekani ujue ni Rais hakubaliani na bajeti iliyopitishwa na House of Representatives.
You can do that but you have to remember sababu moja nchi zinakiongozi mkuu mmoja ni kwa sababu tunahitaji mtu wa kufanya decision kwa niaba ya nchi ya wote ipo ivyo duniani kote.

Kazi ya bunge ni kutunga sheria sio kumpangia raisi, wanachoweza kufanya ni ku challenge maamuzi ya raisi based on law. But then there is politics uwezi kuondoa factor hata bungeni maamuzi ya raisi kama yanabaraka ya wabunge wake and if they form the majority ni halali regardless of your feelings.

Tatizo lenu ni kulazimisha mambo nje ya siasa; mambo mengi mnayo mlaumu nayo JPM ni ya mfumo wa CCM kushinda katiba wakibariki wao inatosha that’s how party politics work.

Ni kama CDM walivyoamua Mbowe afanye atakavyo that’s part politics; the difference raisi is doing it national level. Sasa uwezi pangia maamuzi ya chama cha siasa wakishabariki.

Hila sakata la katiba ni waste of time; CCM wawapelekee jaji Werema sioni wa kujibizana nae kwenye constitutional law.
 
Wewe katiba mpya haikuletei ugali mezani, wananchi hatutaki siasa tunataka pesa.

Ila wewe huwezi kuelewa maana kila kitu anakuhudumia mumeo
kwani hiyo iliyopo inaleta ugali mezani? Umeambiwa tunatafuta ugali hapo? we need justice and rights that we deserve. Pamoja na kulaaniwa na kulaanika hadi jiwe na genge lake wanateketea bado hamjifunzi
 
Taifa linamiradi mingi ambayo ni very critical iliyoachwa na mwenda zake ambayo taifa letu litakapo yumba kuwalipa wakandarasi,taifa letu litaingia katika hasara na madeni makubwa kupindukia,
Sisi wananchi tunalielewa hili na Mh.rais wetu hatuwezi kugombana naye kwa sababu tunaelewa majukumu mazito aliyoachiwa ambayo ni lazima ayatimize,tumuache rais wetu kwa sasa.
Sisi wananchi tunakuunga mkono kwa RAIS wetu kwa 100%.
 
Mama Samia ni Rais, na alisha sisitiza hivyo, kwanini mnahisi yeye yuko pale kama roboti kwamba yanayofanyika anashauriwa vibaya na lawama hazimuhusu?

Ni kama kuonyesha yaliyofanyika awamu iliyopita pia hayamuhusu wakati yeye alikuwa makamu wa Rais, na amepata nafasi ya kuwa Rais kupitia hiyo.
 
Mh Rais, Kwasiku 100 ulizoongoza nchi zimekuwa za kutukuka sana, Taifa limepumua na kuonyesha mageuzi makubwa sana, Kwahakika nakupongeza sana sana, Umewathibitishia wazi unaweza kwa wale waliodhani huwezi kuongoza nchi.

Jambo la msingi leo naomba kuzungumzia kikao chako cha jana, ambapo nimesikiliza mazungumzo yako na Wahariri vya Vyombo vya habari nchini ambayo ni mazuri sana,

Pamoja na uzuri huo, Majibu yako kuhusu shughuli za kisiasa na mchakato wa Katiba Mpya yamenitia hofu huko tuendako kama kweli tutatibu tatizo la nchi ama tunafunika kombe la utawala uliopita.

Kimsingi jana tulitaraji utengue AMRI YA KIRAIS iliyotolewa na utawala uliopita kuhusu kusitisha shughuli za kisiasa (za wapinzani). Lakini pia tulitaraji utupe mwelekeo wa lini mchakato wa katiba mpya utaanza, Japo la Katiba ulilijibu lakini jibu lake limekuwa lilelile alilotwambia Rais Magufuli wakati anaingia madarakani.

Suala la shughuli za kisiasa ni la kikatiba na kisheria sio la hisani ya Rais, Nimelazimika kwenda kusoma sheria ya vyama vya siasa iliyofanyiwa marejeo 2019, kifungu cha 11, haki ya chama cha siasa kufanya mikutano ipo sio hisani ya mtu yoyote bali ni utekelezaji wa sheria tu.

Sasa rais wangu UMEAPA KUILINDA KATIBA NA SHERIA ZAKE, Ninakuomba sana, liangalie hili kwa umakini, huenda kuna wasaidizi wanakupotosha kuwa shughuli za vyama vya siasa zinakwamisha maendeleo, Hao wanakugombanisha na umma.

Watanzania sisi ukitaka tusikusumbue tuache tuongee, tulie na kucheka, tutanyamaza wenyewe, lakini sio utulazimishe tuongee, utulazimishe tulie wala utulazimishe kunyamaza. Kwahakika tutakusumbua kwelikweli, si jela wala mahakama havitatutibu. Shahidi utawala uliopita.

Labla nirejee nyuma kidogo, Msingi wa mpasuko wa taifa hili hadi kufika kuvuruga uchumi na mengineyo, ulitokana mwanzo kabisa kuzuia haki za watu kukutana na kutoa mawazo yao ambayo ni haki ya kikatiba na kisheria, Waliozuia walikuja na hoja hiyohiyo ambayo leo Rais umesema kuwa unanyoosha nchi.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alipoanzisha mchakato wa Katiba nchi ilikuwa hivihivi wala hakuwa na kigezo cha nchi imenyooka au imepinda, na alipoahirisha nchi ilibaki vilevile, Mchakato wa Katiba mpya hauwezi kuzua miradi ya maendeleo nchini wala hauwezi kukuzuia Mh Rais kuendesha nchi. Vivyo hivyo shughuli za kisiasa.

Katiba mpya ndio msingi wa mambo yote katika nchi, Tukipata katiba mpya itaondoa kazi ya kunyoosha uchumi wa nchi unayoifanya leo Mh Rais kwakuwa hakuna atakayekuja kuipindisha nchi tena.

Na Yericko Nyerere

View attachment 1834432View attachment 1834433
Una point nzuri sana mimi ni CCM na mwana fikra huru. Mtazamo ama fikra yaweza kuwa katika namna ifuatayo.
1. Rais huyu ni Mchanga, Hakujiandaa, koti hili ni kubwa, ukomavu na ustahimilivu wa mawimbi ya kisiasa pia mchanga
2. Msingi wa malezi, tamaduni, dini si ule kuwa na hali ya kujiamini kwa kiwango cha nafasi hio na kuheshimiwa kikwelikweli katika muktadha mambo tajwa na wahusika wa mambo hayo tajwa.
3. Kipindi cha mpito cha Covid19 na cha Awamu yake si wakati muafaka kufanya hayo yenye mukari, haina ubishi mtake msitake haiwezekani atoke madarakani kwa taswira ya Rais wa Mitkasi never.
4. Msiojua Utulivu hasa kiulinzi na Usalama mtasumbuka sana. Strategically huu si wakati wa boat Tanzania kuyumba.
5. Hakuna mwaka uporaji wa kisiasa utakosekana ama matumizi ya dola. Namna mojawapo mjaribuni kwa kuitisha mikutano muone alivyoanza vizuri na utawala katiba na sheria.
6. Msiojua hali si shwari kiihivyo mjuavyo hasa katika msigano wa nguvu ya kimadaraka,e.g kivisasi, kimaslahi, kuelekea 2025, na e.tc
7. Mwambieni aimarisha Chama katika Mashina na Matawi katika ngazi hizi hamasa ya kuvuna na kuvuta wanachama na wapenzi iamke, Tuone viongozi wa CCM katika ngazi hizi waonekane viongozi na waheshimike, wapeni posho boresheni ofisi, amsheni mioyo iliokufa ya umaskini ya wanachama na viongozi.
8. Aruhusu walau Monthly Grassroot Political Mobilisation Campaigns. Hii inahitaji akili kubwa kisiasa na ustahimilivu.
9. Political Rapes and Defilements have devasting evils in economics terms more than they may think.
10. Nguzo yetu ni Uhuru na Umoja. Nashauri na napendekeza, salamu ya kitaifa ibadilike itumike hii " Uhuru na Umoja" kiitikio " Nguzo yetu", tunarudia kinyume chake " Nguzo yetu" kiitikio " Uhuru na Umoja"
11. Basi yote afanyayo yaakisi kuimarisha Uhuru na Umoja. Aachane na Nawasalimu kwa Jina la JMT ....Kazi iendelee waliomshauri hii slogan hawakuwa na expansive na Inclussive oriented thinking kwa wakati huo na hopefully hawakuwa na muda wa kutosha kwa jukumu hilo.
Nitapokea kwa moyo mkunjufu, wa kizalendo, wenye ukomavu na himilivu maoni na mtazamo kinzani= Diversity/ Variety is healthier than the opposite
 
Hivi wewe una kumbukumbu au huna?

Tume ya Warioba ilifanya kazi gani? Yaani huna hata ufahamu kuwa unachokiuliza, kilimalizwa na Tume ya Warioba?
Mkuu, unachoshangaa hapa si nilichouliza mimi hapo juu

Nisome vizuri.
 
Back
Top Bottom