PreGE2025 Rais Samia: Vyombo vya ulinzi na usalama msiruhusu watovu wa nidhamu (wanaharakati) wa nchi nyingine kuja kutovuka nchini

PreGE2025 Rais Samia: Vyombo vya ulinzi na usalama msiruhusu watovu wa nidhamu (wanaharakati) wa nchi nyingine kuja kutovuka nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Umeleta hoja ya kuwa watu wengine kuingia nchi nyingine na kutaka kupata ushawishi kwa context hiyo ndio nikaitaja FRELIMO.

FRELIMO , mizizi yake ni watu wa Mozambique na iliundwa Dar es Salaam 1962 na makao yake makuu yalikuwa hapo hapo Dar es Salaam lengo kuu lilikuwa ni kupigania uhuru /ukombozi wa Mozambique.

Tukija katika point yangu kwanini nimeiweka FRELIMO, sababu Nyerere alisema hatuwezi kusema tuko huru na majirani hawapo huru.

Kwa sasa Kenya ndio nchi pekee iliyoonekana ni walau salama kwa Africa mashariki kupokea hata wakimbizi wa kisiasa waliokimbia vitisho vya tawala dhalimu.

Naweza kutoa mifano miwili tu ambayo ni kwa Lema & Maria Sarungi hata Lissu on transit akiwa katika matibabu alitokea Kenya , kwa zamani ni Oscar Kambona.

Sasa nikisikia unasema wanaharakati/wanasheria wanakuja kutetea mambo ya Tanzania ni kosa sijui unamaanisha nini hasa.

Martha Karua ni senior counsel ,ni member wa LSK na EALS kuja kusikiliza kesi ya uhaini kunakuwa na kosa gani?

Kama Tanzania tuliikomboa Mozambique kupitia Dar es Salaam kuna shida gani hao majirani wakija kusikiliza kesi na kutoa maoni yao kama wataalam wa sheria , Tanzania mnaficha kitu gani?

Mkileta hoja ya kuingilia uhuru inakuwa sio kweli sababu hawa watu wataruhusiwa kusikiliza na kutoa maoni hii ni haki ya kikatiba ila hawatohusika kutoa maamuzi.

Nauliza tena Tanzania mnachoficha ni nini kwenye hii kesi?
Wanajificha kwenye kivuli cha amani lkn uoga wa kuachia madaraka ndio tatizo kuu la ccm.
 
Shukran kwa ufafanuzi wako.

FRELIMO walikuwa wa-Mozambique na sidhani kama walikuwa wanapewa hifadhi kwenda kupambana na democratic elected government.

Tuache hizi nasaha za kugombania uhuru siasa hizo zishapitwa na wakati.

Huyo Mkenya hana kibali cha jurisdiction ya ku practice sheria Tanzania, huo ndio uhalisia. Anapoingia Tanzania pia hana uhalali wa kushiriki siasa za Tanzania.

Ni hivi tuache ku-encourage undesired behaviour za wakenya kisa it suits our position kwenye matukio ya siasa.

Lissu ana anastahili fair trial yes 100% and public hearinng, wakenya wana uhalali wa kuingilia siasa zetu wakiwa ndani ya Tanzania no 100%. Waongelee huko kwao mambo ya Tanzania.

Na jinsi baadhi ya raia wao wanavyopenda mambo ya xenophobia tayari nimeona post mmoja anatukana watanzania wote.

Huyo dada anataka watanzania wafukuzwe Kenya na matusi kede kede na ana shauri wakenya warudi kwao (now huu sio mtazamo wa wakenya walio wengi) ni taahira mmoja tu.

Either way hii incident inaleta excuse kwa baadhi ya wakenya wenye psychological issues kuinua sentiments za nationalism na chuki zidi ya Tanzania.

Sasa kama wana akili timamu serikali yao inabidi ikiri hao wana harakati wao wanavuka mipaka ya rights za Tanzania na mbaya zaidi inatakiwa kuwakanya retired civil servants kuingilia siasa za Tanzania.

Wakenya wana utoto mwingi sana
Nikianza na kauli ya kusema tuache kuiona FRELIMO kama chama kilichotumia "base" ya Tanzania kujikomboa utakuwa unakosea maana historia ipo tuisome na ina tabia ya kujirudia.

Ukisema uhalali wa hii serikali kuwa ni "democratically elected" nadhani tutahitaji mjadala mwingine mpana zaidi maana tukitable hapa evidence ya yote yaliyofanyika sidhani kama ni serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.

Nikija katika hoja ya pili Martha Karua hakuja kupractice , amepractice kule Uganda kwenye kesi ya Besigye ambapo kwa mujibu wa sheria aliapply temporary practicing licence wakamnyima mara ya kwanza lakini baadae alipewa so alikuwa na jurisdiction na sio kwa kesi ya Lissu.

Kuhusu chuki , serikali yetu ndio imetengeneza chuki na wanawajibika kutengeneza mazingira, kwanini ? Jibu ni jepesi wao kama wanajumuiya wanapata uhalali wa mkataba ule kuruhusu freedom of movement katika jumuiya maana yake wanapata visa on arrival sasa kama wamefika kulikua na sababu gani ya kuwanyima kuingia na hawapewi sababu kwa makosa waliyofanya zaidi ya kunyimwa ruhusa?

Pia kama ni hivyo ni majuzi tu tumeshuhudia naibu katibu mkuu wa Chadema amekamtwa kabla hajasafiri na polisi wanasema amekuwa anatoka nje ya nchi mara kwa mara bila utaratibu je huo utaratibu ni upi mbona hawausemi ?

Serikali kwa kona kona zake inazalisha speculation na ndio chuki zinaanzia hapa.

Tukija katika hearing ya kesi kimsingi kesi hii hadi sasa haina fair hearing

Mosi tarehe 24 mwezi jana wafuasi wa Chadema na wanahabari wasiokuwa na silaha walipigwa vibaya na kujeruhiwa na polisi kwa kwenda kusikiliza tu kesi mahakamani hadi leo hakuna chombo chochote kimetolea maelezo sababu ya kuwapiga hao wafuasi na wanahabari.

Pili , Lissu alinyimwa haki ya kuongea na wanafamilia na mawakili wake na ilipotokea anapewa nafasi wanawekwa kwa umbali na polisi anakuwa karibu kusikiliza mazungumzo hii ni kinyume na taratibu kwenye kanuni ya natural justice.

Tukubali au tukatae Samia ana wasaidizi inept na ndio waliompotosha kuanzia ukamataji mpaka uendeshwaji wa kesi ya Lissu na hawa ndio wameifikisha hii chuki na bado wanazidi kumwaga mafuta zaidi kwenye moto bila kushtuka.
 
Kuingia nchi ya watu siyo lazima ukubaliwe na siyo lazima kupewa sababu ya kukunyima kuingia nchi husika. Mbona watu wengi tu hunyimwa kuingia USA na Ulaya na bila kupewa sababu yoyote?.
 
Wangelikuwa wanaunga juhudi na kusifu na kuabudu,tungelisikia "Kenya ni ndugu zetu ,mimi na brother Wllly ni kaka na dada!"
 
TANZANIA SIYO KISIWA, IMEKUWA KWA MUDA MREFU NA MASHIRIKIANO YA -,

Misaada ya kihali, utu, kisheria n.k imekuwa ni nguzo yetu kuwa Afrika Ni Moja:

Soma historia hii :

Denosa-Logo.png

337016181_737128954566375_6989782970395493772_n.jpg

DENOSA na wauguzi kukaribisha nyumbani mabaki ya mmoja wa Kundi la Wauguzi 20 wa South Afrika waliosaidia mfumo wa afya wa Tanzania baada ya uhuru warejeshwa airport ya OR Tambo Johannesburg Siku ya Haki za Kibinadamu (21 Machi).​

Machi 20, 2023 by Buyisiwes
PRETORIA - Shirika la Kidemokrasia la Wauguzi la Afrika Kusini (DENOSA) litakuwa miongoni mwa wauguzi wa rika zote katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chief Stuurman huko Gqebera mtawalia tarehe 21 na 22 Machi ili kukaribisha nyumbani mabaki ya mmoja wa wauguzi mashuhuri ambao walikuwa miongoni mwa wale walioitwa 'Kundi la Wauguzi 20 waliosaidiwa na wauguzi wa Afrika Kusini' uuguzi katika jimbo la Tanzania baada ya uhuru kwa amri ya Rais Julius Nyerere mwaka 1961 kufuatia kuondoka kwa wauguzi wengi wa Uingereza nchini humo.

View: https://m.youtube.com/watch?v=iv0kbQCN7ng
Dada Kholeka Rosemond Tunyiswa, aliyezaliwa tarehe 29 Novemba 1936, huenda asifahamike nchini Afrika Kusini alipoondoka nchini akiwa na umri wa miaka 25 na kuelekea Tanzania ambako alifanya kazi ya uuguzi pamoja na wauguzi wengine 19 ambao waliajiriwa kutoka nchini humo, pamoja na dada yake mkubwa, Edith Tunyiswa. Dada Kholeka alifariki jijini Dar es Salaam, Tanzania, tarehe 5 Machi 2023 akiwa na umri wa miaka 87.

Alizikwa katika hafla ya kibinafsi ya familia huko Dar es Salaam tarehe 6 Machi. Wakati aliolewa na ameanzisha familia nchini Tanzania mwaka 1967, mabaki yake yatarejeshwa Afrika Kusini na katika mji aliozaliwa, Gqebera, ambako alisajiliwa na mwanaharakati Govan Mbeki.

Mwili wake utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo saa 15h40 tarehe 21 Machi, siku ambayo nchi itakuwa inaadhimisha Siku ya Haki za Kibinadamu. Mabaki yake yataelekea nyumbani na kuwasili katika mji wake, Gqebera, Jumatano tarehe 22 Machi saa 13:20. Wajumbe wa DENOSA, inayoundwa na wauguzi wanaofanya mazoezi na wauguzi waliostaafu, watakuwa sehemu ya ujumbe utakaomkaribisha nyumbani kwake, wakiwemo wauguzi wa kizazi chake (wauguzi waliostaafu) kutoka katika kitongoji chake, Motherwell. Ibada ya kumbukumbu/mazishi yake yatafanyika tarehe 22 Aprili kama sehemu ya mpango wa serikali wa kujenga kuelekea Siku ya Uhuru nchini. Idara ya Sanaa, Michezo na Utamaduni itaongoza matukio kwa ushirikiano wa karibu na DENOSA.

Maelezo ya matukio:

Tarehe 21 Machi 2023 saa 15h40: Mabaki yake yatawasili pamoja na mwanafamilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa OR Tambo na yatakaribishwa na wajumbe wakiongozwa na Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nocawe Mafu, Nosipho Mshumpela (85) ambaye alikuwa mmoja wa Kundi la Wauguzi 20 walioondoka nchini na Kholeka, na kikundi cha wauguzi wa DENOSA le.

Tarehe 22 Machi 2023 saa 13h20: Mabaki yake yatawasili pamoja na mwanafamilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chief Dawie Stuurman huko Gqebera ambapo atakaribishwa rasmi na wauguzi, vijana kwa wazee, na atapewa ulinzi wa heshima na wauguzi kwa kuwa atakuwa akiwasili nyumbani kwa mara ya kwanza tangu aondoke.

Tarehe 22 Aprili 2023 saa 09h00: Ibada yake ya Kumbukumbu itafanyika Gqeberha kama sehemu ya mpango wa serikali wa kujenga Siku ya Uhuru.
USULI:

Mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru tarehe 9 Disemba 1961, wauguzi wengi kutoka Uingereza walirudi kwa wingi Uingereza, pengine kwa hofu au kutokuwa na uhakika kwa matarajio ya kuongozwa na serikali ya watu weusi wakati huo. Kuondoka kwao kuliacha pengo kubwa katika Tanzania mpya, jambo ambalo lilimfanya Rais Nyerere kuomba msaada wa Rais wa ANC wa wakati huo aliyekuwa nchini Tanzania, Oliver Tambo, kuwaleta Tanzania dada hao wa Afrika Kusini ili kufufua mfumo wa afya wa nchi hiyo.
Kutokana na ombi hili, Tambo anasemekana kutuma ujumbe huo Afrika Kusini. Hii ilikuwa wakati ambapo wauguzi weusi wa Afrika Kusini walichukizwa na Sheria ya Uuguzi ambayo ilikuwa ikilazimisha wauguzi wafundishwe kwa misingi ya rangi zao, ambayo ilikuwa ikianzisha ubaguzi katika taaluma.

Uajiri wa wauguzi wanaohitajika ulipaswa kufanywa kama operesheni ya chinichini kwani ANC na vyama vingine vya kisiasa vilipigwa marufuku. Mradi huu ulishughulikiwa na viongozi katika mikoa mbalimbali (kulikuwa na mikoa minne tu wakati huo). Govan Mbeki aliajiriwa katika Port Elizabeth (sasa Gqebera), Albertina Sisulu huko Transvaal, na Johhny Makhathini aliyeajiriwa huko Natal.

Waliondoka kwa basi kutoka Johannesburg kwenda Bechuanaland (Botswana), lililokuwa likiendeshwa na mwanafunzi mzungu kutoka Chuo Kikuu cha Wits ambaye alijigeuza kuwa kasisi aliyekuwa akiendesha wauguzi kwenye mazishi ya mwenzao huko Bechuanaland. Waliruhusiwa kupita na maafisa wa uhamiaji. Hivyo ndivyo safari yao ya kuelekea Tanzania ilianza, ambapo walipandwa katika vituo mbalimbali wakiwa wauguzi wakuu, wakiwafundisha wauguzi wenzao nchini Tanzania hadi ngazi za Wauguzi Taaluma. Pia waliwashauri wauguzi nchini kuunda Chama cha Wauguzi Tanganyika.

DENOSA na familia yake ya wauguzi wanajivunia mchango ambao wauguzi hao weusi wamechangia kwa moja ya nchi dada wenzao za Kiafrika wakati ambapo jukumu na uwezo wao ulikuwa chini ya mfumo wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini. Kikundi hiki kilitumwa kwa hospitali mbalimbali za wilaya nchini Tanzania katika mikoa kama Der es Salaam, Mbeya, Mwanza, Benguela na nyinginezo.

Wakati nafasi ya uongozi ya wauguzi hawa kabla ya kuwepo kwa DENOSA, hatuna shaka kwamba wao uharakati na fahamu zao zingewasukuma kuwa baadhi ya wanachama waanzilishi wa DENOSA kama wangebaki nchini.

Baada ya kuundwa kwa DENOSA mwaka 1996, shirika lilianzisha uhusiano na jumuiya ya wauguzi katika ngazi za kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuongoza uundaji na ukaribishaji wa Mtandao wa Wauguzi na Wakunga Kusini mwa Afrika (SANNAM), pamoja na kusaidia nchi kama Msumbiji na DRC kuunda Vyama vyao vya Kitaifa vya Wauguzi (NNAs).
 
Mama anaangushwa na watu wachache waliomzunguka huyu mama alikuwa MTU pia Sana na hakuwa na roho hii
Kwa nini unasema hakuwa na roho hiyo ! Huyo ni mnafiki na ni mtu mwenye kiburi ndo maana alikuwa anamsimanga sana JPM lakini mambo ndo yamemharibikia saba!
 
Kuingia nchi ya watu siyo lazima ukubaliwe na siyo lazima kupewa sababu ya kukunyima kuingia nchi husika. Mbona watu wengi tu hunyimwa kuingia USA na Ulaya na bila kupewa sababu yoyote?.
Mtanzania /Mkenya anahitaji visa kabla ya kuingia USA.

Mkenya anapata visa on arrival kuingia Tanzania hali kadhalika kwa mtanzania aingiapo Kenya sababu ni mkataba wa EAC hivyo mfano wako hapa hauna mantiki.
 
SI
Akizungumza Leo hii Mei 19, Kwenye Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la
2024) katika Ukumbi wa JNICC Jijini Dar Es Salaam. Rais Samia amesema wanaharakati waliodhibitiwa katika nchi walizotoka wasituharibie nchi yetu huku akivisihi vyombo vya sheria kuchukua hatua za haraka kila linapotokea jambo la uvunjifu wa Amani.

"Tusiwe Shamba la Bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka...lakini la pili tumeona mtiririko wa wanaharakati ndani ya region yetu hii kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku" ~ Rais Samia.

Pia soma
Si alishalitangazia Taifa ya kwamba KIFO NI KIFO TU.

Watanzania na haswa Watanganyika akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
  • Dislike
Reactions: UCD
Akizungumza Leo hii Mei 19, Kwenye Uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 (Toleo la
2024) katika Ukumbi wa JNICC Jijini Dar Es Salaam. Rais Samia amesema wanaharakati waliodhibitiwa katika nchi walizotoka wasituharibie nchi yetu huku akivisihi vyombo vya sheria kuchukua hatua za haraka kila linapotokea jambo la uvunjifu wa Amani.

"Tusiwe Shamba la Bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka...lakini la pili tumeona mtiririko wa wanaharakati ndani ya region yetu hii kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku" ~ Rais Samia.

Pia soma
Atawadhibiti wangapi? Ameua, amepoteza, ameteka, amefunga, anatisha, nk. Ila kila siku wakosoaaji wake wanazidi tu kuongezeka. Mimi nafikiri hivyo vyombo vya usalama vingetafakari kwanza hizo kauli zake ili kuepukana na maafa makubwa zaidi ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom