Rais Samia: Wale Waliokuwa Wanatugawia Shilingi Shilingi Hazipo Tena,Watu Wote Walipe Kodi

Rais Samia: Wale Waliokuwa Wanatugawia Shilingi Shilingi Hazipo Tena,Watu Wote Walipe Kodi

nadhani tunapaswa kuangalia matumizi zaidi, tunakopa 170bn za BRT za kununua buses 225, wakati mradi tumeubinafsisha kwa waarabu, hizi hela za kazi gani?

tunafanya uchaguzi kwa 775bn uchaguzi gani huo? tunaulizwa sgr itafika lini meatu tupakie ngombe tunakuwa wakali
 
hakyamungu kifo cha mafuru ni pigo. hii mipango ya hovyo sasa tunaanza kuiona, hivi tuambizane ukweli kilichowapeleka simiyu ni nini kama sio kufungua kiwanda cha gabacholi, tumeua jineri za ngulyati gangabili mwanhuzi nassa ngasamo kumpa upenyo ponjoro, tukiwaambia tunawadai mnakuwa wakali
 
Deni mkope Nyie kulipa tulipe Sisi? Idiots
View attachment 3375076
Kwanini alimshinikiza Job Ndugai kujiuzulu uspika ambaye alishauri kiungwana lakini akamfukuza kiaina na kumpachika kasuku wake?
1750266487786.png
 
Wanakugawia?.....Wakugawie kwa lipi ulilowafanyia?...au ndio mnabadilishana na rasilimali....otherwise ni mkopo..nothing for free!
 
My Take
Hakuna mjomba wa kukuletea maendeleo kila mmja awajinike kulipa Kodi

"Juzi nilizindua Jengo la TRA ndani ya Mkoa huu (Simiyu) nikawasifia sana TRA ndani ya Mkoa huu kwa kufikia malengo ya ukusanyaji, sasa nirejee wito wangu kwamba wafanyabiashara wote kodi kwa maendeleo ya nchi yetu na sio wafanyabiashara peke yao, hata sisi wenye biashara ndogondogo, wafugaji zile tozo zote tulizowekewa tuzilipe Halmashauri kwaajili ya maendeleo yetu.

Ulimwengu sasa hivi haueleweki, vita kila pahali, kila ukiamka ni vita kule ni vita huku, leo asubuhi tumeamka Iran huko na wenzao Israel wanatwangana kwelikweli. Wanapopigana kule madhara yanakuja kwetu, sasa hivi tu tutasikia bei za mafuta zimepanda,sasa hivi utasikia bidhaa zimepanda kwasababu wale ndiyo wenye nguvu, walioshikilia soko la dunia.

Tusipokusanya ndani lakini kwasababu ya vita vile, fedha ya kuletwa huku hakuna, wale ambao walikuwa angalau shilingi shilingi wakitugaia, fedha ile itakuwa hakuna. Ni lazima maendeleo yetu tujidhatiti sisi wenyewe, kwahiyo niombe sana na hii sio kwa Simiyu peke yenu, mikoa yote, Halmashauri zote zijitahidi kukusanya mapato.Niombe sana mjidhatiti kwenye makusanyo ili maendeleo yaende kama tulivyoweza kuyapeleka miaka mitano hii inayomalizika."- Rais Samia Suluhu akihitimisha ziara yake Mkoani Simiyu leo Jumatano Juni 18, 2025.
SAMIA uwe unasikiliza ushauri hawa wazungu kwa uwezo wako huwezi kuwakwepa,ww endelea kulea wezi serikalini ili uvune mabua.
 
Back
Top Bottom