Rais Samia - Wachagga tupunguze matayarisho ya pombe kutokana na upungufu wa nafaka

John7371

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2018
Posts
2,994
Reaction score
6,676
"Niwaombe sana ndugu zangu wa Kilimanjaro, tupunguze kidogo matayarisho ya Mbege na vinywaji vingine kwa kutumia nafaka, tujue kwamba mwezi wa 10 hatukupanda, tutapanda Machi na kutakuwa na upungufu kidogo wa chakula,,"-Samia Source-Nipashe Tanzania.
 
Mtapangiwa hadi namna ya kutambika, mmezidi sana kujikomba na kujipendekeza
 
Kawaambia wanakilimanjaro au Wachagga tu?

Wachagga mkianzisha mada huwa mnasahau kuwa KLM inabeba pia Wapare na Wagweno wa Upareni na wahamiaji wengine.

Kichwa cha habari unasema Wachaga, ila ndani unazungumzia KLM yote.
 
Nadhani hawahitaji ushauri..., wanahitaji kipindi cha mazao mengi kuwe na soko la kutosha mazao yakipungua chakula kiletwe na kuuzwa kutoka ghala la taifa...

Kwani hatuna akiba kama taifa ? (Na kama hatuna ni uzembe wa nani) ?
Hii milio kutoka kwa Rais naona kama inaleta shida mno, au nchi ndo imeshaanza kukumbwa na baa la njaa na serikali inakimbia wajibu wake?
 
"Niwaombe sana ndugu zangu wa Kilimanjaro, tupunguze kidogo matayarisho ya Mbege na vinywaji vingine kwa kutumia nafaka, tujue kwamba mwezi wa 10 hatukupanda, tutapanda Machi na kutakuwa na upungufu kidogo wa chakula,,"-Samia Source-Nipashe Tanzania.
Unapokuwa mbele ya kadamnasi maneno mengine hutoka bila control.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…