Thread 'Ndani ya muda mfupi Rais Samia amefanya kufuru, licha ya kuupiga mwingi sasa anakimbiza mwizi kimya kimya' Ndani ya muda mfupi Rais Samia amefanya kufuru, licha ya kuupiga mwingi sasa anakimbiza mwizi kimya kimyaKwani anachapa kazi? Mi naona anachanja mbuga tu, anatengeneza filamu ya utalii na mipasho mingi tu!!!
Hakikac tunaambiwa mjini ma mama ndo dili kwa sasa
Achana na mbumbumbu za ufipaSio kwamba katiba inasema Rais akitokea upande mmoja wa muungano makamu wa rais atoke upande wa pili wa muungano !!??
Tunyooooshe tunyoooshe Mamaaaa ....Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.
"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana
Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.
Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.
Alisema Rais Samia Suluhu
Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.
Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Kama ww si mwanasiasa na huna maslahi na siasa za upinzani pole sana kwa kazi uifanyayo🤣.Hii kauli amewadhalilisha sana wanaume kwa kujiona anauwezo na nguvu cha kufanya chochote kwa raia wa nchi-NO
Hakupaswa sana kuongelea nia yake ya uraisi huku akihusisha gender.huu ni ushahidi mwingine. mama uwezo wake ni mdogo vibaya sana. Sio level za Migiro
Hapaswi kuwa na hofu, yeye ndio raisi na ndio mwenyekiti wa chamaAmefanya vizuri kuwatahadharisha mapena wanaojikusanya kusanya vichochoroni huko.
Ha ha ha!!!!2025 rais Ni Gwajima,makamu wake Ni Polepole,Waziri mkuu Musiba.
Mkuu hata kama wataweka kivul upande wa pili au jiwe, nnauhakika watu watachagua jiwe au kivuli, hli kosa halitajitokeza Tena ktk nchi hii hata ccm wenyewe linawaumiza mnooooo..Hakuna cha mitano tena wala nini yeye amalize urithi wake asepe akacheze na wajukuu ufukweni huko!!!..Hatutaki tena raisi mwanamke kwenye nchii hii,Raisi unashindwa kuwa na maamuzi binafsi yaani unapangiwa cha kufanya mpaka raia wanashtukia mchezo mzima..Tunataka raisi mwenye misimamo wa kariba ya Magufuli(RIP)
Mgombea yeyote atakayewekwa hawezi kumshinda rais aliyeko madarakanikushinda kwake kunategemea upinzani wataweka mgombea gani
HayaHapaswi kuwa na hofu, yeye ndio raisi na ndio mwenyekiti wa chama
Nakunywa kvant kwanza nikilewa nakujaRais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.
"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana
Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.
Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.
Alisema Rais Samia Suluhu
Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.
Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Kama ulivyomnogea yule dhalimu mwendakuzimu hadi akataka kubadili katiba atawale mileleUrais umeshamnogea, anataka tena.