CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Wasalaam,
Akiendelea na ziara yake jijini Mbeya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameendelea kusisitiza uwajibikaji kwa viongozi wote wa Serikali kuanzia yule wa chini hadi yule ya juu,
Rais ameenda mbali kwa kutumia msemo maarufu wa vijana "Wanikizingua Nawazingua " sasa wewe RC, DC, DED,DAS zingua kwenye 18 za mama uone,
Aidha Rais Samia amefurahishwa Sana na ujenzi wa Jengo bora la mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ( Value for Money )
Pamoja na mambo mengine Rais amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma na wahudumu,
Mtakumbuka Rais yuko Jiji Mbeya kwa ziara ya siku tatu huku akitarajiwa kufunga maonesho ya kibiashara ya "Nanenane" ambayo mwaka huu yanafanyika Kitaifa Mkoani Mbeya,
Rais pia hakusita kuwatahadharisha DCs, DED & DAS kuhusu mkeka mpya,