Rais Samia: Waliosema nimeuza Bandari na Bahari faida yake ndio hii

Rais Samia: Waliosema nimeuza Bandari na Bahari faida yake ndio hii

DP World wameanza kazi mwezi April! Sina hakika kama wamezalisha kiwango hicho.
Mpaka leo Wastaafu wa TPA hawajapewa mafao yao! Gawio linarudishwaje?
 
..kwa hiyo hilo gawio tumepewa na DP world?

..bila DP world tulikuwa hatuna uwezo wa kupata gawio hilo?
Bandari tangu 2000 nije mjini nasikia inapigiwa kelele,kuanzia wizi wa mizigo ya watu mpaka uzembe kiutendaji,Kuna mkongo kontena la tv akakuta maboksi na nylons,siku zote hizo tija imekosekana,unakuja kuuliza Leo Hilo swali!!?
 
DP World wameanza kazi mwezi April! Sina hakika kama wamezalisha kiwango hicho.
Mpaka leo Wastaafu wa TPA hawajapewa mafao yao! Gawio linarudishwaje?
Inashangaza sana ... Ila ccm inatakiwa isome alama za nyakati. Hizi sio enzi za propaganda na uwongo . Na kama ccm bado inajiamini kwamba wataendelea na mazoea yao ya kuiba kura , 2025 watajua hawajui .
 
My Take
Mlisema Samia ameuza Bandari Kuna bango lenu hili hapa, ni spana tuu Kwa kwenda mbele.

Tafuteni hoja nyingine 👇👇

======

“TPA (Mamlaka ya Bandari Tanzania) mwaka jana (2023) nina hakika kiwango chenu hakikuwa hiki, lakini kwa mageuzi yaliyotokea bandarini mmeweza kufikia kiwango hiki na mwakani tunatarajia kiwango kikubwa zaidi pengine mara mbili yake ya hiki mlicholeta leo, hakuna sababu kama mtaendesha bandari na sekta iliyopo pale na pale kuna watu wawili ambao tumeshawaruhusu.

Mmeomba maombi zaidi lakini hata wale wawili mwakani mnaweza kuleta mara mbili ya hiki kiwango na huko ndiko tulikuwa tunaelekea ndugu zangu . Wale waliopiga kelele mama kauza bahari sijui mama kauza bandari mama kauza nini mama kauza..mauzo yale faida yake ni hii hapa leo, na huu ni mwanzo tutatarajia kutapata faida kubwa zaidi kwa bandari zetu zote kubwa ambazo zipo ndani ya nchi”- Dkt. Samia.

View: https://www.instagram.com/reel/C8E2TrhNxHA/?igsh=MWNhMXI1cWM2dGVvMQ==

Asijifanye hatuelewi tunaosema ameuza. Sisi tunataka usimamizi mzuri wa serikali wa mashirika na taasisi zake kwa tija bila kuwepo ufisadi. Hatuwezi kugawa kila kitu eti kupata hela nyingi wakati tunajua vigogo sasa wanakula na wawekezaji badala ya kula moja kwa moja. Lazima wananchi tuendeshe nchi yetu wenyewe kwa uadilifu. Tufaidi kwa wananchi kupata kazi na nchi kupata yenyewe faida.
 
Ndio maana unaona pesa zinamiminika ndio tafsiri ya ufanisi wa mashirika,huko mlikotoka hakuna kitu mlikuwa mnafanya
 
mbona mzigo unatetewa sana nakumbuka kuna yale magawio ya ttcl ila leo kiko wapi
 
TOKAAAAA MAREHEMH ASEMEE AMEFANYA MABADILIKOK KTK WAKURUGENZI WA MASHIRIKA NA MAKAMPUNI BAADA YA KUSIKIA KUNA BAADHI YA WAKURUGENZJ WANAKOPA BENKI PESA KUBWA KULETA KWENYE GAWIO WAKITESA WAFANYAKAZI KWENYE MALIPO KISA PESA ZA BENKI

SINAHAMUNAZO TENA HIZI GAWIO
 
Bandari tangu 2000 nije mjini nasikia inapigiwa kelele,kuanzia wizi wa mizigo ya watu mpaka uzembe kiutendaji,Kuna mkongo kontena la tv akakuta maboksi na nylons,siku zote hizo tija imekosekana,unakuja kuuliza Leo Hilo swali!!?

Suala hili liwekwe kwa uwazi zaidi.

TPA waripoti mapato yao.

DP world waripoti wanachotupatia.

Adani waripoti wanachotupatia.

Tukiwa na taarifa sahihi za hao watatu tutajua namna bora ya kuendesha bandari zetu.
 
Umeambiwa hawatoripoti?
 
Hakika Mwenyezi Mungu ametushushia Samia, eewe mama yetu ulishushwa na mola wetu mlezi, watu wanakuonea kijicho kwakua u kiumbe mtiifu wa allah. Samia to 2030.
 
DP World walianza kitambo, makabidhiano rasmi ndio yamefanyika mwezi Jana ila toka mwaka Jana DP World wapo kazini, waulize importers.
Mbona sijawahi kuona mabadiriko yoyote kuhusu kuwahi kutoka mizigo bandarini, nina zaidi ya miaka 3 napitisha mizigo yangu pale
 
..mbona bandari ya Mombasa wamekuwa wakifanya vizuri kutuzidi bila kujiuza kwa Dp World?

..kuna uwekezaji mkubwa ulifanyika wakati wa Jpm kwa kutumia mkopo wa World Bank je uwekezaji huo amechangia kiasi gani?

..uwekezaji ambao tuliambiwa Dp world atafanya haukuwa mkubwa kusema Tanzania haiwezi kukusanya nguvu yenyewe.

..maamuzi yameshafanyika kwa hiyo hakuna namna tena. Tuombe tu mambo yasije kuharibika mbele ya safari.
Kwani Kenya hawajaingia kwenye mkataba nao?
 
Back
Top Bottom