Rais Samia: Waliosema nimeuza Bandari na Bahari faida yake ndio hii

Kitu kimeuzwa mlitaka kisipakwe mafuta??

Kwanini mnatutukana Watanganyika!?
 
Samia hafanyi maigizo,ambao hawapati faida Gawio la nini? Wanatoa wapi?

Na mama ndio alitumegea Siri kwamba hataki ule ujinga wa kampuni kukopa Benki na kutoa Gawio kama ilivyokuwa awamu ya 5.

Kwa kasi hii kumbe DPW watatufaa sana.Kama wamekabidhiwa rasmi bandari hata mwezi mmoja haujaisha wametoa gawio hilo,je baada ya mwaka mmoja itakuwaje.
 
kwani taarifa ya namna haiwezi kuwa "imepikwa?" kwa malengo yaleyale ya kui justify dpw
 
Hivi hizi Sarakasi si kuna kipindi walitwambia mpaka Fire walikuwa wanatoa Gawio ? Anyway tuache hayo...., Sasa kama Gawio limeongezeka, Watalii lukuki baada ya Royal Tour iweje Tozo hazipungui na kitaa maisha yanaendelea kuwa magumu kwa wabangaizaji ?
 
Aache uongo na usanii. Tunaofuatilia tunajua hao DP wanaopigiwa chapuo wala hawajaanza au ndiokwanza wanakabidhiwa shughuli. Kama kuna ongezeko la mapato ni zao la TPA inayoendeshwa bado na wazalendo. Hii pia inaonyesha kukiwa na usimamizi madhubuti wa serikali kwa bandari inawezekana kuwepo ufanisi bila kukabidhi bandari yetu kwa mwekezaji kama DP. Huyu ni mwekezaji nchi nyingi ameingia mikataba ya kilaghai kujidai anawekeza huku nchi husika imeshawekeza hela zake kibao kisha wao kutaka kumiliki kama bandari ni mali yao. Licha ya mifano mingi kama ule wa Djibuti sisi tumejiingiza kichwakichwa.
 
Kwa hiyo kakubali kweli aliuza, na nimesikia kasrma huu ni mwanzo tu.....😒
 
Soma maelezo ya Mbossso acha kuongea ujinga mnalishana na Nyumbu wenzio huko ufipa πŸ‘‡πŸ‘‡

View: https://www.instagram.com/p/C8Ht26kMeDf/?igsh=eWlxY2ljY3I3YnZ6
 
Wala huelewi kama gawio linatoka kwa kipindi fulani cha utendaji kwa mfano mwaka. Sasa uwekezaji gani miezi miwili mitatu kuwepo gawio. Usanii mtupu. Wewe ndio chawa wala hujui.
Soma maelezo ya Mbossso,usiniulize maswali ya kijinga au hujaelewa nini hapo?

Ushaambiwa DP World ameshawekeza hapo Toka walivyosainiana mkataba mwaka Jana unaleta stori za kipuuzi za huko ufipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…