Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.

Alisema Rais Samia Suluhu

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Tunyooooshe tunyoooshe Mamaaaa ....
 
[emoji117]PEPO LA ULAFI WA MADARAKA shindwaaaaaaaaah..../
Ooooooh..../
Duuuh...../

[emoji117]NILIAMBIWA KUWA, MADARAKA YANALEVYA !!
NIMEANZA KUAMINI KITAMBO ILA LEO NATHIBITISHA RASMI....../

[emoji117]MAMA SAMIAH SHKAMOO..../
[emoji117]HIVI MAMA 2025, UTAKUWA NA UMRI GANI...../
[emoji117]MBONA WATAKA KUFIA MADARAKANI!!!!!!
 
Hakuna cha mitano tena wala nini yeye amalize urithi wake asepe akacheze na wajukuu ufukweni huko!!!..Hatutaki tena raisi mwanamke kwenye nchii hii,Raisi unashindwa kuwa na maamuzi binafsi yaani unapangiwa cha kufanya mpaka raia wanashtukia mchezo mzima..Tunataka raisi mwenye misimamo wa kariba ya Magufuli(RIP)
Mkuu hata kama wataweka kivul upande wa pili au jiwe, nnauhakika watu watachagua jiwe au kivuli, hli kosa halitajitokeza Tena ktk nchi hii hata ccm wenyewe linawaumiza mnooooo..
 
Na yeye amshajiona potential presidential candidate? huyu hata kama magu angemaliza muda wake hiyo nafasi ya urais angekuwa anaiota ndotoni tu, amalize tu ngekewa zake ili watu ambao wanaweza kuthibiti mamlaka ya nafasi ya rais waingie......naona kaanza kuwaingiza kingi wanawake.
 
CCM imuweke SAMIA kugombea?

Najua mara zote huwa inafanya dhuluma lakini sifa za mgombea aliyepo huwafanya angalau wapate hata 50% za ukweli alafu ndo waibe nyingine hata 20% Ili kujazia.

Kumuweka SAMIA itawaladhimu kuiba zaidi ya asilimia 60% ya kura Ili apite,kitu ambacho kitawaladhimu kutumia nguvu kibwa sana kuliko zile waliowahi kutumia huko nyuma na hapo ndipo tunaweza kuliingiza Taifa katika phase nyingine kabisa (maana kuna muda unapigwa tukio hata kuiba inabaki kuwa aibu) waangalizi ZAMBIA kama mfano, au ile nchi aliyowahi kuirithi Joyce banda.

Akisimama SAMIA 2025, kushinda kwa upinzani kutakuwa si kigumu tena, itategemeana tu na watakae msimamisha(asiwe LISSU), maana kuliuhalisia tangu 2015 CCM ilishachokwa watu walichagua mtu (Magufuli) na sio kwa mapenzi ya chama.

Nakumbuka uke muda JK anataka kutoka, iliafika muda hata mtu akivaa tu nguo ya CCM alikuwa anazomewa mitaani, Magufuli aliweza kuirudisha ila hadhi japo kwa uchache, na aliweza kwa kuwashika majority kwa ujenzi wake wa miundombinu huku akiwafinya minority.

SAMIA hafit, anyways huwezi jua labda mwisho wa CCM ndo unafika kwa style hii.
 
Hivi aoni ata live events zake watanzania hawana ata habari nae; yaani live views za mikutano yake huwa azifiki watu ata 150.

Ndio kwanza ana miezi sita wananchi washamchoka hawana jinsi tu. Bado ana miaka minne mingine zaidi ya kuwachosha.

Halafu anataka kuongeza na mitano mingine kwa kazi gani hii ya makangomano yake ambayo watu wanatumia hiyo nafasi kupiga.
 
Rais Samia Suluhu Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani Mkoani Dar amesema wanawake bado hawajamuweka Rais mwanamke bali aliyekuwepo amepatikana kwa kudra ya Mungu na matakwa ya katiba. Amesema walichofanikiwa wanawake ni kusukuma mpaka kumpata makamu wa Rais mwanamke.

"Kufika hapa, kama isingekuwa kudra ya Mungu ingekuwa ngumu sana, sasa ndugu zangu Rais mwanamke tutamuweka 2025. Mwaka 2025 tukifanya vitu vyetu vizuri, tukishikamana, tukimuweka Rais wetu, tutakutana hapa kwa furaha kubwa sana

Wameanza kutuchokoza kuandika kwenye vigazeti kwamba Samia hatasimama, nani kawaambia? Wanawake oyee. Fadhila za mwenyezi Mungu zikija mikononi mwako usiziachie.

Wanawake wamefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi hii, Wanawake tumefanya kazi kubwa kujenga siasa za nchi hii, tumebeba sana wanaume katika siasa za nchi hii, leo Mungu ametupa baraka mikononi, tukiiachia Mungu atatulaani.

Alisema Rais Samia Suluhu

Mengineyo, Rais Samia amesema ataendeleza mema yote katika awamu zote na watajitahidi kuongeza mema mengine.

Kuhusu usawa wa jinsia amesema hawajafika lakini wanawake wataendelea kuongezeka kwani asipofanya yeye hakuna ambae atafanya.
Nakunywa kvant kwanza nikilewa nakuja
 
Back
Top Bottom