Wakuu !
Naandika uzi huu saa7 na dk 9 usiku baada ya kuwaza na kuwazua bila kupata majibu.
Kama tittle ya huu uzi inavyosomeka, wiki hii kumekuwa na video nyingi kwenye mitandao ya kijamii (YouTube, X, TikTok nk) zikionyesha jinsi Vijana wa taifa la Kenya wanavyomshambulia kwa matusi mazito raisi wetu Mh. Samia na Watanzania wengi tunatukanwa.
Najiuliza hivi kwanini Serikali yetu haijatoa tamko lolote kukemea haya maneno machafu yanayotamkwa na GenZ wa Kenya?
Ukimya huu unadhihirisha nini ?
Kwamba Watanzania ni kweli ni mambumbu, huduma za kijamii (Elimu, afya) zinazotolewa na serikali zipo chini ya ubora na viwango?
Watanzania hasa Wasanii ni kweli ni Mashoga ? ( Hakuna hata kanusho kwa Wasanii waliotajwa)
Ni kweli lugha ya kiingereza kwa Watanzania ni changamoto.
Watanzania wanaoishi Kenya wametukanwa sana. (Wachafu, ombaomba, wanafanya biashara za kuuzwa njururu, kahawa etc.
Na vitisho vya GenZ kwa mamlaka za Serikali yetu Parliament, Court na Ikulu) kuwa watavamia ipi mbona Msemaji wa Serikali hajatoka hadharani na kutoa tamko la Serikali ?
La kisikitisha ni yale matusi anayotukanwa raisi wetu, ukiachana na uraisi wake yeye ni Mama, Mke na binadamu mwenye moyo wa nyama. Wako wapi wale wanaomuimba Mama, Mama, Mama ? Wameshindwa kutoa kauli yoyote?
Kwa Ukimya huu, Je GenZ wameogopeka ? Au Serikali imeamua kunyamaza na kufunika Kombe ?
Hii ni dharau sana kwa Taifa letu. Pamoja na mambo ambayo yanayoendelea nchini kwetu Ifikie wakati Serikali itoe kauli ya kulaani na kukemea kauli zinazoendelea ku trend mitandaoni.
Wakati mwingine ufike wakati Viongozi wa Serikali muwe mnapata ridhaa ya wananchi sio kubebwa bebwa na Tume ya Uchaguzi na TAMISEMI. Tunatukanwa na Watoto wa nchi jirani na mmenyamaza hakuna kauli yoyote iliyotoka.
Ifikie wakati kama Taifa viongozi wa Serikali muwe na baraka za Wananchi sio michezo ya kupitishana bila baraka za wananchi.
Naamini kama mngekuwa na baraka za Wananchi hata Sisi Watanzania tungejibu hivyo vita vya maneno. Tena sisi Wabongo kwa maneno machafu tuko vyema sana.
Nawasilisha