PreGE2025 Rais Samia: Vyombo vya ulinzi na usalama msiruhusu watovu wa nidhamu (wanaharakati) wa nchi nyingine kuja kutovuka nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
𝐎𝐍𝐘𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐆𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐎𝐓𝐔𝐌𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐀 𝐊𝐔𝐇𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua za haraka kwa wanaotumia mitandao na teknolojia vibaya, akikemea pia wingi wa Wanaharakati kutoka nje ya nchi wanaojaribu kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania na kutaka kuivuruga amani.

Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salam leo May 19, 2025 wakati akizindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la 2024), ambapo amesema hatotoa nafasi kwa watovu wa adabu kutoka nje ya nchi kuja kujaribu kuvuruga amani, utulivu na usalama uliopo nchini Tanzania.

“Tusiwe shamba la Bibi kwamba Mtu anaweza kuja Tanzania akasema analolitaka, lipo Tanzania halipo, Watu wakajisemea tu, tumeanza kuona mwenendo wa Wanaharakati ndani ya Ukanda huu kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku, sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia, tusitoe nafasi walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika ni hapa kwetu, niwaombe Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutotoa nafasi kwa Watovu wa adabu wa nchi nyingine kuja kutovuka hapa kwetu, hapana”

“Nimeona clip kadhaa za kunisema, nipo bias na nini, ninalofanya ni kulinda nchi yangu na ndiyo wajibu wangu niliopewa, kwahiyo hatutotoa nafasi kwa kiumbe yeyote kuja kutuvurugia hapa awe yupo ndani ama anayetoka nje”

Katika maelezo yake, Rais Samia ameitaka Wizara na Maafisa wanaohusika kutoa ufafanuzi kuhusu yale yanayosemwa na Wanaharakati na Watu mbalimbali, kukanusha ama kuchukua hatua za haraka ikiwa yanayosemwa yana ukweli kuhusiana na sekta zao mbalimbali.
 
Attachments

  • VID-20250519-WA0009.mp4
    38.3 MB
zimwi la mwendazake linatafuna mnyororo.
 
Huyu zanzibar ana ugojwa wa akili . Kikweti ulaniwe na kizazi chako chote. Kuwezesha vichaa kuwa raisi ukifikiri watakufanya uonekane vizuri. Mimi nilifikiri baada ya kufanya makosa ya kumfanya mwendawazimu Magufuli kuwa raisi na watu kumia sana. Basi ugejuta na kujirudi lakini badala yake ukaleta mwendawazimu mwingine wa kike tena kutoka visiwani. Ipo siku kikwete na familia yako mtalipa damu za watanzania zinazo endelea kumwagwa.
 
Huyo ni 'mmama', tena wa kizanzibari. Hao wa mama wa ukanda huo ni wachambaji wazuri sana. Wakenya wamejaa kwenye mfumo wake anawachamba "ya kwao yamewashinda" ila hoja zao hawezi kuzipangua.

Sasa no reforms no election haichambiki na haipanguliwi kwa hoja hata akili iwe kubwa kiasi gani, 'mmama' wa watu hana namna zaidi ya kuikalia kimya na kuwasulubu watu kimyakimya
 
hotuba yake imeripotiwa na vyombo vya habari vya kenya na kuleta reaction kali kwa wananchi...tutarajie mdororo wa mahusiano hasa baina ya wananchi wa hizi mbili
 
Serikalini kuna mambo mengi, wenyewe wanakimbazana South Africa kwa matibabu kimya-kimya kila siku kwa jinsi wanavyowindana.

Kama hizo sio stress za kutosha, wakenya nao wanataka kuwa sehemu ya equation ya matatizo ya uongozi wake ‘spare a thought’.

Ila Kenya inavuka mipaka ya diplomacy, ni sawa vyombo vya habari vya Kenya kuja Tanzania na kuripoti,

Lakini majaji wastaafu wa Kenya hiyo ni no-no-no for diplomatic relations. Kwa upande wa wanaharakati wa Kenya kuja na kujifanya watetezi tena kuongea na media; huo ni uchokozi kwa serikali yeyote duniani.
Naomba niulize hivi FRELIMO kilikua chama cha wanaharakati au kikundi cha kigaidi?
 
Swali mbona kawai kujibu Hawa

Kwanini hoja zetu hazijibu?

Tanzania ni kisiwa? Je anashindwa Nini kujibu hoja za no reform no Election?

Samia mchawi ni wewe usimtafute kenya!

Wewe ndiye mchawi na serikali yako endelea kushupaza shingo you will be suprise!!!

GrUbMtJXYAI3aUy.jpeg
 
𝐎𝐍𝐘𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐆𝐄𝐍𝐈 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐎𝐓𝐔𝐌𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐀 𝐊𝐔𝐇𝐀𝐑𝐈𝐁𝐔 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐙𝐀𝐍𝐈𝐀

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua za haraka kwa wanaotumia mitandao na teknolojia vibaya, akikemea pia wingi wa Wanaharakati kutoka nje ya nchi wanaojaribu kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania na kutaka kuivuruga amani.

Rais Samia amesema hayo Jijini Dar es salam leo May 19, 2025 wakati akizindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la 2024), ambapo amesema hatotoa nafasi kwa watovu wa adabu kutoka nje ya nchi kuja kujaribu kuvuruga amani, utulivu na usalama uliopo nchini Tanzania.

“Tusiwe shamba la Bibi kwamba Mtu anaweza kuja Tanzania akasema analolitaka, lipo Tanzania halipo, Watu wakajisemea tu, tumeanza kuona mwenendo wa Wanaharakati ndani ya Ukanda huu kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku, sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia, tusitoe nafasi walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika ni hapa kwetu, niwaombe Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutotoa nafasi kwa Watovu wa adabu wa nchi nyingine kuja kutovuka hapa kwetu, hapana”

“Nimeona clip kadhaa za kunisema, nipo bias na nini, ninalofanya ni kulinda nchi yangu na ndiyo wajibu wangu niliopewa, kwahiyo hatutotoa nafasi kwa kiumbe yeyote kuja kutuvurugia hapa awe yupo ndani ama anayetoka nje”

Katika maelezo yake, Rais Samia ameitaka Wizara na Maafisa wanaohusika kutoa ufafanuzi kuhusu yale yanayosemwa na Wanaharakati na Watu mbalimbali, kukanusha ama kuchukua hatua za haraka ikiwa yanayosemwa yana ukweli kuhusiana na sekta zao mbalimbali.

Kwa amani ipi tulio nayo tuache vichekesho. Mama weka reform

View: https://youtu.be/m4nuMV-UjAA?si=xdvaH4k-9Mu5DYwK
 
Naomba niulize hivi FRELIMO kilikua chama cha wanaharakati au kikundi cha kigaidi?
Kiongozi

Hoja ulete wewe majibu nitoe mimi, umeona wapi.

Wewe ndio unielemishe sasa hao FRELIMO ni hakina nani. Maana hakuna sehemu niliyowataja.
 
Back
Top Bottom