Rais Samia: Wale Waliokuwa Wanatugawia Shilingi Shilingi Hazipo Tena,Watu Wote Walipe Kodi

Rais Samia: Wale Waliokuwa Wanatugawia Shilingi Shilingi Hazipo Tena,Watu Wote Walipe Kodi

My Take
Hakuna mjomba wa kukuletea maendeleo kila mmja awajinike kulipa Kodi

"Juzi nilizindua Jengo la TRA ndani ya Mkoa huu (Simiyu) nikawasifia sana TRA ndani ya Mkoa huu kwa kufikia malengo ya ukusanyaji, sasa nirejee wito wangu kwamba wafanyabiashara wote kodi kwa maendeleo ya nchi yetu na sio wafanyabiashara peke yao, hata sisi wenye biashara ndogondogo, wafugaji zile tozo zote tulizowekewa tuzilipe Halmashauri kwaajili ya maendeleo yetu.

Ulimwengu sasa hivi haueleweki, vita kila pahali, kila ukiamka ni vita kule ni vita huku, leo asubuhi tumeamka Iran huko na wenzao Israel wanatwangana kwelikweli. Wanapopigana kule madhara yanakuja kwetu, sasa hivi tu tutasikia bei za mafuta zimepanda,sasa hivi utasikia bidhaa zimepanda kwasababu wale ndiyo wenye nguvu, walioshikilia soko la dunia.

Tusipokusanya ndani lakini kwasababu ya vita vile, fedha ya kuletwa huku hakuna, wale ambao walikuwa angalau shilingi shilingi wakitugaia, fedha ile itakuwa hakuna. Ni lazima maendeleo yetu tujidhatiti sisi wenyewe, kwahiyo niombe sana na hii sio kwa Simiyu peke yenu, mikoa yote, Halmashauri zote zijitahidi kukusanya mapato.Niombe sana mjidhatiti kwenye makusanyo ili maendeleo yaende kama tulivyoweza kuyapeleka miaka mitano hii inayomalizika."- Rais Samia Suluhu akihitimisha ziara yake Mkoani Simiyu leo Jumatano Juni 18, 2025.
Mkaandaa vikundi vya kumtukana Magufuli mara o amekosana na wahisani wote hadi tunakosa hela,aya sasa yamefika wapi,Ww Samia ni wa kutuambia ss hivyo bado tunakumbuka ushenzi wote hatujasahau,mlisema mnajua kutafuta hela,Ss watanzania tunashangaa rafiki wa wazungu amekosana tena na wazungu,eti tulipe Kodi yamekuwa hayo tena,kwani wazungu wajomba zenu wamekufa,NDUGAI nae akaongea yakamkuta ya kuundiwa zengwe akafulushwa uspika.UONGOZI UNATAKA AKILI TIMAMU NA KUBWA vilaza hawawezi kuongoza nchi.
 
Ina vitega uchumi kila kona ya Nchi hii pamoja na Ruzuku nono na yenye Minofu iliyopo kisheria kabisa.
Halali wapi?Wakati fomu za washindani zinaporwa,ili kupita bila kupingwa pamoja na na tekateka juu?
 
Back
Top Bottom