Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Rais Samia: Wameanza kuandika kwenye vigazeti kwamba sitasimama 2025, nani kawaambia?

Nami namuunga Mkono Rais Samia Hassan Suluhu kugombea na kuteuliwa kushika ticket ya Chama cha Mapinduzi katika nafasi ya Urais hapo 2025.

Mungu atujaalie uzima kwa Jina lake Yesu Kristo!
 
UNAFIKI ni kitu kibaya sana si alipiga marufuku watu kutangaza kuhusu kugombea 2025? [emoji15]
Ndio hapo sasa, alisema kuhusu 2025 wasubiri mpaka huko baadae
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kwa utamaduni wa chama chetu, incumbent President hawezishindanishwa na mwanachama mwingine. Habari ndio hiyo. Cha msingi HE Hangaya kati ya sasa na 2022 apunguze watu wenye nguvu serikalini waliotokana na mwendazake hasa wale wafuasi wa tabia zake na ambao wanaonekana kutounga juhudi zake mama. Then come 2022 uchaguzi wa chama apate wajumbe 50% wake na kati ya hao apate wajumbe wake wa Kamati kuu. Sectretariat tayari keshasafisha. With JK in, deal done. Itabaki uso kwa uso tu na upinzani Hangaya anaoendelea kuuvuruga kidhuluma. All the best mama. Politics wallah!
 
Baada tu ya kusimikwa kuwa mtemi, mtemi Hangaya katangaza Nia lol mbona mapema?
 
Mama kuwa makini na haya mambo ya uchaguzi wa 2025....ni bora ukae kimya, unaweza kuyumbishwa kuelekea hiyo 2025 mpaka ukajuta....
 
Huyu mwanamke nae ana nyodo kweli.Ndo maana akaolewa mke wa tatu.

Wanawake wenzio wengi wanamkubali, wewe unakwama wapi dada!!!! Unataka uongozwe na rais katili?

Ukweli usemwe,,, Huyu mama imani yake pia imechangia kuwa na huruma, hofu ya Mungu, dhuluma hapendi, rais wa wanyonge/masikini na tajiri wote anawatakia mazuri.


Binadamu hamkosagi maneno,,, akifanya mabaya mutamponda, akifanya mazuli mutatafuta lolote lile baya ili tu aonekane mbaya.


1 Mwinyi✔
2 Kikwete✔ japo aliwaachilia sana walaji, but maisha yalikuwa poa mazee
3 Mama samia✔

Nyerere❌
Mkapa ❌
Magu❌
 
Wasalaam
Ndugu wanajamii mmesikia huko (wanawake wanaweza)..
Kwa ufahamu wangu na Mungu akitujalia Kwa haya ninayoona hakika 2025 ni Mama Samia

CCM oyeee,Mama oyeee sasa Kazi iliyobaki ni kuweka uwanja Sawa wa kidemocrasia..

Kwa haya ninayoona Kwa Kazi hizi Kwa muda huu mfupi kwakweli nitakua waajabu kama nisiposema
Samia 2025 twende

Nani kama mama hivi kuna linaloshindikana Kwa Mama, nimefurahi kwenye siku hii muhimu kuonyesha mwelekeo wako Mama Samia!!

Hongera Kwa uteuzi wa Mawaziri hawa wapya, tunasubiria wakuu wa mikoa na wilaya pia wakuu wa Idara Mbali mbali za serikali wabadilishwe,hawaendi na maelekezo na dira yako Mama!!
SO WHAT ???
 
Yupo sawa ni kudra za mwenyezi Mungu kuwapo hapo.

Sasa 2025 ndo wakati hasa wa kujipima kama mwanamke kugombea uongozi wa nchi.

Nami natumaini akizichanga vyema karata kipindi hiki mpk 2024, atapata kura kuanzia ndani ya chama mpaka kwa wananchi sie.
 
Hatutaki wezi wa kura wagombee urais 2025.Ni aibu kwa Taifa.
7nbv654311.jpg
 
Lakini katiba haimpi nafasi ya kugombea. Labda aibadili.
No,
Katiba inamruhusu kipindi kimoja kwa kuwa alichukua nchi ikiwa na zaidi ya miaka 4 ya kutawala,
Ingekuwa wakati anachukua imebaki miaka 3 basi angeweza kugombea tena vipindi 2
 
sasa mambo ya machifu na makabila si tulishayakataa huko nyuma!?
Sasa itakuwaje tuki,leta anayetokea kwenye machifu, si ataturudisha huko
 
Back
Top Bottom