PreGE2025 Rais Samia: Vyombo vya ulinzi na usalama msiruhusu watovu wa nidhamu (wanaharakati) wa nchi nyingine kuja kutovuka nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
nani anataka kuja kuharibu amani?

You guys are so delusional aisee
 
Ameshasahau kuwa Mwanaharakati Field Marshall John Okelo wa Uganda ndiye alileta uhuru Zanzibar?

Hata uhuru wa pili wa Tanganyika utaletwa kwa kushirikiana na wana Afrika Mashariki
Umeongea ukweli mama huyu shule ilimpoga chenga alipaswa kuyajua haya kabla ya kuzungumza
 
too late mama

wakenya wameshakuvua nguo zote!
 
Unawaza jambo ambalo kamwe halitokaa litokee. Anayeamini kama wewe eti ipo siku Samia atajiuzulu ana matatizo ya akili
Hoja yako ilikuwa nini ? Ulitaka pendekezo nini kifanyike sio?

Samia hatoweza kujiuzulu ndio ila 2025-2030 kwake itakuwa chungu Sana .hapo kisutu Tu kuna dimbwi hizo utadhani CCM wamenzisha kilimo cha vyura na samaki
 
Unajua maana ya mawakili wa kimataifa?
 
RAIS SAMIA: HATUTATOA NAFASI KWA KIUMBE YOYOTE KUJA KUTUHARIBIA NCHI YETU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezielekeza Wizara zinazohusika pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoa ufafanuzi au kukanusha haraka matamko mbalimbali yenye nia ovu yanayotolewa na wanaharakati mbalimbali dhidi ya Tanzania.

Rais Samia amezungumza hayo katika uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la 2024) uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo Mei 19, 2025.

"Tumeanza kuona mwenendo wa wanaharakati wa ukanda wetu kuanza kuingilia na kuvamia mambo yetu, sasa kama kwao wamedhibitiwa, wasije kutuharibia huku" - amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Samia amesema kuwa baadhi ya wanaharakati walishaharibu kwao, walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika, watu wako na amani, usalama na utulivu, ni hapa kwetu, hivyo tusitoe nafasi kwa kiumbe yoyote kuja kuharibu nchi yetu.
SAMIA: HATUTATOA NAFASI KWA KIUMBE YOYOTE KUJA KUTUHARIBIA NCHI YETU

Attachments

  • VID-20250519-WA1270(2).mp4
    16.4 MB
Linsongea kwa hasira na jazba nyingi Rohoni.

Unamfunga mtu kamiminiwa mvua Risasi

SHAME
 
Kweli watu wanabadirika, huyu ana kiburi na jeuri zaidi ya Magufuli

Ngoja tuone bila shaka hata EU watakazikwa kwa jeuri na kiburi

Wavhina na Wajomba wanatutosha siyo?
 
Rais wa mpito
 
Unajua maana ya mawakili wa kimataifa?
Ndio anakuwaje, huyo?

Anapewa kibali cha ku-prectice law bila ya β€˜jurisdiction’.

Embu tuwe serious saa zingine, ukiwa ndani ya Tanzania; you are subjected to Tanzania laws.

Serikali ya Kenya inatakiwa ku-defuse hii potential diplomatic rift, inayotaka kuletwa na raia wake wenye vihere-here.

Huyo msemaji wao na media zao ni muda wa kuwaeleza raia wa Kenya hasa wanaharakati ukienda Tanzania your subjected to their laws.

Hata hao wazungu wanawaonya kabisa raia wao, mnapoenda huko duniani wenyeji wanasheria zao.

Sio kukutetea udhalimu wowote, lakini rules are rules.
 
Wamepanick juzi kakayake Jk Upareni mazishi ya Msuya kayakoroga Leo dada anazidi

Albadili zinafanya kazi
 
Taa ya kijani hiyo… mwenye macho aambiwi tazama.
 
Kiongozi

Hoja ulete wewe majibu nitoe mimi, umeona wapi.

Wewe ndio unielemishe sasa hao FRELIMO ni hakina nani. Maana hakuna sehemu niliyowataja.
Umeleta hoja ya kuwa watu wengine kuingia nchi nyingine na kutaka kupata ushawishi kwa context hiyo ndio nikaitaja FRELIMO.

FRELIMO , mizizi yake ni watu wa Mozambique na iliundwa Dar es Salaam 1962 na makao yake makuu yalikuwa hapo hapo Dar es Salaam lengo kuu lilikuwa ni kupigania uhuru /ukombozi wa Mozambique.

Tukija katika point yangu kwanini nimeiweka FRELIMO, sababu Nyerere alisema hatuwezi kusema tuko huru na majirani hawapo huru.

Kwa sasa Kenya ndio nchi pekee iliyoonekana ni walau salama kwa Africa mashariki kupokea hata wakimbizi wa kisiasa waliokimbia vitisho vya tawala dhalimu.

Naweza kutoa mifano miwili tu ambayo ni kwa Lema & Maria Sarungi hata Lissu on transit akiwa katika matibabu alitokea Kenya , kwa zamani ni Oscar Kambona.

Sasa nikisikia unasema wanaharakati/wanasheria wanakuja kutetea mambo ya Tanzania ni kosa sijui unamaanisha nini hasa.

Martha Karua ni senior counsel ,ni member wa LSK na EALS kuja kusikiliza kesi ya uhaini kunakuwa na kosa gani?

Kama Tanzania tuliikomboa Mozambique kupitia Dar es Salaam kuna shida gani hao majirani wakija kusikiliza kesi na kutoa maoni yao kama wataalam wa sheria , Tanzania mnaficha kitu gani?

Mkileta hoja ya kuingilia uhuru inakuwa sio kweli sababu hawa watu wataruhusiwa kusikiliza na kutoa maoni hii ni haki ya kikatiba ila hawatohusika kutoa maamuzi.

Nauliza tena Tanzania mnachoficha ni nini kwenye hii kesi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…